Dhana duni ya 'Mfumo Kristo'

Status
Not open for further replies.
Nimeusikia mfumo huo ila maana halisi sijaitambua, Mfumo wa Kisiasa wa Kikristo au Mfumo wa Uvuvi huko Mbegani? Kama ni wa kiserikali basi sijaelewa maana Viongozi wote Wakuu wa Nchi ni Muslims ni mfumo upi tena.... Ufafanuzi ni Rais, Makamu wa Rais, Rais ZNZ, Mawaziri, DC, RC nk. Mfumo unaouzungumia hapa ni upi. Mmejaribu kuwatenganisha Watanzania Kutoka katika Muungano mmechemsha, Mmejaribu kuwatenga kwa ukabila mmechemsha, sasa mnabeep kwa udini hamtawapata Watanzania. Hisiavzangu ninyi ni kundi la Mashoga chini ya mwamvuli wa dini ndo mnadai mfumo huu ni mfumo Kristo, wekeni bayana tuwasaidie kuliko kuichafua dininya Mwenyezi Mungu ISLAM kwa kusema uongo.
 
UDINI UDINI umewajaa vichwani mwenu,kila jambo mnaingiza udini tu hakika ipo siku litatugharimu Watanzania wenzangu mbona hatubadiliki?
 
kila kukicha, unajitokeza ushahidi kwamba kiwango cha kufikiri miongoni mwa wa-tanzania wengi ni duni. Siku hizi, kwa mfano, imeibuka hii dhana ya mfumo kristo.

Walioibuni dhana hii na ambao wanaieneza wana ajenda ya kujenga hoja kuwa mfumo wa utawala na uchumi tanzania unaendeshwa kwa misingi ya kikristu, na kwa lengo la kuwanufaisha wa-kristu na kuwakandamiza na kuwanyima wa-islam fursa na haki wanazostahili, katika nyanja mbali mbali, kama vile elimu na uongozi.

Hii ndio dhana ya msingi ya hiki kinachoitwa mfumo kristo. Wanaojenga hoja hii wanadai kuwa serikali ya tanzania yenyewe inaendeshwa na maaskofu kama sehemu ya uendelezaji wa huu wanaouita mfumo kristo.

Kwanza napenda kusema, kama ninavyosema daima, kuwa kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake. Uhuru huu ni pamoja na uhuru wa kuyahoji au kuyapinga mawazo ya wengine, kufuatana na mchakato wa kujielimisha na kutafakari masuala. Ni pamoja na uhuru wa kuyapinga mawazo yako mwenyewe.

nashangaa kwa nini mfumo mbovu uhusishwe na jina la yesu kristu. Dini zote mbili, u-islam na u-kristu, zinamtambua na kumheshimu yesu. Yesu anatambuliwa kama mungu katika u-kristu. Na katika u-islam, anatambuliwa kama mtume maarufu. Dini zote zinamheshimu sana yesu.

kama mfumo wa tanzania umeoza kama inavyosemwa, hauwezi kuwa mfumo kristo. Kuuita mfumo kristo ni dhihaka isiyo kifani. Huwezi kuuhusisha uchafu wowote na mungu au mtume. Kama kweli maaskofu wanaendekeza na kuulinda mfumo wa dhuluma, wanakiuka mafundisho na maadili ya kristo. Huu si mfumo kristo. Mfumo kristo ni mfumo wa haki na maadili aliyotufundisha kristo.

sidhani kama inahitaji akili ya pekee sana kuitambua hoja hii. Lakini ni wazi kuwa watu wengi tanzania wana kiwango duni cha kufikiri au kuelewa mambo. Kwa dhana yao ya mfumo kristo, wanaudhihaki u-kristo, na pia wanaudhihaki u-islam. Ila, kutokana na akili zao duni, hawatambui hilo. Kilichopo ni kuwaombea dua njema, waweze kujitambua na kujirekebisha.

Tatizo lipo....hawasemi kwa bahati mbaya...kuna mifano wanaitaja...sasa hizi ni tuhuma zina elekezwa kwa serikali...ni hili tangu zamani ..serikali inatuhumiwa...wakati wa mwalimu hali ya waislam ilikua mbaya zaid...sisi kama raia wa kawaida hatuwezi kujibu hoja hizi...ni serikali inatakiwa ije safi...ijikoshe mbele ya jamii...itamke kwamba serikali mawaziri, wabunge, makuu wa mikoa,wa wilaya, bodi za mashirika , wakurugenzi, jeshi, polisi, mahaka..

Inatakiwa mfano waziri mkuu akanushe madai haya aseme wazi kwamba serikali haibagui na mtendaji yoyote ambae anaweka dini yake mbele kwenye maamuzi basi atawajibishwa.
Sasa serikali inakaa kimya..tena kimyaa..cha mshindo..maana yake nini? Kisheria ukikaa kimya basi umekubali yanayosemwa...

Na upande wa kanisa ....linatuhimiwa....nalo kuwaashindiza waumini wao waliopo serikalini walipendeee kanisa na wawabane waislam..sasa hapa tuhuma zipo kwa kanisa ...nao..wawatoe mashaka ....waislam kwamba wao hawafany hayo...ila wanataka uadulifu katika mambo ya serikali.
Lakini nao wamekaa kimya...maana yake nini?

Sasa sisi tukikaa hapa tukijibu kwa niaba ya serikali ama kanisa shutuma zitakuwepo...tu...lakini hebu tujikumbushe kidogo historia...kanisa linaonekana kusema sana anapokuwa rais muislam...lakini akiwa mkrissto ..atauza, nbc, atauza madini yote,atanunua ndege mbovu,reli itabinafsishwa kinamna namna..lakini hata siku moja hawa wezi kulaumu..hata siku moha....kwao hakuna ufisadi...na hpa ndipo penye mashaka
lakini tofauti yao na masheikh ...wao akiwa mkristo akiwa muislam madam amekosea watamsema...
Tuwachieni kanisa na serikali wajibu hoja hizi..

Mutambue waislam hawana ugomvi na wakristo bali serikali kwa kukubali mashindikizo
 
Hapa naona mambo makubwa mawili;

  1. 1. Yawezekana rais ameamua kubalance wafanyakazi kwa kufanya teuzi nyingi kuwapa waislam ukilinganisha na viongozi waliopita hivyo wakristo na wengineo wanaona ajabu kwani hawakuzoea au,
  2. 2. Rais ni mdini kweli ameamua kuwapendelea waislam kwa kigezo hicho cha kubalance watumishi wa serikali.
My take: Raisi awe anafanya teuzi za hawa viongozi kwa kuzingatia utendaji/uwajibikazi mzuri wa wateule hawa na hii itasaidia kuondoa hii dhana ya udini serikalini.
 
Nauunga mkono 100% mawazo yako, udini usitufakarishe leo, udini kiweza kunitenganisha na rafiki zangu na ndugu zangu, basi hiyo sio dini tena ni fitna. Tuwe macho na hawa mafisadi wanao kwenda kweny misikiti na makanisa kufanya uchochezi. Hii ni mbinu moja wapo ya kufucha uchafu/uwizi na unafiki wao.

Watanzania wote ni ndugu tuungane
 
Si hela zetu za walipa kodi ndo munagawiwa nyinyi na huyo kikwete mukajenge hospitali na mashule halafu unasema kanisa linajenga au ushasahau mkuu ile munayochota kule ikulu
 
Udini is undoubtedly Kikwete's major legacy. But we're more than ready to give his seed a proper treat if and when needed.
 
Kila kukicha, unajitokeza ushahidi kwamba kiwango cha kufikiri miongoni mwa wa-Tanzania wengi ni duni. Siku hizi, kwa mfano, imeibuka hii dhana ya mfumo Kristo.

Walioibuni dhana hii na ambao wanaieneza wana ajenda ya kujenga hoja kuwa mfumo wa utawala na uchumi Tanzania unaendeshwa kwa misingi ya kiKristu, na kwa lengo la kuwanufaisha wa-Kristu na kuwakandamiza na kuwanyima wa-Islam fursa na haki wanazostahili, katika nyanja mbali mbali, kama vile elimu na uongozi.

Hii ndio dhana ya msingi ya hiki kinachoitwa mfumo Kristo. Wanaojenga hoja hii wanadai kuwa serikali ya Tanzania yenyewe inaendeshwa na maaskofu kama sehemu ya uendelezaji wa huu wanaouita mfumo Kristo.

Kwanza napenda kusema, kama ninavyosema daima, kuwa kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake. Uhuru huu ni pamoja na uhuru wa kuyahoji au kuyapinga mawazo ya wengine, kufuatana na mchakato wa kujielimisha na kutafakari masuala. Ni pamoja na uhuru wa kuyapinga mawazo yako mwenyewe.

Nashangaa kwa nini mfumo mbovu uhusishwe na jina la Yesu Kristu. Dini zote mbili, u-Islam na u-Kristu, zinamtambua na kumheshimu Yesu. Yesu anatambuliwa kama Mungu katika u-Kristu. Na katika u-Islam, anatambuliwa kama mtume maarufu. Dini zote zinamheshimu sana Yesu.

Kama mfumo wa Tanzania umeoza kama inavyosemwa, hauwezi kuwa mfumo Kristo. Kuuita mfumo Kristo ni dhihaka isiyo kifani. Huwezi kuuhusisha uchafu wowote na Mungu au mtume. Kama kweli maaskofu wanaendekeza na kuulinda mfumo wa dhuluma, wanakiuka mafundisho na maadili ya Kristo. Huu si mfumo Kristo. Mfumo Kristo ni mfumo wa haki na maadili aliyotufundisha Kristo.

Sidhani kama inahitaji akili ya pekee sana kuitambua hoja hii. Lakini ni wazi kuwa watu wengi Tanzania wana kiwango duni cha kufikiri au kuelewa mambo. Kwa dhana yao ya mfumo Kristo, wanaudhihaki u-Kristo, na pia wanaudhihaki u-Islam. Ila, kutokana na akili zao duni, hawatambui hilo. Kilichopo ni kuwaombea dua njema, waweze kujitambua na kujirekebisha.

Ama kweli mla kunde husahau bali mla maganda hasahau. Suala la kwamba watu hawafikiri ni matusi kwani ni haki ya kila mtanzania kueleza fikra zake na zinatakiwa zijadiliwe kama zilivyo sio kuleta matusi. Mfumo huo upo nchi hii na tukilalamika twaambiwa sisi ni wadini badala ya kujadili na tuone tutarekebishaje?
 
Kila kukicha, unajitokeza ushahidi kwamba kiwango cha kufikiri miongoni mwa wa-Tanzania wengi ni duni. Siku hizi, kwa mfano, imeibuka hii dhana ya mfumo Kristo.

Walioibuni dhana hii na ambao wanaieneza wana ajenda ya kujenga hoja kuwa mfumo wa utawala na uchumi Tanzania unaendeshwa kwa misingi ya kiKristu, na kwa lengo la kuwanufaisha wa-Kristu na kuwakandamiza na kuwanyima wa-Islam fursa na haki wanazostahili, katika nyanja mbali mbali, kama vile elimu na uongozi.

Hii ndio dhana ya msingi ya hiki kinachoitwa mfumo Kristo. Wanaojenga hoja hii wanadai kuwa serikali ya Tanzania yenyewe inaendeshwa na maaskofu kama sehemu ya uendelezaji wa huu wanaouita mfumo Kristo.

Kwanza napenda kusema, kama ninavyosema daima, kuwa kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake. Uhuru huu ni pamoja na uhuru wa kuyahoji au kuyapinga mawazo ya wengine, kufuatana na mchakato wa kujielimisha na kutafakari masuala. Ni pamoja na uhuru wa kuyapinga mawazo yako mwenyewe.

Nashangaa kwa nini mfumo mbovu uhusishwe na jina la Yesu Kristu. Dini zote mbili, u-Islam na u-Kristu, zinamtambua na kumheshimu Yesu. Yesu anatambuliwa kama Mungu katika u-Kristu. Na katika u-Islam, anatambuliwa kama mtume maarufu. Dini zote zinamheshimu sana Yesu.

Kama mfumo wa Tanzania umeoza kama inavyosemwa, hauwezi kuwa mfumo Kristo. Kuuita mfumo Kristo ni dhihaka isiyo kifani. Huwezi kuuhusisha uchafu wowote na Mungu au mtume. Kama kweli maaskofu wanaendekeza na kuulinda mfumo wa dhuluma, wanakiuka mafundisho na maadili ya Kristo. Huu si mfumo Kristo. Mfumo Kristo ni mfumo wa haki na maadili aliyotufundisha Kristo.

Sidhani kama inahitaji akili ya pekee sana kuitambua hoja hii. Lakini ni wazi kuwa watu wengi Tanzania wana kiwango duni cha kufikiri au kuelewa mambo. Kwa dhana yao ya mfumo Kristo, wanaudhihaki u-Kristo, na pia wanaudhihaki u-Islam. Ila, kutokana na akili zao duni, hawatambui hilo. Kilichopo ni kuwaombea dua njema, waweze kujitambua na kujirekebisha.

Mtaacha lini kutukana watu? watanzania ni pamoja na wewe unayeandika makala mbofu mbofu ka k.ijinga kama hizi, huu udini udini uchokozi, mnataka nini? there are so many things out there to discuss, mambo ya udni mabaya ndugu zangu, we should not entertain this, inaweza hali ikawa sivyo unavyotarajia. Ukiristo na uislamu, wengi mmezaliwa tu mkiwa na imani hizo wala hamjatafuta dini ya kweli ni ipi na wala hamtarajii, na mnajua deep down your hearts jinsi ambavyo inauma ukisikia dini yako inasemwa vibaya na uko tayari kufanya lolote! tujiepushe na hii mijadala uchwara, nenda ukahubiri kanisani au msikitini, ile dhana ya great thinkers inaenda wapi? aaaah, this is too much!
 
waambie waulize hilo swali la dini kwenye sensa halafu utajuaakina nani wengi, statistics is about credibility, siyo mambo ya kudhania!
Wewe umesema waislam ni wengi nchini!
Mbona hujatoa data zinazo onesha waislam ni wengi kuliko wakristo?
Kuto kujiamini tu ndio tatizo la watu!
 
Kila kukicha, unajitokeza ushahidi kwamba kiwango cha kufikiri miongoni mwa wa-Tanzania wengi ni duni. Siku hizi, kwa mfano, imeibuka hii dhana ya mfumo Kristo.

Walioibuni dhana hii na ambao wanaieneza wana ajenda ya kujenga hoja kuwa mfumo wa utawala na uchumi Tanzania unaendeshwa kwa misingi ya kiKristu, na kwa lengo la kuwanufaisha wa-Kristu na kuwakandamiza na kuwanyima wa-Islam fursa na haki wanazostahili, katika nyanja mbali mbali, kama vile elimu na uongozi.

Hii ndio dhana ya msingi ya hiki kinachoitwa mfumo Kristo. Wanaojenga hoja hii wanadai kuwa serikali ya Tanzania yenyewe inaendeshwa na maaskofu kama sehemu ya uendelezaji wa huu wanaouita mfumo Kristo.

Kwanza napenda kusema, kama ninavyosema daima, kuwa kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake. Uhuru huu ni pamoja na uhuru wa kuyahoji au kuyapinga mawazo ya wengine, kufuatana na mchakato wa kujielimisha na kutafakari masuala. Ni pamoja na uhuru wa kuyapinga mawazo yako mwenyewe.

Nashangaa kwa nini mfumo mbovu uhusishwe na jina la Yesu Kristu. Dini zote mbili, u-Islam na u-Kristu, zinamtambua na kumheshimu Yesu. Yesu anatambuliwa kama Mungu katika u-Kristu. Na katika u-Islam, anatambuliwa kama mtume maarufu. Dini zote zinamheshimu sana Yesu.

Kama mfumo wa Tanzania umeoza kama inavyosemwa, hauwezi kuwa mfumo Kristo. Kuuita mfumo Kristo ni dhihaka isiyo kifani. Huwezi kuuhusisha uchafu wowote na Mungu au mtume. Kama kweli maaskofu wanaendekeza na kuulinda mfumo wa dhuluma, wanakiuka mafundisho na maadili ya Kristo. Huu si mfumo Kristo. Mfumo Kristo ni mfumo wa haki na maadili aliyotufundisha Kristo.

Sidhani kama inahitaji akili ya pekee sana kuitambua hoja hii. Lakini ni wazi kuwa watu wengi Tanzania wana kiwango duni cha kufikiri au kuelewa mambo. Kwa dhana yao ya mfumo Kristo, wanaudhihaki u-Kristo, na pia wanaudhihaki u-Islam. Ila, kutokana na akili zao duni, hawatambui hilo. Kilichopo ni kuwaombea dua njema, waweze kujitambua na kujirekebisha.
Babu Lao ama kweli babu lao maana uliyaandika mazito sana na yamejiikita sana ktk Imani ya dini ambayo sisi wote tunaitumia vibaya sana ktk maandalizi ya wokovu kwanza hapa duniani na akhera..

Labda nikuase tu ya kwamba ingekuwa vizuri sana kwanza ufanhamu malamiko ya Waislaam. Binafsi yangu nilikuwa siamini na wala sina hakika ya uhalisia wa mfumo huu uliopo kwa jnsi gani unapuuza mambo muhimu sana ya kiutawala ambayo yanaweza kabisa kutafsirika kama ndio Mfumo KRISTU..

Labda niorodheshe hapa madai niliyoambiwa wazi kabisa bila kufichwa na ustaadhi mmoja alo tumia akili na hekima zaidi kuanisha mfumo uliopo na kwa jinsi gani unawakandamiza waislaam.

1. Ni swala la Mahakama ya Kadhi - Waislaam wamepeleka maombi yao kwa serikali, lakini majibu hutolewa na Wakristu iwe mapadre, viongozi na kadhalikakwa imani zao. Jambo hili huwashangaa kwa nini wakristu huingilia maswala ya Waislaam kwa serikali wakati wao waislaam hawaingilii maswala ya Wakristu wanapoiomba serikali?. Iwe haki ama sii haki - Hili sii jukumu la waumini wa Kikristu kutoa majibu kwa sababu hawakuombwa wao wala Waislam hawahitaji ruksa yao.

2. Ushirikiano wa Kimataifa na vyombo vya dini;_
Swala hili vile vile Waislaam wamekuwa wakikataliwa ushirikiano wowote na chombo ama nchi za kiislaam iwe kiuchumi ama kibiashara wakati ushirika wa madhehebu na dini nyinginezo hautafuti majibu kutoka waumini wa Kiislaam. Kwa Mfano OIC imekataliwa na wakristu lakini taasisi kama hizo za kikristu zinafanya kazi nchini bila ruksa wala ushauri toka kwa Waislaam.

3. ELIMU na AFYA
Kufuatia muafaka wa MoU, Wakristu wamerudishiwa shule na Hospital zao, wameingizwa ktk mradi wa serikali kuendesha elimu na Afya nchini lakini Waislaam wamenyimwa fursa hiyo. Na kibaya zaidi shule za Kiislaam zinachukua wanafunzi walioshindwa MITIHANI kuendelea na masomo (Failures) iwe darasa la saba, form iv na kadhalika baada ya serikali kuchagua kundi la watoto wlaiofanya vizuri na kuwapeleka shule zake au za makanisa japokuwa ada za shule hizi ni sawa au zaidi ya shule za kiislaam.

Hivyo shule za kiislaam zinafundisha walishindwa mitihani na ndio maana matokeo yake sii mazuri lakini huchekwa kutoa wanafunzi walioshindwa (failures) badala ya kufikiria kwa nini tunawapa makapi?. Nusu ya fedha za bajeti ya Elimu na Afya ni mikopo kutoka nchi za nje na hizi fedha hupewa makanisa kupitia CSSC wakati deni hilo la mikopo hiyo ni la Kitaifa na hulipwa na kodi za wananchi wote wakiwemo Watanzania. Swali lao ni kwa nini Waislaam hawakuhusishwa ktk ujenzi wa mfumo wa ELIMU nchini?.

Haya ndio kwa wake naweza yaorodhesha leo na pengine niseme kwamba YESU hahusiki na ujenzi wa mfumo huu. YESU hahusiki na kuwepo kanisa Katoliki, Anglican wala WaLutheni ni sisi binaadamu tuloamua kuitafsiribiblia tunavyofikiria kuwa sawa na kutofautiana kiasi kwamba zimekuwapo dini tofauti na madhehebu tofauti. Ufalme wa YESU unabakia palepale hata sisi tukijichanganya maana kazi yake imesha kamilika..

Vita kubwa ya Watanzania ni vitu vitatu - UMASKINI, UJINGA na MARADHI na maadam tupo ktk Ubepari ambao haufungamani na imani ya dini ktk kutoa huduma bure, basi vita hivi vinapiganwa kwa kutazama Faida (who is making the Mulla) na wanaofaidika na mfumo huu ni Wakristu. Money and profit ndioo maendeleo ya jumuiya. Hivyo kipigo wanachokipata waislaam ktk Ujinga na Maradhi ni kipigo cha kiuchumi na hakika bila fedha huwezi kujenga msingi jamii. Kama utaachwa nyuma ktyk mamboa haya matatu basi kamwe hutaweza kuendelea na mfumo uliopo umehahakikisha waislaam hawapati silaha tosha za kupambana na maadui hawa..

Ukiweza kunipa majibu toka hayo maswali haya matatu, Kwa nini jamii ya Waislaam inawekewa vikwazo pengine tunaweza kupata suluhu. Ni vizuri sana kujadili kitu kwa kutumia vichwa vyetu badala ya kumwingiza YESU maana sidhani kama maamuzi haya yametokana na YESU bali baadhi ya watu walikaa na kuamua hivyo bila kiapo wala biblia mkononi..Na wala haisaidii kabisa kuutukana Uislaam kwa sababu WASABATO ni Wakristu na wanaheshimu SHERIA..

Na Tawala zote duniani zinaheshimu sheria walizotunga mbele ya kila kitu..tatizo mloshindwa kulielewa nyie wenzetu ni kwamba mnazikataa sheria za Mungu na kukumbatia sheria za binadamu ambazo mnaziweka mbele ya zile za Mungu.. Sii vibaya kukubaliana kutokubaliana lakini kukashifu dini ya mtu inaonyesha wazi jinsi gani tulivyokuwa magarasha kichwani..
 
Kila kukicha, unajitokeza ushahidi kwamba kiwango cha kufikiri miongoni mwa wa-Tanzania wengi ni duni. Siku hizi, kwa mfano, imeibuka hii dhana ya mfumo Kristo.

Walioibuni dhana hii na ambao wanaieneza wana ajenda ya kujenga hoja kuwa mfumo wa utawala na uchumi Tanzania unaendeshwa kwa misingi ya kiKristu, na kwa lengo la kuwanufaisha wa-Kristu na kuwakandamiza na kuwanyima wa-Islam fursa na haki wanazostahili, katika nyanja mbali mbali, kama vile elimu na uongozi.

Hii ndio dhana ya msingi ya hiki kinachoitwa mfumo Kristo. Wanaojenga hoja hii wanadai kuwa serikali ya Tanzania yenyewe inaendeshwa na maaskofu kama sehemu ya uendelezaji wa huu wanaouita mfumo Kristo.

Kwanza napenda kusema, kama ninavyosema daima, kuwa kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake. Uhuru huu ni pamoja na uhuru wa kuyahoji au kuyapinga mawazo ya wengine, kufuatana na mchakato wa kujielimisha na kutafakari masuala. Ni pamoja na uhuru wa kuyapinga mawazo yako mwenyewe.

Nashangaa kwa nini mfumo mbovu uhusishwe na jina la Yesu Kristu. Dini zote mbili, u-Islam na u-Kristu, zinamtambua na kumheshimu Yesu. Yesu anatambuliwa kama Mungu katika u-Kristu. Na katika u-Islam, anatambuliwa kama mtume maarufu. Dini zote zinamheshimu sana Yesu.

Kama mfumo wa Tanzania umeoza kama inavyosemwa, hauwezi kuwa mfumo Kristo. Kuuita mfumo Kristo ni dhihaka isiyo kifani. Huwezi kuuhusisha uchafu wowote na Mungu au mtume. Kama kweli maaskofu wanaendekeza na kuulinda mfumo wa dhuluma, wanakiuka mafundisho na maadili ya Kristo. Huu si mfumo Kristo. Mfumo Kristo ni mfumo wa haki na maadili aliyotufundisha Kristo.

Sidhani kama inahitaji akili ya pekee sana kuitambua hoja hii. Lakini ni wazi kuwa watu wengi Tanzania wana kiwango duni cha kufikiri au kuelewa mambo. Kwa dhana yao ya mfumo Kristo, wanaudhihaki u-Kristo, na pia wanaudhihaki u-Islam. Ila, kutokana na akili zao duni, hawatambui hilo. Kilichopo ni kuwaombea dua njema, waweze kujitambua na kujirekebisha.

Nchi yetu imefikwa na tatizo na dawa ya tatizo hili ni kulizungumza waziwazi ili ipatikane sulhu vinginevyo tutajafikwa na janga ambalo wenzetu limewafika. Naweka hapa chini fikra zangu kutoka mswada wangu kuhusu tatizo la udini nchinin kwetu. Hiki ni kipande kidogo kutoka katika kazi hiyo Christian Hegemony and the Rise of Muslim Militancy in Tanzania. Hii ilikuwa mada ambayo niliitoa Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin mwaka 2011. Mada hii iligusa hisia za wengi.

Introduction

In order to understand the Tanzanian political environment and to appreciate this study we first need to establish even in a nut shell the source of the problem. Why is the Church in Tanzania and particularly the Catholic Church in control of the government and all that it entails? Why are Muslims, fifty years after independence still backward, uneducated and form the lower strata of society? Is this by default or design? Having seen this we have to analyse and deeply explore the hopes and aspirations of Muslims in free Tanganyika as Tanzania was known then and ask, are Muslims satisfied with this unequal status? We also have to ask again did Muslims spearhead the struggle for independence so that the Church could replace the colonial government. Although for reasons which are to be deduced later, this historical fact is still in contention. No one can ignore the role of Islam and Muslims in resisting foreign domination beginning with German colonialism when in 1905 Muslims rose up in arms against Germans in Maji Maji War to free Tanganyika from bondage; to the period of British rule when Muslims formed the backbone of resistance against British rule.

Subsequently Muslims dominated both labour and nationalist politics. Tanzania Mainland celebrates fifty years of independence this year but the role of Muslims in resisting foreign rule and in liberating Tanganyika from colonialism has not been requited nor have the heroes of independence struggle been honoured.[1] We again have to pose a question why is this so? Is it that Tanzania is an ungrateful nation and therefore hates its heroes? Answers to all those questions will lead us closer to understanding the problem which Muslims in Tanzania face. Answers to these questions will make us reflect and uncover reasons which caused Muslim independence aspirations not to be realised. This is now the bone of contention between Muslims and the government. Muslims without mincing words are now pointing an accusing finger to the Church particularly the Catholic Church which in connivance with President Nyerere for being anti Islam and for frustrating the hopes and aspirations of Muslims in free Tanganyika, a country they liberated from colonialism in 1961.[2]

History in Revision

Muslims are now organising nationwide mass rallies which openly and in live broadcasts denounce the church, criticise the government and church agents within the ruling party Chama Cha Mapinduzi (CCM) and the Parliament for oppressing Muslims. Seemingly derogatory words like pandikizi (singular) and mapandikizi (plural) meaning turncoats; or the new coined word Mfumo Kristo roughly meaning Christian dominance are now part of the Muslim and Swahili vocabulary. These analogies are used freely in the Muslim media and among Muslims in every day conversation. But what usually thrills Muslims and utterly significant showing that times have changed is when in the rallies and in normal discussion Muslims refer to Nyerere hitherto known respectfully as Baba wa Taifa as Baba wa Kanisa, meaning Church Elder.[3] The move by the Catholic Church to make him a saint has not helped matters. More so it proves all the allegations levelled against Nyerere that he never was a nationalist but a Catholic zealot. Respect and love which Muslims once had for Nyerere has been completely wiped out. The new generation of Muslims no longer believe in the official history of TANU and the propaganda that it was Nyerere who single handed defeated the British. Muslims instead are honouring the forgotten heroes of independence movement and in so doing invoking emotions particularly in the new generation to stand up against oppression as their forefathers had done against Germans and the British. Muslim heroes of the Maji Maji War like Suleiman Mamba, Ali Songea Mbano,[4] and Muslim nationalists like Abdulwahid [5] and Ally Sykes,[6] Dossa Aziz, Sheikh Hassan bin Amir,[7] Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh Yusuf Badi, Bibi Titi Mohamed,[8] Bibi Tatu bint Mzee, Bilali Rehani Waikela,[9] Ali Migeyo[10] and others are now part of nationalist history which was suppressed for many years.[11]

Muslims are demanding the restoration of their history and honour as true liberators of Tanganyika. This is unprecedented. One can only speculate and wonder where this would lead to. Can we identify this phenomenon as corrective and revision of history or is it a lesson of anarchy in recording history?[12] The result of all this is that the Church has been made to stand naked. That the Church did not play any role during Maji Maji[13] or during the struggle against the British or that it has worked hand in hand with the government to sabotage Islam and Muslims is now common knowledge.

[1] On 27 th April, 1985, Julius Nyerere, before stepping down from power, in a colourful ceremony at the State House grounds, conferred a total of 3,979 medals to Tanzanians who had contributed to the development of the nation. None of the Muslim patriots who spearheaded the independence struggle was in that list. The names of those honoured make very interesting reading.

[2] Catholics form 76% of all members of Parliament the remaining 24% seats are divided between Christians of other dominations and Muslims. Muslims control a mere 6% of the seats. Most areas which are under developed in Tanzania mainland are areas with Muslim majority like Kigoma, Tabora, Kilwa, Mtwara, Lindi etc. These areas are now re-examining themselves and are gradually turning into local factions of radical Muslim politics reminiscence of the era of nationalist politics of the 1950s. This could be a source of civil unrest in the very near future. Signs of this have begun to show in the recurrent violent conflicts between Muslims and the government. Tanzania has experienced the Buzuruga Muslim-Sungusungu Conflict (1983), Pork Riots (1993) and Mwembechai Upheaval (1998). For more information See Hamza Mustafa Njozi, Mwembechai Killings and Political Future of Tanzania, Globalink Communications Ottawa, 2000. (The book is banned by the government). In all these conflicts, Muslim blood has been shed. In between these conflicts Muslims have sent several petitions to the government requesting it to look into these problems but all of them have been ignored. As a result of this Muslims from all regions of Tanzania met in Dar es Salaam at Masjid Tungi in 1990 and issued the Tungi Declaration which among other things stated that Muslim should prepare to defend their rights by all means even if it means by force of arms.

[3] The late Prof. Haroub Othman after reading Sheikh Ali Muhsins book Conflict and Harmony in Zanzibar and the writers book The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 -1968 The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press, London 1998 and having come across hitherto unknown information on Nyerere was devastated because he was a great admirer of Nyerere as a patriot and a nationalist. The two books had painted him differently. Prof. Haroub confronted Nyerere and told him that the allegations in those two works have tarnished his image and he advised him to respond to them. Nyerere never did. Christian lecturers at Dar es Salaam University are discouraging students from making references to those two books. Dr. Harith Ghassanys book Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru, has also come up with more information on Nyerere hitherto unknown in the Zanzibar Revolution and the bloodbath which followed.

[4] In all historical references to Maji Maji War hero and Chief of Wangoni Ali Songea Mbano, his Muslim name Ali would be omitted and he would be referred to as Songea Mbano.

[5] Mohamed Said, The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 1968), The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika Minerva Publishers, London, 1998.

[6] Mohamed Said, Broken Dreams, The Life of Ally Kleist Sykes, Phoenix Publishers, Nairobi 2011 (Forthcoming).

[7] Issa Ziddy, Sheikh Hassan bin Ameir (1880-1979). Also See Mohamed Said, Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27[SUP]th[/SUP] February 4[SUP]th[/SUP] March 2004.

[8] Bibi Titi was recruited into TANU by Schneider Abdillah Plantan and began to mobilize people particularly women to join the party even before he came to know Nyerere.

[9] Bilali Rehani Waikela one of the TANU founder members in Western Province in 1955 and Regional Secretary of the East African Muslim Welfare Society (EAMWS) was detained by Nyerere in 1964 for mixing religion and politics. His personal papers were of great help in understanding the EAMWS crisis of 1968 and the reasons why Nyerere detained prominent sheikhs and banned the society in 1968. A documentary of his political life has been made and although not officially recognized as a patriot Muslims now consider him as one of the heroes of the independence movement. For more information see Mohamed Said, In Praise of Ancestors, Africa Events (London) March/April 1977.

[10] G. Mutahaba, Portrait of a Nationalist: The Life of Ali Migeyo, East African Publishing House, 1969.

[11] Maji Maji Museum in Songea has been greatly desecrated removing all signs of Muslim symbols during the Maji Maji War with Germans. The Maji Maji Museum at Peramiho under the Catholic Church has closed its doors to young Muslims for fear of criticism for distorting history. All Muslim symbols in Maji Maji War against Germans have been obliterated in the Maji Maji Museum.

[12] A childrens book authored by the current writer, Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2007 has been blacklisted and cannot be included as a reader in schools because it contravenes the official history.

[13] Yusuf Halimoja, Historia ya Masasi, East African Literature Bureau, Nairobi, 1977 pp 163 175 gives a narration how Christians fought alongside Gerrmans during Maji Maji. Also see P. Gerold Rupper, OSB, Pugu Hadi Peramiho: Miaka 100 wa Wamishionari Wabenediktini Katika Tanzania, Benedictine Publications, Ndanda Peramiho, 1980, pp 31- 42.
 
tatizo lipo....hawasemi kwa bahati mbaya...kuna mifano wanaitaja...sasa hizi ni tuhuma zina elekezwa kwa serikali...ni hili tangu zamani ..serikali inatuhumiwa...wakati wa mwalimu hali ya waislam ilikua mbaya zaid...sisi kama raia wa kawaida hatuwezi kujibu hoja hizi...ni serikali inatakiwa ije safi...ijikoshe mbele ya jamii...itamke kwamba serikali mawaziri, wabunge, makuu wa mikoa,wa wilaya, bodi za mashirika , wakurugenzi, jeshi ,polisi,mahaka..
Inatakiwa mfano waziri mkuu akanushe madai haya aseme wazi kwamba serikali haibagui na mtendaji yoyote ambae anaweka dini yake mbele kwenye maamuzi basi atawajibishwa.
Sasa serikali inakaa kimya..tena kimyaa..cha mshindo..maana yake nini? Kisheria ukikaa kimya basi umekubali yanayosemwa...
Na upande wa kanisa ....linatuhimiwa....nalo kuwaashindiza waumini wao waliopo serikalini walipendeee kanisa na wawabane waislam..sasa hapa tuhuma zipo kwa kanisa ...nao..wawatoe mashaka ....waislam kwamba wao hawafany hayo...ila wanataka uadulifu katika mambo ya serikali.
Lakini nao wamekaa kimya...maana yake nini ?
Sasa sisi tukikaa hapa tukijibu kwa niaba ya serikali ama kanisa shutuma zitakuwepo...tu...lakini hebu tujikumbushe kidogo historia...kanisa linaonekana kusema sana anapokuwa rais muislam...lakini akiwa mkrissto ..atauza, nbc, atauza madini yote,atanunua ndege mbovu,reli itabinafsishwa kinamna namna..lakini hata siku moja hawa wezi kulaumu..hata siku moha....kwao hakuna ufisadi...na hpa ndipo penye mashaka
lakini tofauti yao na masheikh ...wao akiwa mkristo akiwa muislam madam amekosea watamsema...
Tuwachieni kanisa na serikali wajibu hoja hizi..
Mutambue waislam hawana ugomvi na wakristo bali serikali kwa kukubali mashindikizo
Imetulia
Straight corner said:
My take: Raisi awe anafanya teuzi za hawa viongozi kwa kuzingatia utendaji/uwajibikazi mzuri wa wateule hawa na hii itasaidia kuondoa hii dhana ya udini serikalini.
Bado mfumo utatulalia Waislamu Mkuu!
Tuchukulie mfano (mfano) Raisi atapelekewa listi ya candidates watano kwa ajili ya post ya Ukatibu Mtendaji NECTA katika hiyo listi wanne watakuwa Wakatoliki na mmoja ni dhehebu jingine la Kikristo! na tutaambiwa kuwa Katibu Mtendaji amechaguliwa na rais ambaye ni Muislamu mwenzenu, lakini ukweli wenyewe utakuta ni mfumo ndio uliomuweka huyu Katibu Mtendaji pale.

Unafikiri Mkuu wa Shule ya Ndanda alipata wapi jeuri ya kukaidi agizo la Waziri wa Elimu?!.... hivyo solution nyingine yoyote ile isipokuwa kuubadilisha huu mfumo ni kujisumbua na kupoteza wakati tu.
 
Viongozi wa serikali wakristo wanatumikia kanisa badala ya wananchi e.g. MoU haina faida kwa wananchi wa Tanzania lakini ina faida kwa kanisa na walioubariki mfumo huu wa kinyonyaji ni wakristo

Viongozi wa serikali wakristo wanapowabagua waislam na kuwapendelea wakristo kwenye ajira na kujiunga na sekondari wanafanya hivyo ili kupata paradise (na kuwa please maaskofu) bila kujali hatari kubwa kwa nchi

Tutafika tu; hakuna dhuluma itakayodumu milele
 
Hii topic imekaa kimtego na kiasi flani kama uchokozi kama sio uchonganishiKwa upande wangu sihitaji data kuchangia hoja hii bali nitaenda na uhalisiaViongozi wakuuNyerere 1961 – 1984 Alikuwa na timu yake kimuundo kuanzia chini mpaka juuMwinyi 1985-1995 Alikuwa na timu yake kimuundo kuanzia chini mpaka juuMkapa 1995-2005 Alikuwa na timu yake kimuundo .......................mpaka juuKikwete 2005 .....

Wapi forodhani sekondari?
 
UKISTO UISLAM ni divide and rule strategy ya Serikali.. Ukiweza kuwagawa utaweza kuwatawala, kuwaibia na hata kuwauwa kirahisi na wasiweze kuuliza. Wabelgiji waliposhindwa kuitawala Rwanda walihubiri mfumo kabila Mhutu na Mtutsi. Wote tunajua alifanikiwa kuwatawala na kuishi kati yao bila yeye kupata madhara.

Leo hii miaka 50 baada ya uhuru, Treni imekufa, Ndege hakuna, wawekezaji wamechukua migodi wazawa wanateswa na kuuawa. Wenye hela wanadhulu bila kuchuliwa hatua, umaskini unazid kuongezeka, ardhi inaporwa mijini (Kigamboni) na vijijini, polisi wanaua raia bila kuchukuiwa hatua. Elimu ndio kaputi kila kiongozi anapeleka mtoto nje au internatonal school gov school zimebaki kwa walala hoi wakati miaka 10 tu iliyopita kufaulu lasaba na kuchaguliwa shule ya serikali ilikua ni jambo la Heshima sasahivi ni kinyume. Wakati huo huo watawala wanatuambia tunaweza, tumesubutu na tunasonga mbele.

Tukikubali kuwagombanishwa kwa maneno yakijinga tutaendelea kuona umaskini, dhuluma ikikua kushamiri na kuota miziz katikati ya waTZ wote bila kujali dini zao. Mwenye hela atamyanyanyasa asiyekua nazo bila kujali dini yake mfano halisi na wakaribu ni binti aliyenyang'anywa mtoto mchanga na kunyonyeshwa na inlaw's wake (kwa wanaoangalia habari ITV). Tuwe makini na tuinidhamishe serikali na kuacha mijadala yakututenga kwa faida ya watawala dhalimu.
 
Kwanza,penda sema hiv, watanzania hatujuan kwa din zetu wala kabila zetu,wewe uliyeleta Ujinga huu namashaka na akili yako,
Pili,ukisema "MFUMO KRISTO"Inamaana unongelea udini,kuhusu elimu,sisi waislam tuna vyuo vikuu vingapi hapa Tanzania?sekondary ngap?na za msingi ngap?

Mimi nakifaham chuo kimoja cha morogoro niambie vingine,wakristo wanavyo hiv:Tumain iringa,mwanza,Augustine mwanza,arusha,dar,ST.JOSEPH,Morogoro,n.k,na sekondary zao ni nying,hata sisi watoto wa wakiislam tunasoma ktk shule zao,huoni kwamba wanafursa kubwa ya kuwa na wasom wengi?

Katika uongozi,Rais wako dini gan?makam Rais pia?mawaziri wote hawa ni waislam utabisha nalo?mfano:
Adam malima naibu waziri kilimoDr.,Shukuru kawambwa,waziri elim,Dr.Aly mwinyi,wazir afya,Shamshi vuai nahodha,waziri wa ulinzi,hao ni baadh yao pamoja na manaibu wao,unajua wewe usichokoze watu kwa udini na kabila zao.
Kwanza hili jukwaa la kisiasa dini za nini?

NB:The stupid qustion make sens than stupid words,
Samahan kama nitakua nimekukera ila liwe fundisho kwa wenye UBAGUZI, kama wewe,kazi njema.
 
Je na sisi wengine ambao hatupo kwenye uislam au ukristo inakuwaje? Hii yote ni dhana duni watanzania wote kwa ujumla wetu tuna hali mbaya wakristo, waislamu na sisi wengine tusiofungamana na hizi dini za wageni wote tupo kapu moja la umaskini wa kutisha.

Kuanza kuangalia eti hoo mbona wenzetu wanakula zaidi ni upotoshwaji, tz yote imechoka na haya maneno hayasaidii, kwa sasa tujadili jinsi gani ya kuendeleza nchi yetu toka kwenye huu umaskini wa kutupwa kwenda kwenye hali nafuu zaidi hicho ndio cha msingi sio nani dini gani...vilevile uteuzi uwe kwa uwezo wa mtu na si dini yake.

Hawa wezi wa sasa na wabadhirifu mbona wanatoka dini zote? Hakuna mwenye nafuu watu wateuliwe kwa uwezo wao na si dini, Period.

Mi sijali nani au kuna mawaziri au wakurugenzi wangapi waislamu au wakristo najali kuangalia utendaji wa mtu au taasisi wanazoongoza kama zinafanyakazi kiufanisi, hicho ndio kigezo cha msingi na nafikiri watz wengi pia ndio kitu wanachotaka na sio dini ya mtu...after all hizi dini zote mbili zililetwa hapa kwetu kutugawanya (divide and rule), tukiendelea hivi hiyo dhana ya kikoloni itaendelea kututafuna milele...tuachane na hizi dini za kigeni kuleta mapinduzi ya kweli ya kifikra, bila hivyo tutaendelea kuwa watumwa milele
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom