Dereva wa daladala afungwa kwa kutoza nauli kubwa...

Dickson Ng'hily

JF-Expert Member
Oct 22, 2010
451
485
MAHAKAMA ya Wilaya ya Chato mkoani Kagera imemhukumu kifungo cha mwaka mmoja dereva wa gari dogo la kusafirisha abiria maarufu kama vipanya, baada ya kushindwa kulipa faini ya shilingi 600,000 baada ya kupatikana na hatia ya kubeba abiria wengi na kuwatoza nauli kubwa zaidi ya kiwango kinachotakiwa kisheria.
Akisoma mashikata mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Chato, Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi, Mathias Maduhu, alidai kuwa Mei 26, mwaka huu mshitakiwa Boniphas Suka alikamatwa eneo la Kijiji cha Muungano majira ya saa sita na dakika 30 mchana akiwa na abiria 12 kwenye gari alilokuwa akiliendesha kinyume cha sheria za usafirishaji wakati gari lake likiwa na uwezo wa kubeba abiria watano.
Akisoma mashitaka dhidi ya mshitakiwa alisema alikuwa akiwatoza nauli abiria kati ya shilingi 4,000 hadi shilingi 5,000 katika umbali wa kilometa 80 wakati nauli halali iliyopangwa na Sumatra ni shilingi 2,500 .
Mshitakiwa alikiri kosa na kutakiwa kulipa faini ya shilingi 600,000 na aliposhindwa kulipa faini hiyo mahakama ilimhukumu kifugo cha mwaka mmoja jela

Source: Tanzania Daima
 
tajiri wake pia ameshindwa kumnusuru mwajiriwa wake?, ahaaa nimekumbuka, inabidi askari magereza amwongezee
miaka ya kukaa huko kama alivyokuwa anaongeza yeye kwenye nauli
 
Tukiwafanyia hivi wataacha ujinga.
Mwajiri hajui gari lake kama linaingiza mihela kiasi hiki.
 
tajiri wake pia ameshindwa kumnusuru mwajiriwa wake?, ahaaa nimekumbuka, inabidi askari magereza amwongezee
miaka ya kukaa huko kama alivyokuwa anaongeza yeye kwenye nauli

good wamezoea kutuhangaisha,MARA WAKATISHE RUTI MARA SIJUI NINI AAAHA WACHA AKACHAFUE NDOO!WAJE HUKU DAR BWANA
 
MAHAKAMA ya Wilaya ya Chato mkoani Kagera imemhukumu kifungo cha mwaka mmoja dereva wa gari dogo la kusafirisha abiria maarufu kama vipanya, baada ya kushindwa kulipa faini ya shilingi 600,000 baada ya kupatikana na hatia ya kubeba abiria wengi na kuwatoza nauli kubwa zaidi ya kiwango kinachotakiwa kisheria.
Akisoma mashikata mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Chato, Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi, Mathias Maduhu, alidai kuwa Mei 26, mwaka huu mshitakiwa Boniphas Suka alikamatwa eneo la Kijiji cha Muungano majira ya saa sita na dakika 30 mchana akiwa na abiria 12 kwenye gari alilokuwa akiliendesha kinyume cha sheria za usafirishaji wakati gari lake likiwa na uwezo wa kubeba abiria watano.
Akisoma mashitaka dhidi ya mshitakiwa alisema alikuwa akiwatoza nauli abiria kati ya shilingi 4,000 hadi shilingi 5,000 katika umbali wa kilometa 80 wakati nauli halali iliyopangwa na Sumatra ni shilingi 2,500 .
Mshitakiwa alikiri kosa na kutakiwa kulipa faini ya shilingi 600,000 na aliposhindwa kulipa faini hiyo mahakama ilimhukumu kifugo cha mwaka mmoja jela

Source: Tanzania Daima

Wallahi, haya ni masihara ya Tanzania. Mtu anagonga bajaji na kuua watu wawili na kuendesha gari pasi leseni anapigwa faini ya laki saba.

Mwingine anajaza abiria na kuongeza nauli anapigwa faini ya laki sita!!!!!

Tujiulize na kutafakari, je sheria zetu ni kwa maslahi ya nani??

Huyu wa daladala na aliyejenga mashimo mawili ya vyoo kwenye shule ya msingi kwa milioni sabini nani ana kosa kubwa???
 
Back
Top Bottom