Depreciation of tanzania shilling, are policy makers still asleep?

Kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania kwa kiasi kumesababishwa na hali ya soko la fedha za kigeni duniani kote lakini na yafuatayo pia yanachangia sana:
  • Kushuka kwa ujazo wa bidhaa zinazouzwa nje.
  • Kuongezeka kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ambazo si za muhimu.
  • Kutopata fedha zilizotarajiwa kutoka kwa Wahisani.
  • BOT kushindwa kuelewa kiasi cha fedha za Kigeni katika mzunguko ('volume') hivyo kushindwa kujua ukubwa wa tatizo.
  • Fedha chafu zinazosafishwa kwa kununua dola.
  • Kuongezeka kwa matumizi ya dola nchini ('dollarization').
  • BOT kuigiliwa na Siasa katika utendaji.

Suluhisho la muda mfupi:
  • Kufunga maduka ya kubadilisha fedha za kigeni au
  • Kuweka dawati la BOT katika kila duka la hela za kigeni ('Bureau de change') na katika Mabenki,Mahoteli makubwa ya kigeni n.k ili kufanya udhibiti.
  • Kupiga marufuku biashara zinazotumia dola au fedha za kigeni kama urari wa bei.
  • Kudhibiti utoroshaji wa fedha za kigeni kupitia mipaka ya nchi na viwanja vya ndege.
  • Kuzuia mahoteli ya kitalii kubadili fedha za kigeni kinyemela.
  • Kupiga marufuku uuzaji wa chenji za sarafu za Kitanzania.


Suluhisho la Muda mrefu.

  • Kuanza kutumia mashine za ATM katika ubadilishaji wa fedha za kigeni.
  • Kuzuia Taasisi na Mamlaka za Serikali kutumia dola katika huduma inazotoa( TFDA n.k).
  • Kuongeza uzalishaji wa kilimo na Viwandani kwa soko la nje.
  • Kutoa 'incentives' kwa viwanda vya nguo ili viweze kuzalisha.
  • Kuangalia namna wafanyabiashara wataenda kununua mali toka nje bila kuchukua dola au fedha za kigeni hapa nchini mfano wanaoenda Uchina n.k.
  • Kuweka utaratibu wa Makampuni makubwa ya Madini, Mafuta n.k. kuweka dhamana ya hela za Kigeni katika Mabenki yetu.
  • Kuimarisha kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu 'Financial Intelligence Unit (FIU)' katika wizara ya Fedha.
  • Kuifanyia mabadiliko makubwa ya Kimfumo na Kirasilimali watu BOT.
  • Kudhibiti biashara ya 'Real Estate' na makampuni yanayotumia dola katika kukodi nyumba na Ofisi na serikali kupitia TRA kutopata mapato yoyote.

Tanzania kama nchi ikiyafanyia kazi baadhi ya haya huenda tukawa katika sehemu nzuri zaidi..
 
Back
Top Bottom