Abdulhalim
Platinum Member
- Jul 20, 2007
- 17,193
- 3,011
Wakuu heshima mbele,
Nina swali linalonitatiza. Nawasihi mniwie radhi kama litaonekana la kijinga kwa baadhi yenu. Nataka kuitumia fursa ambayo jamvi linatupatia kujielimisha, if possible.
Kuna hili suala la kuvutia wawekezaji. Nchi zote ulimwenguni, masikini kwa tajiri zinazungumzia kuhusu hili suala.
Kwa mujibu wa uelewa wangu mwekezaji ni mtafuta faida. Ni kweli anapokuja kuwekeza huleta kiasi cha mtaji (fedha, mitambo, ujuzi n.k) lakini kama atafanikiwa, ina maana baada ya muda huchuma faida kutoka sehemu aliyowekeza. Kwa maana rahisi ni kuwa atakuwa amechuma kutoka sehemu au nchi aliyowekeza, yaani atakuwa na mtaji alokuja nao jumlisha na faida amabyo hakuwa nayo hapo awali.
Kwa upande wa nchi inayomwalika mwekezaji, baada ya muda huo huo, kiwango cha utajiri(overall wealth) kitakuwa kimepungua kwa kiwango sawa na faida alopata mwekezaji.
Sasa hapa, inakuwaje watu wanang'ang'ania kuvutia wawekezaji na mitaji kutoka nchi za nje? Nini faida zake?