Dereva wa gari la mashindano kizimbani - HII IMEKAAJE?

Ustaadh

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
413
19
DEREVA Dharam Pandya (29) mkazi wa Dar es Salaam, ambaye inadaiwa alisababisha vifo vya watu watano katika ajali ya gari la mashindano iliyotokea juzi mkoani Morogoro jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani humo na kusomewa mashtaka 16.

Mbele ya Hakimu Mkazi,Maua Yusuph, Mwendesha Mashtaka Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Augustine George aliieleza mahakama kuwa, Pandya, anashitakiwa kwa makosa 16, ikiwa ni pamoja na kusababisha vifo vya watu watano na kujeruhi wengine 13.

Alidai kwa kutambua ni kinyume cha sheria za usalama barabarani kifungu cha (40) (i) 27 A na kifungu kidogo cha (ii) A cha mwenendo wa makosa ya barabarani, mshitakiwa aliyekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili KAK 9208 wakati wa mashindano ya magari yaliyofahamika kama Morogoro Pathfinder alitenda makosa hayo.

Alidai kuwa, mshitakiwa katika makosa matano ya kwanza anashitakiwa kwa kuendesha gari kwa mwendo kasi na uzembe hali iliyosababisha gari kuacha njia na kusababisha vifo hivyo na majeruhi hao eneo la Mikese.

Alidai kuwa mshitakiwa aligonga pikipiki yenye namba za usajili T 449 BCD iliyokuwa ikiendeshwa na Nasar, pia aligonga gari lenye namba za usajili 435AEC iliyokuwa ikiendeshwa na Mohamed Amry na pia aligonga baiskeli mbili na kusababisha vifo vya watu watano pamoja na majeruhi 13.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mshitakiwa huyo bila halali na akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria alisababisha vifo vya watu watano ambao ni Wilson Job (14) , Kulwa Deus, Said Mohamed (40), Jacob Mshaka ( 6) na John Job ( 9).

Pia iliendelea kudaiwa mahakamani hapo kuwa mshitakiwa huyo katika ajali hiyo alisababisha majeruhi ya watu 13 ambao ni Alex Musa, Hadija Said,Hamis Rajab, Mwanaid Said, Abdul Shakur, Mgelwa Deus, Idd Mtamwa, Juma Abdala Shimba, Daniel Masanja, Shukuru Roma, Mwanahamisi Rajab na Nassar Daud.

Mshitakiwa alikana mashitaka hayo, upelelezi wa kosa hilo bado haujakamilika na kesi hiyo kuahirishwa hadi Desemba 28 itakapotajwa tena na ameachiwa kwa dhamana ya Sh milioni 10 na wadhamini wawili.

...................................................................................................
Nawapa pole waliofiwa na wale waliojeruhiwa....kwa mnaojua sheria, ni halali kumfungulia mashitaka dereva wa gari la mashindano?
 
Back
Top Bottom