Diallo: Rais ajaye awe dikteta mzalendo

tunduruboy

JF-Expert Member
Mar 16, 2013
423
218
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Dk Antony Diallo, amesema anatamani rais wa awamu tano awe dikteta, lakini anayepatikana kwa njia ya kura ili awatie adabu Watanzania.

Dk Diallo aliyasema hayo wakati akizungumza na watendaji wa ngazi za juu wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, katika kikao alichokiitisha kwa ajili ya kubadilishana mawazo ya namna ya kuboresha shughuli za jiji la Mwanza.

Mwenyekiti huyo wa CCM, alisema kuwa hivi sasa taifa linakabiliwa na tatizo la wananchi, hasa wanasiasa la kutotii sheria na kujiamulia mambo kiholela na hivyo kuleta hofu kwa wananchi.

"Ninatamani sana rais ajaye wa awamu ya tano awe dikiteta, lakini ambaye atakuwa amechaguliwa kwa kura na wananchi, ili aje atutie adabu, kwani taifa liko katika hali mbaya, kila mmoja ni mjuaji na yote haya yamekuwa yakisababisha uvunjifu wa amani," alisema Dk Diallo.

"Watanzania ni waoga sana, wakisikia mlio wa bunduki wengi watakimbilia uvunguni mwa kitanda, tunataka Rais ajaye awe dikteta ili ainyooshe nchi hii, kwani imefikia katika hali mbaya, kuna watu wanaichezea amani yetu na ni mabingwa wa kuhamasisha vurugu na wanazungumza mambo wasiyoyajua," alisema Dk. Diallo, ambaye pia amewahi kuwa Naibu Waziri na Wizara katika serikali za awamu ya tatu na nne.

Mwenyekiti huyo pia alisema kuwa sheria za nchi pia zinapaswa zitazamwe upya katika kuilinda nchi hii kuepuka kupata viongozi wasiofaa na kuitaka Idara ya Usalama wa Taifa kuhakikisha inaisaidia serikali katika kupata viongozi bora na wasio na kasoro.

Alisema kuna baadhi ya maeneo baadhi ya watu wamejipenyeza kugombea uongozi na kushinda, huku wakiwa si watu safi, hali ambayo inaiyumbisha nchi.

"Kuna baadhi ya wabunge na madiwani ni X Criminals, ni wahalifu sugu wamefanikiwa kushika nafasi hizo, hapa unatarajia nini na kuna kiongozi mmoja hivi sasa ni kiongozi wa chama cha siasa katika ngazi ya wilaya huyu siyo Mtanzania, tatizo hapa katika siku za karibuni vyombo vyetu vimelegalega," alisema Dk Diallo.

Chanzo: Mtanzania
 
tunduruboy said:
"Kuna baadhi ya wabunge na madiwani ni X Criminals, ni wahalifu sugu wamefanikiwa kushika nafasi hizo, hapa unatarajia nini na kuna kiongozi mmoja hivi sasa ni kiongozi wa chama cha siasa katika ngazi ya wilaya huyu siyo Mtanzania, tatizo hapa katika siku za karibuni vyombo vyetu vimelegalega," alisema Dk Diallo.
Oh yeah?

Kina nani hao ambao ni x criminals? Kwenye bold sitii neno mie
 
Hivi anataka ashuhudie udikteta gani zaidi ya kung'oa watu kucha, meno na kukata vidole? Kubambikizia watu kesi za kisiasa kw msaada wa vyombo vya dola ni jambo dogo?

Kweli si kila mtu anafaa kuwa kiongozi!
 
Hivi huyu kasoma? Ama udokta wa heshima.kila siku magamba na kauli tata,wacha kwa kauli hizo wajimalize
 
Angefafanua zaidi tumuelewe yuko wapi na anamlenga nani? Upinzani au huko gambani kwake? Ila serikali inaongozwa na magamba kwahiyo nchi imefika hapa kwa ajili yake yeye na wenzake huko CCM
 
Hakuzungumzia Uraia wa Katibu wake Mkuu? Mbona ni Raia wa Somalia? Kwa kweli CCM Ilipo fikia ni Ukingoni kabisa, kama Kikao cha Kuangalia Utendaji wa kazi kinageukam kuwa kikao cha Kuzungumzia Siasa basi kwisha kazi,
 
Kwa hili hata mimi nina muunga mkono kwa kiasi fulani. Ni lazima nchi kwa sasa ipate Rais ambaye ni mkali lakini anayesimamia misingi ya utawala bora.

Kama hatuwezi kupata Rais ambaye ni mkali basi ni lazima tuwe na waziri mkuu mkali. Historia ya nchi yetu imekuwa na viongozi wa namna hiyo ambao walifanikiwa sana pamoja na kuwa na mapungufu kama binadamu wengine.
Angalia orodha yenyewe, katika mawaziri waliofanikiwa kikazi ni wale waliokuwa wakali hata kama Rais alikuwa mpole na wengine walifanikiwa kwa vile Rais alikuwa mkali even though, mawaziri wakuu walikuwa wapole.

Mizengo Pinda hafai kabisa katika macho yangu pamoja na muda mrefu wa utumishi wake amekuwa ndani ya ofisi za waziri mkuu na Rais.
Rashidi Kawawa
Edward Moringe Sokoine
Cleopa David Msuya
Edward Moringe Sokoine
Salim Ahmed Salim
Joseph Sinde Warioba
John Malecela
Cleopa David Msuya
Frederick Sumaye
Edward Ngoyai Lowassa
Mizengo Pinda
 
Angefafanua zaidi tumuelewe yuko wapi na anamlenga nani? Upinzani au huko gambani kwake? Ila serikali inaongozwa na magamba kwahiyo nchi imefika hapa kwa ajili yake yeye na wenzake huko CCM

CCM kwa sasa wamechanganyikiwa kweli, Hakuna hata Mmoja anaye Gusia Maisha Bora kwa Kila Mtanzania, Ahadi za JK 2010 ZILIFIKIA TRILIONI 300 SAWA na Bajeti ya USA, ila hakuna hata mmoja anaye zungumzia hilo,

Jamaa wanatumia Propaganda zilizo kuwa zinatumiwa na Vyama vya Kikomonist huko Ulaya Mashariki kabla na Baada ya Kusambaratila kwa USSR
 
kiasi fulani awe kama gadafi. asiwe kama mobutu.

kweli kama tungekuwa na Rais dekteta hakika mimi ningeanza na waliomtumia sms za matusi SPIKA na wale waote walidiriki kumkashfu rais kuwa ni dhaifu na maneno mengine ya kipuuzi kama hayo wote wangeozea segerea.
 
CCM kwa sasa wamechanganyikiwa kweli, Hakuna hata Mmoja anaye Gusia Maisha Bora kwa Kila Mtanzania, Ahadi za JK 2010 ZILIFIKIA TRILIONI 300 SAWA na Bajeti ya USA, ila hakuna hata mmoja anaye zungumzia hilo,

Jamaa wanatumia Propaganda zilizo kuwa zinatumiwa na Vyama vya Kikomonist huko Ulaya Mashariki kabla na Baada ya Kusambaratila kwa USSR

Ina maana shughuli za maendeleo zinazoendelea hamzioni? endeleeni na kufumba macho yenu, CCM yenyewe inachanja mbuga.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom