Deos Khamis Hubert Mndeme ateuliwa kuwa Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania

Status
Not open for further replies.

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,230
13,414
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UTEUZI WA POSTA MASTA MKUU WA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Bwana Deos Khamis Hubert Mndeme kuwa Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania.

Kulingana na taarifa iliyotolewa leo, Jumatano, Septemba 26, 2012 mjini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peter Ilomo, kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inasema kuwa uteuzi huu umeanza tarehe 21 Septemba, 2012.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
26 Septemba, 2012

Hicho ki press release mbona hakina nyama?

Na kabla ya uteuzi huu huyo jamaa alikuwa anafanya kazi wapi?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Hii ni aina gani ya Press Release? Yaani hakuna hata a short CV ya mteuliwa? Jamani hebu tujifunze uandishi wa Press release, what? who?when?w. how? etc.That is katika uandishi wako ukiweza kuweka 5ws? basi angalau tutaelewa. I real question uandishi wa hiyo kurugenzi???
 
Shirika la posta TZ linahitaji 'damu mpya', vinginevo litaishia kutoa huduma vijijini tu .. sasa tusubiri, sijui huyu jamaa ana nini kipya?
 
Mbona ni mwaka huu ama mwaka jana aliteua posta masta kwani ameshindwa kazi au amestaafu
 
Nime google sijaone kitu substantial sana kwa huyu jamaa zaidi ya kuwa amemaliza LLB Open enrolled 2006 na kumaliza 2011.
 
Ni kweli ingepatikana CV yake ili hata sisi ambao hatumjui, tumjue kutokana na CV yake.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UTEUZI WA POSTA MASTA MKUU WA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Bwana Deos Khamis Hubert Mndeme kuwa Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania.

Kulingana na taarifa iliyotolewa leo, Jumatano, Septemba 26, 2012 mjini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peter Ilomo, kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inasema kuwa uteuzi huu umeanza tarehe 21 Septemba, 2012.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
26 Septemba, 2012

Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu wana matatizo, sijui walipataje kazi? Angalia hapo kwenye red. Wameandika kama 'third party'! Hili ni kosa. Kurugenzi ya mawasiliano, katibu mkuu Ikulu, Kaimu wa katibu mkuu ikulu, rais = wote hawa ni kitu kimoja kwa maana ya IKULU.

Kurugenzi wakiandaa press statement wanatakiwa wakumbuke wanatoa kama Ikulu (one office). Huwezi kuandika 'Kulingana na taarifa iliyotolewa leo, ... na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi (Ikulu) Bw. Peter Ilomo, kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, (Ikulu)!!!

Gazeti au chombo kingine nje ya 'Ikulu' ndio wangeweza kutumia huo uandhishi wa third party. Lakini kama ni Ikulu, walitakiwa waende straight to the point kwamba rais kafanya nini.

Ukiangalia karibu statements zote kuhusu teuzi toka hii Kuregenzi zinatumia huo mtindo wa kuandika kama wao ni chombo tofauti na Ikulu! Sahihisheni hili.
 
ikulu kumejaa wakaanga pweza vizazizabina rweyemamu na yule dada kibanga, hovyo kabisa
 
Shirika la posta TZ linahitaji 'damu mpya', vinginevo litaishia kutoa huduma vijijini tu .. sasa tusubiri, sijui huyu jamaa ana nini kipya?

Na watu watakaoangalia mambo differently...by engaging their minds. Vinginevyo ni shirika muflisi kama mengine maana sijui linafanya biashara gani.
 
hilo shirika bado lipo?? na linashugulikia nn siku hizi??

lipo na kazi zao ni kuuza vocha,luku,kutoa photocopy,kulipa mafao wastaafu, huduma ya e mail, kudai ada za masanduku,eastern union service, kugawa vipeperushi ktk mabox.
 
Hicho ki press release mbona hakina nyama?

Na kabla ya uteuzi huu huyo jamaa alikuwa anafanya kazi wapi?

Halafu imetolewa na kaimu katibu mkuu kiongozi Ilomo badala ya Ombeni Sefue ; kwa kuogopa kuwa watu watasema kuwa Sefue kamsaidia Mpare mwenzie kupata ulaji!!
 
Mkuu huyo alikuwepo
kwenye nafasi hiyo tangu 2009 madai anakaimu, hakuwa Benki ya Posta
labda alikuwa mjumbe wa bodi ktk benki ya Posta lakini nakumbuka alikuwa
kitengo cha Masoko ktk shirika la Posta.

kakaimu miaka yote hiyo?
 
Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu haina matatizo kihivyo... Mmesahau ya kuwa Mkulu huwa anafanya uteuzi wa vihiyo mfano wa jaji asiye na shahada ya kwanza ya sheria nk. sasa huyo wa posta kama yupo kundi hilo la wateule unataka Kurugenzi ya Habari wapate wapi CV.. Inawezekana hata kwenye faili hipo,, ni juu kwajuu.. Twende taratibu tutafika 2015
 
nashukuru kwa kuliona hilo, mara nyingi najiuliza sana juu ya uandishi w taarifa za ikulu

Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu wana matatizo, sijui walipataje kazi? Angalia hapo kwenye red. Wameandika kama 'third party'! Hili ni kosa. Kurugenzi ya mawasiliano, katibu mkuu Ikulu, Kaimu wa katibu mkuu ikulu, rais = wote hawa ni kitu kimoja kwa maana ya IKULU.

Kurugenzi wakiandaa press statement wanatakiwa wakumbuke wanatoa kama Ikulu (one office). Huwezi kuandika 'Kulingana na taarifa iliyotolewa leo, ... na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi (Ikulu) Bw. Peter Ilomo, kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, (Ikulu)!!!

Gazeti au chombo kingine nje ya 'Ikulu' ndio wangeweza kutumia huo uandhishi wa third party. Lakini kama ni Ikulu, walitakiwa waende straight to the point kwamba rais kafanya nini.

Ukiangalia karibu statements zote kuhusu teuzi toka hii Kuregenzi zinatumia huo mtindo wa kuandika kama wao ni chombo tofauti na Ikulu! Sahihisheni hili.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Na watu watakaoangalia mambo differently...by engaging their minds. Vinginevyo ni shirika muflisi kama mengine maana sijui linafanya biashara gani.

Maendeleo ya teknolojia yanawa-challenge sana posta. Siku hizi wanauza hadi vocha
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom