Dhana ya kujivua gamba na kuvaa gwanda.

Nakapanya

JF-Expert Member
May 22, 2012
2,096
708
Nyoka anapojivua gamba;hufanya hivyo ili kuondoa gamba lile lililochoka ambalo haliwezi tena kutenda kazi ya kumlinda,kujongea na hata kumwezesha katika harakati za kuendeleza maisha yake kwa ujumla,hivyo hujivua gamba la zamani lilichoka ili kupata jipya ili kutimiza hayo hapo juu.CCM walipokuja na dhana ya kujivua gamba walikuwa na dhamira ileile kama ya nyoka yaani kuvua magamba(viongozi na wanachama)ambao wamechoka na hawana uwezo tena wa kukisaidia chama kutimiza malengo yake ya kila siku ya kuwaletea wananchi maendeleo.CHADEMA wamekuja na kampeni yao ya kuvaa gwanda(nijuavyo mimi ni askari tu ndio huvaa magwanda),nadhani wanavaa gwanda ili kuingia katika vita na mapambano ya kushika dola mwaka 2015,lakini katika vita hiyo wanataka kutumia sungusungu kupamban,hakikia mtashindwa;kwanini nasema hivyo;CCM wamevua magamba na kuyatupa kwa kuona hayafai tena,ila sasa hao CHADEMA wana pita nyuma na kuyaokota yale MAGAMBA NA KUYAVIKA MAGWANDA ili yakapigane,hakika mtashindwa milele na CCM itaendelea kutawala milele.Ni hayo tu na ni mtazamo wangu wa ki-shallow.
 
Ama kweli ni mtizamo wako wa ki-shallow. Kwani CCM imeisha mvua nani hillo gamba? CDM itawapa tabu sana, hamwazi mbinu mpya isipokuwa kupiga ramli eti lazima watashindwa. Endeleeni kuota.
 
kama vile nyie mnavyoota kushika dola;forget about that.
 
Ni kweli ndugu yangu vua gamba vaa gwanda inanipa wasiwasi shibuda alivua gamba kwa sasa amekuwa zaidi ya gamba. Makamanda kama lema, nassari, mnyika, mdee, mbowe, hawakuvua gamba na niwapambanaji wazuri kwanini tuwang'ang'anie tuandae vijana wetu wenyewe kama silinde, heche, na wengineo na si kubeba vinyonga toka ccm.
 
Naona unajionyesha mvivu wa kufikiri,hawachukui magamba bali wanavua magamba na kuvaa gwanda.kwa mantiki hiyo ccm wote ni magamba yanayotakiwa kuvuliwa na kuvikwa magwanda.
 
Hivi unavyosema CCm watatawala milele una maana gani? Ivi unajua sisi wananchi tumeshachoka sana? Hatuna hata matumaini kwa miaka 2 ijayo, tunalala njaa hatuna milo hata miwili kwa siku, huu utawala wa kimabavu, family na kujuana utaisha lini?
 
Utaisha pale tu utakapoamka kutoka usingizi mzito wa kuwaamini wanasiasa. Na kudhani jina chadema, ama Cuf, ama ccm, na upuuzi mwingine kama huo, unaweza kuleta mabadiliko chanya kwa jamii, na kutocheza nafasi yako katka mabadiliko, ni KUJIDANGANYA.
Mzungu amesema wajibu wetu katika mabadiliko upo kwenye kisanduku cha kura tu, then kura zetu zitufanikishie, kila baada ya miaka mitano, tujaribu tena, labda hawa au hawa, upuuzi mtupu! Gwanda, the same to Gamba, is equal to slavery, poverty, ignorance, selfishness, classes and colonialism. Pity!
Mungu wetu anaita!
 
Nyoka anapojivua gamba;hufanya hivyo ili kuondoa gamba lile lililochoka ambalo haliwezi tena kutenda kazi ya kumlinda,kujongea na hata kumwezesha katika harakati za kuendeleza maisha yake kwa ujumla,hivyo hujivua gamba la zamani lilichoka ili kupata jipya ili kutimiza hayo hapo juu.CCM walipokuja na dhana ya kujivua gamba walikuwa na dhamira ileile kama ya nyoka yaani kuvua magamba(viongozi na wanachama)ambao wamechoka na hawana uwezo tena wa kukisaidia chama kutimiza malengo yake ya kila siku ya kuwaletea wananchi maendeleo.CHADEMA wamekuja na kampeni yao ya kuvaa gwanda(nijuavyo mimi ni askari tu ndio huvaa magwanda),nadhani wanavaa gwanda ili kuingia katika vita na mapambano ya kushika dola mwaka 2015,lakini katika vita hiyo wanataka kutumia sungusungu kupamban,hakikia mtashindwa;kwanini nasema hivyo;CCM wamevua magamba na kuyatupa kwa kuona hayafai tena,ila sasa hao CHADEMA wana pita nyuma na kuyaokota yale MAGAMBA NA KUYAVIKA MAGWANDA ili yakapigane,hakika mtashindwa milele na CCM itaendelea kutawala milele.Ni hayo tu na ni mtazamo wangu wa ki-shallow.

kweli uko shallow
 
Hivi unavyosema CCm watatawala milele una maana gani? Ivi unajua sisi wananchi tumeshachoka sana? Hatuna hata matumaini kwa miaka 2 ijayo, tunalala njaa hatuna milo hata miwili kwa siku, huu utawala wa kimabavu, family na kujuana utaisha lini?

sema wewe umechoka usimsemee mwingine,kwahyo kushindia mlo mmoja kutaondolewa na chadema ikiingia madarakani?hahahaaaaaaaaa.......niche mimi.....
 
Back
Top Bottom