Dhana ya kubemenda mtoto: Mitazamo, Ufafanuzi na Ushauri

Sikubaliani na mtoa mada kubemendwa ni jambo lipo na la muda mrefu na nimeshuhudia hata marafiki zangu likiwakuta na watu wenye uwezo hata kiuchumi na hata wasomi limewakuta jambo hili. Tunapenda kudharau vitu vya msingi na vya kale wakati vilisaidia sana. Sasa kuna haja gani ya kufanya mapenzi siku 40 baada ya kujifungua? Hamu gani hii maziwa yanamtoka bado mtoto analialia! Tuweni wastaarabu na huyo mtoa mada kakiri wazi ndani ya siku 40 mama anaweza kupata mimba hivyo kuathiri ukuaji wa mtoto husika na wanandoa wengi wanafanya mapenzi usiku wataoga saa ngapi wakati mtoto kaanza kulia anataka nyonyo na mama na baba wamejaa mijasho ya kumaliza ngono zembe?
 
Kubemenda ipo tena sikwakusimuliwa ni kwangu. Mtt 2 nilijifungua 2010 na 3 2011. Mwanangu alikuwa anapata lishe bora ila nilipopata ujauzito tu mtoto ndo ishara yakwanza kunigutusha alianza kunyong'onyea na pindi ninapomnyonyesha kuhara choo chenye maziwa na kinanuka utaja kimbia. Nashukuru Mungu nilipata dawa za mila potofu isiyokuwa yakupigiwa lamli nilielekezwa nikaichimba nakuitumia, maelekezo mengine nisiwe karibu nae kwakumbeba nakumkumbatia mana joto langu si zuri nashukuru Mungu wote wazima na alitembea alipofunga mwaka ndipo nikamwachisha. Tusiwe wajinga kutukuza mila za wazungu na zetu zote kuita potofu. Napenda mila zetu zisizoleta uchonganishi
 
Yani hili suala la kubemenda linanatatiza kwa kweli, na nimekuwa mbishi kuamini....ila nimeshuhidia watoto wa watatu wanaosemekana wamebemendwa..kuhusu lishe ni kwamba wazazi wao wana pesa..tena huyo mmoja nilikuwa karibu naye....huyo alipewa kila aina ya lishe..lakini wapi mtoto ndo kwanza alikuwa ananyong'onyea akawa kama mdoli...kuja kustuka mamiye ana mimba nyingine.....Mpaka leo mtoto hana nyama..

Me naamini kubemenda inatokana na mama kubeba mimba nyingine wakati bado ananyonyesha na usafi tuu...!
 
1. Ni kweli ukitoka nje ya ndoa mwanao hatatembea?
2. Kuna mifano au mtoto/watoto ambao hawakutembea kwa sababu hiyo?
3. Nini hufanyika/tiba ikitokea hali hiyo?
4. Kwa kawaida huanza kutembea baada ya miezi/miaka mingapi?

Mwenzenu nimepokea kibarua kutoka kwa wakwe ati kama nimetoka nje basi nimjulishe mke wangu vinginevyo..!!, na mm nilikuwa mkoa mwingine kikazi na niligonga sana yale matundu.
 
Dhana ya kubemenda ipo sana!! Na ina kaukweli fulani coz niliwahi kumuona mtoto mmoja ni mkubwa but alikuwa hatembei amechukuliwa na bibi yake baada ya mama yake kumbemenda (alikuwa single parent na changudoa)

Mi tiba sijui ila najua kukinga!! Baada ya kuchepuka unatakiwa ujisafishe kwa kuoga!! Ile najisi baada ya kuzini ndiyo inasadikika kwamba humdhuru mtoto!! So, ukizini nje ya ndoa au mtu ambaye si mzazi mwenzio na ukatoka na kwenda kumshika mtoto ndipo anaathirika kwa kubemendeka.

Nilielekezwa kuwa ili kumjua mtoto aliyebemendwa (huitwa fundi viatu coz huwa hatambai wala kutembea) huchelewa sana kutembea, ngozi yake huvutika kama ya mzee na hupungua uzito hata kama anakula lishe kutoka wapi!!
 
Kitaalamu hili jambo c kweli lipo kiswahili zaidi. Mtoto anodhoofika kwa sababu ya lidhe mbovu tu. Mtafute dr yeyote atakusaidia hili. Ila kaa umeoa ndugu jihadhari na michepuko tulia na mkeo. Kujisifu uhuni sio ujanja.
 
Kuna hili suala linaloitwa 'kubemenda'
mtoto, watu wanadai kuwa sperms huwa
zinaleta madhara kwenye maziwa ya
mama na kumdhoofisha mtoto kiafya na
wengine wanasema ukimshika mtoto
baada ya sex pia ina madhara.
<!--[if !supportLineBreakNewLine]-->

kiukweli suala la Kubemenda ni
imani potofu (myth) na hakuna uhusiano
wa sperms na maziwa ya mama katika
kudhoofisha afya ya mtoto; iwe kwa
kushirikiana tendo la ndoa au kumshika
mtoto baada ya sex.


Je, nini maana ya kubemenda mtoto?
Kwanza hii imani potofu inaeleza kwamba
kubemenda mtoto ni pale wanandoa
wanapojihusisha na tendo la ndoa baada
ya mtoto Kuzaliwa (pale mke anapokuwa
tayari kiafya kwa tendo la ndoa baada ya
kujifungua) kwa maana kwamba sperms
huharibu maziwa ambayo mtoto
ananyonya, si kweli hakuna uhusiano
wowote kati ya maziwa ya mama na
sperms katika kuathiri afya ya mtoto.


Pili kubemenda mtoto ni kitendo cha
wanandoa kujihusisha na tendo la ndoa na
mke kushika mimba miezi mwili tu au
mitatu tu baada ya kujifungua na kupelekea
kuzaa mtoto mwingine baada ya mwaka na
matokeo yake mtoto aliyetangulia Kuzaliwa
huwa dhaifu kiafya (huchelewa kutembea)
na huitwa ni mtoto ambaye
amebemendwa, kitu ambacho ni imani
potofu kwani kuna wanandoa wengi tu
wamezaa watoto waliopishana mwaka na
wote wana afya njema kabisa.


Tatu kubemenda ni kitendo cha
mwanandoa mmoja kutoka nje ya ndoa
(sex) na akirudi ndani huendelea na tendo
la ndoa na matokeo yake mtoto wa ndani
ya ndoa huwa dhaifu, pia ni imani potofu
hakuna kitu kama hicho.


Jambo la msingi ni kufuata ushauri wa
kitaalamu ambao ni wiki sita baada ya
kujifungua.


Je, kuna ukweli wowote kuhusiana na hii
imani potofu
Iwe wanandoa kujihusisha na tendo la
ndoa baada ya mtoto Kuzaliwa au kuzaa
mwingine baada ya mwaka au hata kutoka
nje hakuna uhusiano na mtoto aliyezaliwa
kama suala la usafi na lishe bora
litazingatiwa kwa mtoto anayehusika.


Je, kulikoni mababu zetu wakaweka
imani kama hiyo kwa wanandoa?
Kama zilivyo imani zingine potofu kama vile
mwanamke mjamzito kutokula mayai
mababu zetu walikuwa na somo ndani
yake, inawezekana walitaka kuhakikisha
wanandoa wanashiriki vizuri katika kulea
mtoto kwa pamoja bila kupendekeza tabia
za uchafu na kujirusha nje na ndani ya
ndoa bila utaratibu.


Pia labda mababu zetu walihofia kitendo
cha mwanamke kutoa maziwa (chuluzika)
wakati wa tendo la ndoa hasa anapofika
kileleni (tangu akifungue hadi miezi 8 hivi)
na wakawa wanahofia kinaweza kuathiri
kiwango cha chakula cha mtoto hivyo ili
kuzuia ni kutunga imani (potofu) kwamba
mtoto ataathirika kwa mke na mume
kushiriki tendo la ndoa.


Je, ili mtoto asionekane amebemendwa
wanandoa wanahitaji kufanya kitu gani?
Ni vizuri kufahamu kwamba hakuna
uhusiano wa sperms kuharibu maziwa ya
mama wakati wa kumnyonyesha mtoto
hivyo wanandoa kushiriki tendo la ndoa
halina uhusiano wowote na mtoto kuwa na
afya mbaya kiasi cha kuchelewa kutembea.
Mtoto anahitaji watoto chakula bora chenye
viini-lishe vyote vinavyohitajika ili kukua
vizuri pia mama anahitaji kujiweka
mazingira safi (kuwa msafi) wakati
ananyonyesha, ahakikishe anasafisha
chuchu zake na mikono yake au kuzingatia
usafi kimwili kabla ya kumnyonyesha mtoto
iwe baada ya sex au muda wowote.


Ni jukumu la baba na mama wa mtoto
kuhakikisha wanatumia muda wao
kuhakikisha mtoto anapata lishe bora na
mahitaji yote ya msingi ya mtoto ili kukua
na kuwa na afya njema na si kujinyima
kujihusisha na tendo la ndoa wakihofia
mtoto kuonekana amebemendwa.


Pia suala la usafi wa mazingira ya mtoto
anapoishi (vyombo vya kutumia kwa
chakula cha mtoto, usafi wa mwili wa
mtoto na mama na baba pia) ni muhimu
sana kwani baada ya tendo la ndoa ni
muhimu kwa mume na mke kuhakikisha
wanakuwa safi tena bila kujihusisha na
kumnyonyesha mtoto huku hawajanawa au
kuoga.


MUHIMU
Suala la kubemenda (binafsi naweza kuita
ni utapiamlo au kwashakoo kingereza-
Kwashiorkor) huzungumzwa sana na jamii
za “mtanzania wa kawaida” huwezi kusikia
katika nchi zilizoendelea na watu ambao
wameenda shule na wanafuata misingi ya
afya na uzazi katika kulea watoto wao na
pia mke na mume kuwa karibu kimapenzi.


Huwezi kusikia takataka za neno
kubemenda katika nchi zilizoendelea
kama Canada, Sweden, Australia,
Ujerumani nk why?

Ni traditions (Myth).
 
Kuna hili suala linaloitwa 'kubemenda'
mtoto, watu wanadai kuwa sperms huwa
zinaleta madhara kwenye maziwa ya
mama na kumdhoofisha mtoto kiafya na
wengine wanasema ukimshika mtoto
baada ya sex pia ina madhara.
<!--[if !supportLineBreakNewLine]-->

kiukweli suala la Kubemenda ni
imani potofu (myth) na hakuna uhusiano
wa sperms na maziwa ya mama katika
kudhoofisha afya ya mtoto; iwe kwa
kushirikiana tendo la ndoa au kumshika
mtoto baada ya sex.


Je, nini maana ya kubemenda mtoto?
Kwanza hii imani potofu inaeleza kwamba
kubemenda mtoto ni pale wanandoa
wanapojihusisha na tendo la ndoa baada
ya mtoto Kuzaliwa (pale mke anapokuwa
tayari kiafya kwa tendo la ndoa baada ya
kujifungua) kwa maana kwamba sperms
huharibu maziwa ambayo mtoto
ananyonya, si kweli hakuna uhusiano
wowote kati ya maziwa ya mama na
sperms katika kuathiri afya ya mtoto.


Pili kubemenda mtoto ni kitendo cha
wanandoa kujihusisha na tendo la ndoa na
mke kushika mimba miezi mwili tu au
mitatu tu baada ya kujifungua na kupelekea
kuzaa mtoto mwingine baada ya mwaka na
matokeo yake mtoto aliyetangulia Kuzaliwa
huwa dhaifu kiafya (huchelewa kutembea)
na huitwa ni mtoto ambaye
amebemendwa, kitu ambacho ni imani
potofu kwani kuna wanandoa wengi tu
wamezaa watoto waliopishana mwaka na
wote wana afya njema kabisa.


Tatu kubemenda ni kitendo cha
mwanandoa mmoja kutoka nje ya ndoa
(sex) na akirudi ndani huendelea na tendo
la ndoa na matokeo yake mtoto wa ndani
ya ndoa huwa dhaifu, pia ni imani potofu
hakuna kitu kama hicho.


Jambo la msingi ni kufuata ushauri wa
kitaalamu ambao ni wiki sita baada ya
kujifungua.


Je, kuna ukweli wowote kuhusiana na hii
imani potofu
Iwe wanandoa kujihusisha na tendo la
ndoa baada ya mtoto Kuzaliwa au kuzaa
mwingine baada ya mwaka au hata kutoka
nje hakuna uhusiano na mtoto aliyezaliwa
kama suala la usafi na lishe bora
litazingatiwa kwa mtoto anayehusika.


Je, kulikoni mababu zetu wakaweka
imani kama hiyo kwa wanandoa?
Kama zilivyo imani zingine potofu kama vile
mwanamke mjamzito kutokula mayai
mababu zetu walikuwa na somo ndani
yake, inawezekana walitaka kuhakikisha
wanandoa wanashiriki vizuri katika kulea
mtoto kwa pamoja bila kupendekeza tabia
za uchafu na kujirusha nje na ndani ya
ndoa bila utaratibu.


Pia labda mababu zetu walihofia kitendo
cha mwanamke kutoa maziwa (chuluzika)
wakati wa tendo la ndoa hasa anapofika
kileleni (tangu akifungue hadi miezi 8 hivi)
na wakawa wanahofia kinaweza kuathiri
kiwango cha chakula cha mtoto hivyo ili
kuzuia ni kutunga imani (potofu) kwamba
mtoto ataathirika kwa mke na mume
kushiriki tendo la ndoa.


Je, ili mtoto asionekane amebemendwa
wanandoa wanahitaji kufanya kitu gani?
Ni vizuri kufahamu kwamba hakuna
uhusiano wa sperms kuharibu maziwa ya
mama wakati wa kumnyonyesha mtoto
hivyo wanandoa kushiriki tendo la ndoa
halina uhusiano wowote na mtoto kuwa na
afya mbaya kiasi cha kuchelewa kutembea.
Mtoto anahitaji watoto chakula bora chenye
viini-lishe vyote vinavyohitajika ili kukua
vizuri pia mama anahitaji kujiweka
mazingira safi (kuwa msafi) wakati
ananyonyesha, ahakikishe anasafisha
chuchu zake na mikono yake au kuzingatia
usafi kimwili kabla ya kumnyonyesha mtoto
iwe baada ya sex au muda wowote.


Ni jukumu la baba na mama wa mtoto
kuhakikisha wanatumia muda wao
kuhakikisha mtoto anapata lishe bora na
mahitaji yote ya msingi ya mtoto ili kukua
na kuwa na afya njema na si kujinyima
kujihusisha na tendo la ndoa wakihofia
mtoto kuonekana amebemendwa.


Pia suala la usafi wa mazingira ya mtoto
anapoishi (vyombo vya kutumia kwa
chakula cha mtoto, usafi wa mwili wa
mtoto na mama na baba pia) ni muhimu
sana kwani baada ya tendo la ndoa ni
muhimu kwa mume na mke kuhakikisha
wanakuwa safi tena bila kujihusisha na
kumnyonyesha mtoto huku hawajanawa au
kuoga.


MUHIMU
Suala la kubemenda (binafsi naweza kuita
ni utapiamlo au kwashakoo kingereza-
Kwashiorkor) huzungumzwa sana na jamii
za “mtanzania wa kawaida” huwezi kusikia
katika nchi zilizoendelea na watu ambao
wameenda shule na wanafuata misingi ya
afya na uzazi katika kulea watoto wao na
pia mke na mume kuwa karibu kimapenzi.


Huwezi kusikia takataka za neno
kubemenda katika nchi zilizoendelea
kama Canada, Sweden, Australia,
Ujerumani nk why?

Ni traditions (Myth).
Mkuu wewe umejibu...asante kwa kuchukua muda wako! Umeniondolea hofu.
 
mkuu hili swala linawapa shida wengi,wengine mke na mume hushaurina wazungu wawamwagie nje kumuepusha mtoto na kubemendwa.
 
me siiamini dhana hii...nimegonga nje mara kibao lakini mwanangu ana afya yake tena bonge kuliko kawaida
 
Toka zamani nikiwa mdogo nikawa nasikia wakina mama wakisema mara mtoto huyu kabendwa na wazazi wake.... Lakini maana halisi nikawa sielewi vizuri ... Naomba mnijuze wadau....
 
Nini maana halisi ya hiyo terminology kubemenda mtoto kati ya hizi.
# mwanamke kunyonyesha mtoto wakati ana mimba

## mwanamke kushiriki tendo la ndoa na mwanaume nje ya ndoa wakati ana nyonyesha.

Je kuna FACTS za kitaalamu kuhusu hizi dhana mbili?

Dalili za mtoto aliyebemendwa ni zikoje?
 
Kubememenda mtoto ni hali ya kuzorota kwa afya ya mtoto..mara nyingi hutokea pale mama anaposhindwa kumuhudumia mtoto wake hasa kumnyonyesha na kumtunza katika hali ya usafi..
Hii utokea hasa pale mama anapokuwa busy ba mambo mengine hasa mchepuko wa nje..mda wa kulea mtoto ye yupo anagegendwa hapo ndo afya ya mtoto inapoanza kudhoofu na inajulikana mtoto anahitaj care muda wte...
Ila sasa wabongo tumeunganishwa na kuwa mama kugegedwa nje kunaleta kubemenda..ila hakuna uthibitisho wa kitaalam juu ya hili
 
Ukishindwa kumhudumia mtoto vizut afya yake inadhoofy tu hapo tutasema umembemenda lakini sababu sio kugegendwa.
Dalili huwa ni kwamba afya dhoofu,uzito kupungua,kushambuliwa kirahisi na magonjwa na mtoto kudumaa kushindwa kukua kutokana na rate ya miaka yake
 
Nilikuwa mkoani Njombe kwa siku mbili zilizopita(sio nyumbani) ,juzi ktk pitapita nilikaa sana kwenye kijiwe Kimoja cha draft na wazee pamoja na Vijana huko.Jirani na kijiwe hicho kuna duka ambalo muhudumu wake ni binti mwenye mtoto ambae kama ndo anaanza kutembea hivi,kwa mbali mtoto huyo alikuwa anaonekana kupata tabu pindi alipojaribu kutembea, maana kila baada ya hatua Kama mbili alikuwa akianguka na kutabalia tumbo au kukaa chini kabla hajajaribu tena kuinuka mtoto huyo wa kiume akijaribu mara kwa mara huku ilionekana ni zoezi gumu kwake.

Kijana mmoja alisikika akisema huyu binti " kambemenda mwanae" ndo maana amechelewa kutembea na ata anapojaribu kutembea miguu inaonekana inakosa nguvu,hoja hiyo iliungwa mkono na baadhi ya vijana na ata wazee.

Ndipo nilipopata tashwishwi ya kujua nini maana " kubemenda mtoto" kutoka kwa wenyeji wangu. Walinijibu kuwa ni mwanamke mzazi kutembea na mwanaume / wanaume wakati angali ananyonyesha .Hivyo kitendo hicho kina mdumaza mtoto wake katika ukuaji wake.

Wanajopo naomba mnisaidie kunijibu maswali yafuatayo ,je kuna uhusiano gani kati ya ukuaji wa mtoto na mama yake kufanya tendo la ndoa wakati mtoto angali ananyonya?

Je " kuna neno la Kiswahili linaloelezea maana halisi ya " kubemenda " kama linavyo julikana huko Njombe? Na je hili ni jambo la kisayansi au ni moja ya mambo yaliyokuwa yakisemwa zamani yasiyokuwa na mantiki kama mwanamke mjamzito asile mayai?
 
Back
Top Bottom