Device drivers - tueleweshane, tujadiliane tuulizane

Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,937
1,437
Naam wana jf teknical forum hope mambo muswano. .

Siku za karibuni nimekua naona mabandiko na matatizo ya watu mbali mbali kuhusu madereva(Drivers ) wa computer na laptop zao. Ni sababu hiyo nimeamua hapa kufungua uzi maalum wa device driver tuzielew.ni nini

  • zinafanyaje kazi
  • zina mtatizo gani
  • zinapatikana wapi
  • Kwenye computer zinahifadhiwa wapi
  • zinasimikwa vipi
  • na hata ikiwezekana zinakuwa programmed vipi. lol ( I never like programming though)
  • Nk
Yap si vizuri tukaridhka na kile unachojua . Tutaishia kua end user tu. Tupende kujiuliza maswali magumu........

Ni matumaini yangu wataalamu mbali mbali watashusha ujuvi wao kile wanchofahamu kuhusu device drivers . kwa manufaa yetu
sote...

Driver ( device driver kwenye computer ni nini)?


Driver ni kipande cha program /software kinachoratibu ufanyakzi kazi wa kifaa(device/Hardware fulani ) Devce/harware au vifaa vya komyuta/laptop kama Keyboard, Monitor(VGA) Printer, CDROM, HDD Ethernet card (LAN) Wireless vyote vina driver.

Hizi driver au hawa "madereva" ni kama mtu kati au "mkalimani "wanayesaidia OS (Iwe ni Linux Window au hata Mac) na hardware baadhi yake nilizotaaja nilizotaja hapo juu kuwasilinaa bila matatizo na hivyo kuwezea kompyuta kufanya kazi kama kifaa kimoja.

Kuna baadhi ya driver kam za keybord au kipanya (mouse) hazisumbui sana sababu ni universal. Bila hata installation ya driver unaweza pachika keyboard yeyote au Mouse zinafanya kazi. Lakini una drivers nyingine zinahitaji kusimikwa au kila unapfanya inatalltion ya OS au unapounganisha kifaa.

Tovuti ya za Wikipedia na wisegeek zimemeandika pia maelzo ya kitaalmu zaidi kuhu hawa madereva

Program hizi za device driver zinahifadhiwa wapi?


Mara nyingi tukifanafanya instaltion ya hizi driver Autamaticaly zinapelekwa sehemu. Si wengi tunajiuliza au tunajua niwapi zinapohfadihwa . Watu wa Mac watatuambia lakini kwa wale wenye windows 7 na Vista drivers za vifaa mbali mbal zinawekwa kwenye C:\Windows\System32\DriverStore. Wenye XP mara nyingi madereva wanapelekwa kwenye location C:\Windows\System32

Driver zina mafaili gani?
Katika windows mara nyingi driver zina file la kuu mbili

  • .sys ambalo ndo driver yenyewe
  • .inf hili ndo exeutable ambalo kama unainstall manually ndio linatauwa kutafutwa na kukimbizwa(run)
File nyingine ndani ya driver ni .XML na .PNF.

UMEISTALL OS UNATAFUTA DRIVER UZIPATE WAPI?


Ukiwa unatafuta madereva wa deice fulani kwenye kompyuta kimbilio la kwanza linatakiwa kuwa ni tovuti ya watengezaji wa kompyuta( eg Toshiba, HP, DeLL, Acer,etc )kwenye tovuti hizi kuna sehemu maalum ya Drivers na Download.

Drivers zikikosekana huko labda kwa kuwa umeweka OS ya kisasa zaidi tofauti na lengo la watengenzaji wa koyuta unaweza kupata driver kwenye TOVUTI ya watengenzaji wa drivers zenyewe eg kama ni driver ya Video unaweza tembelea ATI, au Intel au kampuni nyingine iliyotengeneza hiyo driver. Kama ni driver ya sauti(Audio) inaweza kuwa Realtek. Kama ni driver ya Network inawezakuwa reltek au Atheros .
Msisitizo
Kwa hiyo ni jambo la muhimu ni kujua ni driver model gani unatafuta.Yaani utambue harwdware Model ya driver unayotafuta mfano kama ni network Kwa windows ukienda kwenye device manager utaona aina ya driver unatokaiwa kutafua kutona na jina la hardware . mfano Broadcom, Realtek , Atheros ATI radeon

Device manager kwenye widnows 7 itakuonyesha kitu kama hiki na kama kuna driver yenye tatizo itakuwa na ka alama ka mshago na rangi ya njano. So ni muhimu ukiwa na tatizo la driver kutumia device manager kupata mwongozo. Zaidi soma hapa kuhusu how to use device manager

Devicemanager_Win7_2.jpg


Sehemu ya miwsho kutafuta "madereva wa kompyut"a ni tovuti kama CNET na google na nyinginezo kama drivers.com. Huku pote ni muhimu ujue model ya harware unayotakiwa utafuta driver yake . Brand ya kompyuta tu inawweza isisaidee sababu inatoekea brand moja inaweza kutumia model tofauti ya device kulingana na ulinunua mua gani au sehemu gani


Baadhi ya viunganishi vya watengenzaji kompyuta na driver unapoweza kupaua driver ni

Toshiba- Ingiza detail za brand model OS na series na driver unazotaka
Acer - Chagua sytem au brand ya moashine yako na fuata maleeso mpaka utapa driver husika
HP - Ingiza model then fuata maelekezo

Na baadhi ya kampuni zinazotenegza driver unapoweza kuakua driver ni
Realtek - Hwa ni maarufu kwa driver za Audio na NIC
ATI- VGA za ATI zinatengenzezwa na kampuni ya AMD . Ukiingiza detail. Pia wanatengeneza na TV tune na vifaar . Uijaza detail za driver utafiishw aukurasa wa kupakua

Nawasilisha kwa Nyongeza, punguzo kuponda au kupenda, maswali etc

Next japo sipendi program nitadadavua ni vipi drivers zinakuwa programmed na mengineyo. Si google ipo ni kusoma, kuelewa na kuchanganya na za kwako..........









 
Neno madereva siyo tafasiri sahihi. Neno sahihi ni programu unganishi au viunganishi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom