dhambi nyingine ni zakujitakia

pomo

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
267
31
kunajamaa mmoja alikuwa ni muoga sana wa kutenda dhambi, siku moja shetani akamtembelea na kumwambia kijana nakuomba uzini na mke wa mtu nitakulipa pesa, jamaa akakataa na kusema hiyo ni dhambi kubwa sana siwezi kuifanya namuogopa mungu. basi shetani akamwambia naomba uue mtu ntakulipa pesa, yule jamaa jibu likawa ni lilelile kuwa hataki kutenda dhambi. shetani akamwambia ukinywa pombe ntakulipa mara tatu zaidi ya hizo dhambi mbili. basi jamaa akakubali kunywa pombe na akaenda sehemu ipouzwa hiyo pombe alipolewa akaanza kumtongoza yule muuza pombe, yule mama muuza akamwambia yeye ni mke wa mtu.jamaa akasema yeye itakuwa ni kwa siku hiyo tu huyo mama akakubali, wakati wanamalizia kutenda mume wake akatokea na ugomvi uka zuka, jule jamaa kwa bahati mbaya akampiga mume mtu na kitu kizito kichwani na akafa. shetani alirudi na kumwambia yule jamaa mbona umefanya dhambi zote tatu wakati tulikubaliana moja tu!
 
sio pombe, ni ulevi.
Ulevi noumer. mbona ukinywa kama mwanangu makaveli (to your limit haina nomaa!)
tatizo wengine wanataka wazikomoe.
 
To me at least starehe moja inatosha; kama unavuta sigareti, vuta tu sigareti; kama unakunya pombe pekee yake na kama mademu pekee yake usitumie starehe zote si vizuri. Inamaliza pesa na maisha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom