Deo Fulikunjombe aomba mwongozo kukomesha tabia ya kufuja muda

Kwa Bw. Ndugai kudai bunge lisionyeshwe Live alikuwa ana moja yake kichwani, na mojawapo ni kama hilo. Hata kama wakiwanyima watanzania haki ya kuona shughuli za kibunge kupitia Luninga live, kuna wabunge wengine wazalendo kama Deo Fikulunjombe watahitaji uwajibikaji wa bunge bila kuangalia itikadi za vyama.
 
Wana Jf sasa ni dhahiri Deo Fulikunjombe anaingia rasmi kwenye vitabu vya kihistoria, kwa kuwa natumia simu ngoja niwe short and clear.

Ni hivi, kumekuwa na tabia ya Mawaziri kupewa dakika 40 kujibu hoja za Wabunge, lakini cha kustaajabisha waziri anatumia dakika 20 kutaja majina ya wabunge waliochangia bajeti badala ya kujibu hoja.

Sasa Deo ameomba muongozo wa Spika kama jambo hili ni sahihi au kiti kitamke kulikomesha mara moja.

Speaker atatowa mwongozo baadaye kabla ya kusitisha shughuli za Bunge za asubuhi.

My Take: Wanaodhani sisi hasa mimi Matola nina ugomvi na CCM wanajidanganya, nahitaji kuwa na mbunge wa aina hii bila kujali chama chake, hata kama leo Deo Filikunjombe akigombea jimboni kwangu kwa tiketi ya CCM nitampigia kura yangu bila tabu yoyote. Mimi msimamo wangu huwa nachaguwa mtu na siyo chama.

Historia ipi sasa, na hilo liliongelewa wakati wa Sitta na alisema wazi, muache kutowa towa salaam na kuitana majina mnapoteza muda, na aliahidi kuwa litatungiwa sheria, naona Filikunjombe kakumbushia tu.
 
Historia ipi sasa, na hilo liliongelewa wakati wa Sitta na alisema wazi, muache kutowa towa salaam na kuitana majina mnapoteza muda, na aliahidi kuwa litatungiwa sheria, naona Filikunjombe kakumbushia tu.
Kazi unayo rafiki yangu, hiyo system @ work yako labda ni system ya maji taka maana zote ni system.
 
Kule tupo na mkuu Ritz anafunguka huwezi amini kama ni gamba!

Ritz na Rejao wapo kwenye mwezi mtukufu na funga yao inapokelewa na ALLAH bila matatizo yoyote ndio maana wamejitenga na unafki na upumbavu, labda baada ya Ramadhani ndio wanaweza kuzifungia akili zao kabatini tena. Hawa uusiwafananishe na huyu anayeshinda njaa huku akiamini amefunga zomba.
 
Last edited by a moderator:
Ritz na Rejao wapo kwenye mwezi mtukufu na funga yao inapokelewa na ALLAH bila matatizo yoyote ndio maana wamejitenga na unafki na upumbavu, labda baada ya Ramadhani ndio wanaweza kuzifungia akili zao kabatini tena. Hawa uusiwafananishe na huyu anayeshinda njaa huku akiamini amefunga zomba.

Naona umekuwa msaidizi wa Mungu. Kumbuka kuwa ibada zote ni zetu, moja tu ni ya Mungu nayo ni saumu.

Kuingilia kazi ya Mwenyeezi Mungu ni ushirikina wa hali ya juu, wa kushirikisha binaadamu kuwa mungu naona haujakutosha sasa unarukia wa kuamuwa nani kafunga nani hajafunga. Unaskitisha sana jinsi unavyoendelea kupotea.
 
Wakuu kama mko makini swala hili la kupoteza muda hata mh.Wenje aliwahi kuomba muongozo wa spika kuhusu muda unaopotea kutambulisha wageni lakini nakumbuka naibu spika hakutilia manani.

Nafikiri wapinzani hasa chadema waanze kwa kuonyesha mfano kuacha kutaja majina ya wabunge waliohusika ktk kuandaaa maoni ya kambi rasmi ya upinzani kwa kila bajeti ya wizara na pia waache kutaja majina ya wake ama waumwe zao na wanafamilia wao.Hili tatizo nimegundua liko pande zote.

Mimi binafsi hili jambo linanikera sana.Kuna umuhimu gani wa kutaja majina badala ya kusikia hoja.Hivi kusikia jina la mbunge kuwa amechangia hoja fulani lakini kama hukupata nafasi ya kusikia alichochangia itakusaidia nini au utampima tu kwa kusika kuwa amechangia?

Nani asiyejua kuwa wengine michango yao ni mipasho na matusi.Kuna haja gani ya waziri kutaja jina la mbunge alietoa mipasho au matusi wakati wa kuhitimisha hoja yake?
 
Kwa mfano

Wizara ya Ulinzi:

UTANGULIZI
1. Mheshimiwa Spika, baada ya Bunge lako Tukufu kupokea taarifa iliyowasilishwa..

2. Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu,
aliyenijalia afya njema na kuniwezesha kuwasilisha hotuba yangu ya bajeti kwa
mwaka 2012/2013. Pili namshukuru kwa dhati Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuniteua kuwa
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Nawathibitishia Waheshimiwa Wabunge
wenzangu na wananchi wote wa Tanzania kwamba nitatekeleza majukumu niliyokabidhiwa
kwa umakini na uaminifu mkubwa.

3. Mheshimiwa Spika, tatu napenda kutumia fursa hii kuwapongeza Mawaziri na Manaibu
Mawaziri walioteuliwa kushika nyadhifa hizi hivi karibuni.

Vile vile nampongeza Mhe. James Mbatia (Mb.) kwa kuteuliwa na Mhe. Rais kuwa Mbunge.
Nampongeza pia Mhe. Mussa Azan Zungu (Mb.) kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge.
Vile vile napenda kuwapongeza Watanzania waliochaguliwa na Bunge letu Tukufu kuwa Wabunge
wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

4. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2011/2012
Wabunge wenzetu watatu waliiaga dunia. Wabunge hao ni Marehemu Jeremia Sumari,
Marehemu Mussa Silima na Marehemu Regia Mtema. Napenda kutoa pole za dhati kwako
Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge, ndugu, marafiki na Watanzania wote kwa ujumla
kwa msiba huo mkubwa uliotupata. Namuomba Mwenyezi Mungu azilaze roho zao Peponi. Amin.

5. Mheshimiwa Spika, halikadhalika, napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Kamati ya Bunge
ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Edward Lowassa
,
Mbunge wa Monduli kwa kutupa ushauri na mapendekezo mazuri sana wakati wakichambua
mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yangu. Kamati hii imekuwa
ikiishauri vyema Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kuhusu njia mbalimbali za
kuimarisha utendaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Jeshi la Kujenga Taifa ili liweze
kutekeleza majukumu yake ya Ulinzi wa nchi yetu.

6. Mheshimiwa Spika, kabla sijatoa maelezo yangu kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2012/2013
napenda kuungana na Waheshimiwa Wabunge kuwapongeza Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda (Mb),
Waziri Mkuu, Waziri wa Fedha, Mhe. Dk. William Mgimwa (Mb), na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu),
Mheshimiwa Steven Wasira (Mb) kwa hotuba zao ambazo zimetoa mwelekeo katika masuala ya Mipango, Uchumi,
Mapato na matumizi ya Serikali kwa kipindi cha mwaka 2012/2013.
===============================
?????

mkuu umemaliza kila kitu. Wapuuzi sana hawa
 
Nadhani umefanya tathmini kinyume. Muda wa kutaja majina ni muda wa 'kikao' cha bunge hata kama hauhesabiwi lakini bado unapunguza muda wa bunge. Mawaziri wanashindwa kujibu hoja nyingi sana za wabunge kwa sababu muda wa bunge 'hautoshi'. Pitia hansard utaona wabunge wengi wanakosa hata muda wa kuchangia kwa sababu 'muda hautoshi' (maneno ya spika). Lakini wakati huo huo wanatumia hata huo muda mchache kushukuru wake zao, kutaja majina ya wabunge, na kutambulisha wageni wao!

Bunge la Tanzania ni kichefuchefu. Uchaguzi mkuu ulifanyika mwaka 2010, lakini leo hii 2012 mbunge anasimama na kushukuru wapiga kura wake kwa kumchagua! Hivi kwenye campaign alisema ataenda bungeni kuwashukuru?
Ungesoma post ya muanzisha thread ungenielewa nilichokisema
 
Matola nakuunga mkono.Tunachagua watu sahihi hatuchagui chama. Hata mimi sichagui fisadi just because yuko chadema. Halafu nawashauri wamwige Tundu Lissu. Huwa hana muda wa kumpongeza mke wake wala aliyemteua. He is very smart.
 
teh teh teh

Kwanza namshukuru mke wangu ameninunulia hii shati nimevaa hapa, pia namshukuru binti yetu wa pekee Sandra aliyekuja all the way kutoka Afrika kusini ili aje kushuhudia nikisoma bajeti ( Makofi kwaa kwaa), Namshukuru dereva wangu aliyenileta ambaye alinipeleka kula supu asubuhi ya leo (Kwa kwaa). Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipomshukuru HOuse girl wetu anayeitwa Tatu ambaye hunipigia kiwi viatu vyangu na kunipigia pasi (Kwaa kwaa), Namshukuru pia Mheshimiwa rais ambaye alinitumia salaam za bethidei (Kwaa kwaa).

Napenda kumpongeza mheshimiwa Zitto Kabwe kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya mashirika ya umma (KWa kwaa)

Akishamaliza pongezi 80% ya muda , muda unaobakia anaongea kwa ufupi anaenda kukaa jambo la kusikitisha ni kwamba na Chadema wamerithi hii tabia.
 
Matola nakuunga mkono.Tunachagua watu sahihi hatuchagui chama. Hata mimi sichagui fisadi just because yuko chadema. Halafu nawashauri wamwige Tundu Lissu. Huwa hana muda wa kumpongeza mke wake wala aliyemteua. He is very smart.
Kiongozi hizi tabia za kipumbavu ndio zimerithisha ujinga mpaka Wananchi nao wanaona utamu kwenda Bungeni watambilishwe ili waonekane kwenye Tv, ujinga mtupu.

Bunge gani hili la kijinga ambalo kila siku linajaa wageni wanaozidi hata idadi ya Wabunge? Nilitegemea Wanafunzi ndio liwe kundi kubwa linalokwenda kujifunza na siyo jitu kubwa zima kisa Mbunge anawagharamia wanakwenda kujazana tu pale Dodoma, Stupidy citizen.
 
Kiongozi hizi tabia za kipumbavu ndio zimerithisha ujinga mpaka Wananchi nao wanaona utamu kwenda Bungeni watambilishwe ili waonekane kwenye Tv, ujinga mtupu.

Bunge gani hili la kijinga ambalo kila siku linajaa wageni wanaozidi hata idadi ya Wabunge? Nilitegemea Wanafunzi ndio liwe kundi kubwa linalokwenda kujifunza na siyo jitu kubwa zima kisa Mbunge anawagharamia wanakwenda kujazana tu pale Dodoma, Stupidy citizen.

Muda umefika kwa mnadhimu mkuu wa upinzani Tundu Lissu, kuwashawishi chadema ili msimamo wake uwe ndio msimamo wa Chadema wote ili tutofautishe Chadema na ccm. Wabunge wetu hawapaswi kuiga upuuzi huu wa ccm.
 
Back
Top Bottom