Dhana ya kubemenda mtoto: Mitazamo, Ufafanuzi na Ushauri

Hakuna cha imani km baba au mama akijihusisha na mapenzi nje mtoto lazma yatamkuta ya kumkuta watoto wengine hushindwa hata kutembea kwa muda muafaka hata km haumwi wengine hata kuongea ni mambo ambayo practically yapo na tunayaona halafu mtu anasema eti ni imani!
 
It make sense!!!!!!!
Kuna mtoto wa dada mmoja alikuwa na matatizo haya,ikadaiwa kuwa mama wa mtoto ana fanya haya lakini mama wa mtoto akawa anabisha ilifikia yule mtoto akadhoofu hadi kufikia kwamba akiwa ananyonya maziwa ya mama anatapika

Akashauriwa aende hospital alipouluzwa kuhusu jambo hilo mama wa mtoto alikana tena daktari akamwambia mtoto akitapika apeleke matapishi,mama wa mtoto alipopeleka da daktari kuyapima alikuta kwenye matapishi kuna mbegu za kiume za watu wawtatu tofauti

Hili lilinishangaza sana na hadi leo nashangaa hasa ukizingatia namna tunavyoambiwa namna mbegu za kiume zinavyokuwa baada ya kuingia ukeni,nadhani wenye taaluma hii wanaweza kulielezea vyema sana hili

Ilibidi yule dada akubaliane na ukweli alipewa dawa na alisitisha mahusiano na wanaume aliokuwa nao na mtoto alirudi kwenye hali yake ya afya njema

Not exactly
Huwa kuna dawa wanatumia na watoto hawadhuriki!

Btw
Habari ya siku?

Salama tu swahiba. . .za kwako?

Hmmmmm. . .mbegu kwenye matapishi? Again, it doesn't make sense. Bado inabaki kuwa kwenye imani kwasababu kitu kama hicho hakielezeki.

Kuna dada yeye alimini ukuaji wa mtoto wake wa 1yr hauendi mbele kwasababu anaweza akawa mjamzito. Turned out she was pregnant, ila bado siamini kwamba ndio chanzo cha mwanae kutotembea haraka. Pengine ni mmoja wa wale wanaochelewa kutembea kama ambavyo wapo wanaowahi sana.
 
There's no such thing "kubemenda"...ni imani isiyo na mashiko yoyote kibaiolojia...

Nadhani hii ni nadharia iliyowekwa ili kutoa fursa kwa wamama kupata muda wa kukuza wanao pengine na kurejesha maungo ya uzazi katika hali ya kawaida...
 
Salama tu swahiba. . .za kwako?

Njema sana,nafurahi kukuona!

Hmmmmm. . .mbegu kwenye matapishi? Again, it doesn't make sense. Bado inabaki kuwa kwenye imani kwasababu kitu kama hicho hakielezeki.

Hata kwangu haikuleta maana lakini sikubisha wala kukataa kwakuwa sina taalima hiyo
Ila kitendo cha yule binti kukubali kuwa alikuwa anafanya hivyo na kitendo cha yeye kuacha na afya ya mtoto kubadilika kinastua pia!

Kuna dada yeye alimini ukuaji wa mtoto wake wa 1yr hauendi mbele kwasababu anaweza akawa mjamzito. Turned out she was pregnant, ila bado siamini kwamba ndio chanzo cha mwanae kutotembea haraka. Pengine ni mmoja wa wale wanaochelewa kutembea kama ambavyo wapo wanaowahi sana.

Sawa!

Vipi kuhusu watu na matabibu kudai kuwa sigara inasababisha kansa wakati kuna watu wamevuta tangu wana miaka 15 na wamezeeka hawajawahi kupata tatizo lolote na waliwahi kupimwa na hawakua na kansa?

kuna mambo hayaleti maana lakini kutokuleta maana kwetu haimaanishi hayapo!!
 
It make sense!!!!!!!
Kuna mtoto wa dada mmoja alikuwa na matatizo haya,ikadaiwa kuwa mama wa mtoto ana fanya haya lakini mama wa mtoto akawa anabisha ilifikia yule mtoto akadhoofu hadi kufikia kwamba akiwa ananyonya maziwa ya mama anatapika

Akashauriwa aende hospital alipouluzwa kuhusu jambo hilo mama wa mtoto alikana tena daktari akamwambia mtoto akitapika apeleke matapishi,mama wa mtoto alipopeleka da daktari kuyapima alikuta kwenye matapishi kuna mbegu za kiume za watu wawtatu tofauti

Hili lilinishangaza sana na hadi leo nashangaa hasa ukizingatia namna tunavyoambiwa namna mbegu za kiume zinavyokuwa baada ya kuingia ukeni,nadhani wenye taaluma hii wanaweza kulielezea vyema sana hili

Ilibidi yule dada akubaliane na ukweli alipewa dawa na alisitisha mahusiano na wanaume aliokuwa nao na mtoto alirudi kwenye hali yake ya afya njema

Not exactly
Huwa kuna dawa wanatumia na watoto hawadhuriki!

Btw
Habari ya siku?

Daaa hii inashangaza mkuu
 
yeah lisemwalo lipo tanga nakua nayasikia haya sii leo yameanza na mara nyingi it works out!
swala la mmoja wa wazaz wa watoto akitoka nje ya ndoa wakat mama ananyonyesha
mama kunyonyesha wakat akiwa na mimba
au mama kubeba mimba wakat akiwa na mtoto ambae hat hajatembea anambemenda na atachelewa kutembea na kuongea pia.
mtu akitoka kufanya mapenz akimbeba mtoto mchanga anambemenda mfano mgeni akija kwako ili ambebe mtoto lazima anawe mikono kwanza.so mambo haya yapo na yanafanya kazi.AAMINIYE NA AFAHAM
 
Wana jamvi wenzangu kuna swala huwa linanitatiza sana napo ni kuhusu kubemendwa kwa mtoto je ni pale mmoja wa mzazi anapotoka kufanya ngono na kumshika mtoto bila kutoa janaba i mean bila kuoga au ni pale unapotoka kufanya ngono na kuoga then ukifika kwako na kumshika mtoto au ni vyote viwili vinahusika???naomba kujuzwa wanajamvi
 
Hamna kitu kama hicho na wala hakuna mahusiano yoyote ni kujihisi tu ukutoka kufanya hayo fata ratiba yako kama kawaida oga beba mtoto na hata kabla ya hayo waweza beba mtoto bila shaka yyt mtoto ukiwa unamtunza vzr na lishe njema pamoja na mama yake hiyo haipo na wala hakuna mahusiano toa hoja zenu mie nimemaliza
 
mhh hichi kitu nikitata kidogo ila kwa mimi ninavyoelewa ni kitendo cha mama kugegedwa na mwanaume mwengine alafu akaja akamnyonyesha mtoto ambaye ni mdogo xana kama mwaka 0_2.au baba kupiga mechi nje alafu akaja na kwamama akacheza mechi bila kuoga au kunawa xaxa mama akimnyonyesha mtoto tu kutokana na mabadiliko ya joto la mama ndo linaathili ukuaji.cjui kwa wengine wanafahamuje....
 
kwa ufahamu wangu, kubemenda mtoto hutokea pale mama anapobeba ujauzito mwingine af akaendelea kumnyonyesha mtoto inasemekana maziwa huchafuka so mtoto huwa rojorojo kama mlenda
 
kwani wazazi wetu wameishije?inamaana walikuwa hawagegedani mtoto akiwa mdogo? chamsingi ni kuwa na kiasi ngono isiwe kama chai ya kila asubuhi kiukweli kama wazazi wataendekeza ngono kila cku ni rahisi sana mtoto kuharibika mm ninayomifano halisi ya jirani zangu ambao watoto wao wameharibika kwa hilo,mtoto anapokuwa na umri 0 hadi mwaka mmoja mama apewe ngono mara moja angalau kwa ajili ya afya mana ngono kwa wenye ndoa huleta afya ila ngono ikizidi zaidi ya mara 2 kwa wiki ni rahisi kubemenda mtoto coz shahawa ni protin in nature na zina asidi kali sana zikizidi zinaenda kuharibu protini inayopatikana ktk ziwa la mama. upo hapoooooooo?
 
ni kumkwamisha mtoto katika ukuaji wake.ni kumfanya mtoto achelewe kutoka hatua moja ya ukuaji kwrnda nyingine.kwa mfano kutoka kutambaa hadi kutembea.

kadiri nijuavyo,mwili wa mtoto wa aina hii hulegea na kudhoofu kwa kukosa nguvu.inaaminika kuwa kubemenda hutokana na mama kufanya mapenzi bila kinga.baadaye mtoto hunyonya uchafu huo na kumdhuru.

baba mzazi halisi hasababishi kubemenda.mkuu Amavubi upo?
 
Last edited by a moderator:

hapo bold sio kweli manake hata ufanyeje maziwa ya mama hayawez kubeba uchafu wowote ule unless uwe ni ugonjwa ambao mama kama mama atakuwa nao ama uwe ni kemikali tena ambazo zina desturi ya kukaa kwenye maziwa.

haya tuendelee.......... Amavumbi hakuna uhusiano wowote kati ya mtoto kubemendwa na tendo la ndoa ingawa elkimu za mtaani zinaomnyesha wazi kwamba mtoto hubemendwa na hubemendwa ama na baba yake ama mama yake.

mara nyingi hizi ni imani ambazo wengine hasa wangindom huamini mtoto wa kiume hubemendwa na baba na mtoto wa kike hubemendwa na mama.

wahaya huamini mtoto yyte hubemendwa na mzazi yyte anayetoka nje ndoa mtoto akiwa mchanga, lkn baadhi ya makabila huamini kama wangoni wao husema mtoto hubemendwa na hata kutoka kwa wazazi wake. wapo wengine ambao hata binti wa kazi ama mlezi wa mtoto huamin kwamba huweza kumbemenda.

tuachane na hizo porojo, ukweli ni kwamba mtoto mdogo hupenda na hukua vyema iwapo mambo haya atapatiwa , lishe bora, upendo, alale vyema na awe msafi wa mwili na mahali pa kulala. iwapo mtoto atakosa haya yote basoi mtoto hudhoofiuka sana na kushindwa kukua vyema na hatimaye hurudi nyuma kimakauzi. si jambo geni kumkuta mtoto mdogo kalegea kwa kukosa madini kama calcium na phosphorus na hivyo kumkuta kaka lia mfupa wa mgongo kiasi kwamba mtoto huyu akijisaidia choo hutoka kuelekea mbelen badala ya kutoka kuelekea nyuma. pia si ajabu kumkuta mtoto huyu hawez kusmama manake hana nguvu miguuni na mtoto akakonda sana na kudhoofu.

sababu kubwa huwa ni hayo niliyoeleza hapo juu kwamba lishe ni tatizo, usafi na hata mapenzi kwa mtoto. wazazi wengi hujisahau kwenye lishe na usafi wakitegemea dada ama walez na hivyo mwisho wa siku mtoto ananyongea sana.......kiutaalam kuna dawa mtoto anazopewa kama suppliment ya madini ili aweze kuwa na nguvu lkn pia mzazi husahuriwa kuwa msafi na ampende mtoto. upweke huweza kumfanya mtoto akawa mnyomngefu sana.

baadhi ya wazazi hujisahau na kuacha hata kuwakumbatia watoto wao, kisa wakitafuta hela na kumlinda mume asitoke nje na hpo ndipo huaribu mambo kwani mtoto hukosa usimamizi wa karibu.

clinically hakunaga swala la kubemenda ila ni story za mtaani.

kwa wangoni wenzetu husema kabisa ili mtoto asibemendwe basi mama aeke kitambaa cha shughuli mapajan kisha amakande nacho mtoto, wangindo husema mama anawie maji baada ya tendo kisha amwogeshee mtoto, na wengine humvisha mtoto mvule kama wrist band, imani ziko nyingi kwakweli wazaramo wao humkandia mtoto na chupi kisha kumfukiza kwenye moto.....yaani tukisema hapa kila mtu ataje kabila lao wanafanyaje utashangaa sana...........

niongeze pia hakuna uhusiano wowote kati ya mimba na mtoto kunyonya, mama ikitokea kapata mimba wakati mtoto ananyonya basi ajitahd kula vyema vyakula vya kujenga, kukuza na kulinda mwili kisha aendelee kumnyonyesha mtoto wake walau mimba ifike miezi 6-7 ndipo amkomeshe kunyonya.

ikitokea hali ya mama ni mbaya kiafya basi anashauriwa asiendelee kunyonyesha mtoto ila alikizie chakula.
 
Last edited by a moderator:
idriss pia ikumbukwe kwamba mama anyechepuka baada ya kujifungua ni rahisi sana kuambukizwa magonjwa na hivyo kumuambukiza mtoto wakati mwingine. sababu kubwa ni immunity ya huyu mama huwa imeshuka. lkn hata hivyo ni nadra asana hili kutokea.

baba nae akipata ugonjwa nje anaweza kumuambukiza mtoto, but so kwamba wamembemenda

tena ni vyema wazazi wakaliwazana baada ya uzazi ili kuleta ule umoja na ushirika na asiwepo atakayeona kwamba ameachiwa mzigo wa kulea mtoto
 
Last edited by a moderator:
Wana jamvi naomba mnisaidie..kuna dhana kuwa mama aliyejifungua akifanya mapenzi na mwanaume tofauti na yule aliyezaa nae mtoto katika kipindi ambacho mtoto bado ananyonya kuna uwezekano mkubwa mtoto akawa dhaifu na akachelewa kutembea...Je kuna ukweli katika hili? Kuna jirani yangu mtoto wake ana mwaka na nusu bado anasuasua kutembea je inawezakana kabemendwa?
 
huko mkoani Mara ikiwa hali hiyo itatokea kwa mwanandoa hata mmoja kuchepuka nje mtoto ataugua sana na pengine kufa.

Ikiwa mwanaume ndye atachepuka nje haruhusiwi kumshika mtoto moja kwa moja pindi arejeapo home hadi mambo fulani yafanyike.
 
Hakuna kitu kama hicho jamani
Mm nime experience kwa mwanangu mwenyewe, nilikuwa naenda kugonga nje narudi namshika mwanangu lakina mpaka leo hii nazungumza ana miaka miwili afya njema anaongea kama wa miaka mitatu.
 
Back
Top Bottom