Dereva aingiza basi mtaroni kisa nyimbo za CCM zinamkera!

security guard

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
799
603
attachment.php


Basi ilikouwa limebeba wanachama wa chama cha mapinduzi kuelekea kwenye mkutano wa hadhara likiwa limeharibika vibaya na kusababisha majeruhi kadhaa na watatu kulazwa kwenye hospitali ya Huruma, wilayani Rombo. Dereva wa basi hilo inasemekana alikuwa hataki kusikia nyimbo za CCM kwa sababu yeye ni CHADEMA.

Akawaambia atawatia mtaroni kama wataendelea kuimba, baada kuona juhudi za kuwanyamazisha zimekwama akalitia kweli basi mtaroni na kusababisha ajali mbaya.......je wadau mnaonaje ukomavu wa kisiasa wa huyu dereva?????
 

Attachments

  • 4.jpg
    4.jpg
    51.8 KB · Views: 3,061
msema kweli mpenzi wa Mungu ile iyena iyena inauzi kweli kweli, halafu ikianza sasa kumekucha jogoo limeshawika dodoma ni noma, lkn huyo dereva nae kazidi angevumilia tu bana
 
Huo ni uongo, hakuna anaeweza kukata tawi alilokalia. Kwa mantiki hiyo mtu hawezi kukadiria nikilitupa gari mtaroni mimi nitasalimika au nitaumia kidogo.

Jamaa anataka kutuletea stori kama za Ngongo na Lema.

Mkuu ukiangalia kwa makini hilo gari huwezi amini kwamba lilitumbukizwa mtaroni! Huenda hii ni miongoni mwa hadith tamu za kufikirika humu JF
 
Hata mm ningekuwa dereva na nimetoa angalizo alafu hao magamba hawanisikilizi ingeweza kutokea ajali: Yale manyimbo yao yanaboa sana unakuwa ukiendesha huku una hasira so mimi dereva nammsamehe na namtaka hakimu amwachie huru!
 
DEREVA AINGIZA BUS MTARONI KISA NYIMBO ZA CCM ZINAMKERA



4.jpg
Basi lililokuwa limewabeba wanachama wa CCM ,linavyoonekana baada ya ajali hiyo.
10.jpg
Katibu wa NEC,akimfariji mmoja wa majeruhi waliokuwa kwenye bus ambalo ajali yake imesababishwa makusudi na dereva ambaye aliwaambia yeye Chadema na asingependa kusikia nyimbo za CCM.
Chanzo:hakingowiblog

 
Tunataka ushahidi, isije kuwa ni propaganda za kisiasa kufanya ajali ya kawaida ichukue sura ya kisiasa.
 
Hivi kwa nini dereva wa mkulu asipitilize gari pale ocean road, tukaambiwa mkulu kaibukia mkondo wa nungwi!!!??? Nauliza tu! Maderava kama hawa wanahitajika sana, haswa kipindi hiki cha mabadiliko!


HAHAHAAAAAAA cacico UMECHOKA NA KAMA WATANZANIA WENGI WALIIVYOCHOKA
ALIKOTUFIKISHA JK HAMNA ALIYETARAJIA KUFIKA
 
Get well soon MAGAMBAZ! Mwendo kasi unaua! chama kinawalipia matibabu au imekula wenu?
 
Hivi kwa nini dereva wa mkulu asipitilize gari pale ocean road, tukaambiwa mkulu kaibukia mkondo wa nungwi!!!??? Nauliza tu! Maderava kama hawa wanahitajika sana, haswa kipindi hiki cha mabadiliko!

Kwi kwi kwi kwi! Hahaaaaa haaa! Duh unatuvunja mbavu. kweli! Lakini tusifike huko, tupingane kistaarab mkuu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom