Deni la Taifa: Kutoka trilioni 10.5 hadi trilioni 14.4 kwa mwaka?

Hilo ni deni la nje, bado la ndani. Yaani alichoongea Mhongo eti tushawishike kuwa deni ni kubwa kwa sababu ya nishati. Hilo deni ni kubwa kwa kuwa hata miradi ya barabara, na miradi mingine isiyokuwa na uharaka imefanywa kwa fedha hizo za nje. Mwishoni mwa muhula jamaa atajigamba ameleta maendeleo, kumbe amekopa fedha za watoto na wajukuu zetu. Hii no dhambi kubwa. Ben alifanya kazi kubwa ya kukusanya kodi, kujenga barabara zetu, na kulipa madeni. Huyu jamaa wa sasa anasafiria kodi zetu, anakopa mabenki ya ndani kulipa mishahara ya watumishi anakopa nje ajenge barabara na miradi mingine. Kweli tunahitaji kiongozi mwenye maono.
 
sultani yuko bize akipanga safari ya kwenda kumpa pole obama kwa yale mauaji ya wanafunzi....
Hivi Sultani pale magogoni anafanya nini?,kazi kuwaza safari na kwenda kupumzika serengeti tu!
 
Njoja na mie mwaka mpya nikatulize kichwa Kaishozi kama wanavofanya wakubwa maana hii nayo inachanganya
 
Deni la taifa limefikia zaidi ya Sh. Trilioni 20 mwishoni mwa mwaka huu, lakini Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa amesema hakuna sababu ya kupaniki kwa kuwa sehumu kubwa ya deni hilo limewekezwa kwenye miradi ya nishati na maji.

Dkt. Mgimwa amesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja ulioyopita, Tanzania ilipata mkopo wa karibu sh. trilioni moja kutoka China kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar Es Salaam.

Amesema kuwa mradi huo ukikamilika utazalisha nishati zaidi na kwa gharama nafuu. Mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 18 ijayo.

Pia amesema Tanzania imepokea dola za Kimarekani 178.2 kwa ajili ya mradi wa maji Ruvu, kwa hiyo hakuna haja kuogopa kuongezeka kwa deni la taifa.

It's alarming....!

Kama hatutaweka pressure kuzuia ukopaji holela huku wakijua kwamba 2015 kutakua na serikali nyingine itakuja kutuumiza sote.We must borrow prudently.

Sasa hapa Domestic Debt ni kiasi gani na external ni kiasi gani.ni lazima pia tufanye analysis ya kiasi kilichokopwa kutoka commercial banks au international Agencies na terms zake

Hata Nigeria kipindi cha Obasanjo(ingawa namuheshimu sana) walikopa kwa ajili ya investment katika Energy sector lakini fedha nyingi ziliishia mifukoni mwa wanasiasa

The question we should be asking is what meaningful project did they use the debt incurred on?We know so far that In NIgeria forinstance, the 16billion Naira that was main for power generation project went into the pockets of obasanjo and his criminal cohorts.Tanzania should learn

And who is liable for all this debt - TANZANIANS?

Lets look forward to high taxation when the time to repay comes.

We all know there will be nothing tangible for these huge debts we incur - Apart from politicians bank accounts!

The Government (which frequently changes/yes suppose to) is racking up these debts at the expense of the average Tanzanian.

Sasa tunaongeza kasi ya kuipeleka nchi mnadani.Tanzanians are secretly being sold out to the West or recently to the Far East
 
Sasa deni letu ni shilling trillion 20 na zaidi, je ni haki kuwapa watanzania hili deni wakati sote twajuwa pesa karibia nyingi za misaada/madeni zinalimbikizwa na JK na viongozi wake kwa manufaa yao wenyewe? Miradi gani isiyo na faida kwa wananchi? Maji mpaka leo hakuna solution yeyote, na umeme ndiyo kabisaa. Kwa nini hii nchi inaendeshwa kipuuzi hivi? Kwa kweli JK is a useless leader pamoja na viongozi wake wote ukiondoa Mwakyembe na Magufuli.
 

Zitto, Lipumba wawaka
• Wamuonya Waziri Mgimwa kuacha hadaa

na Josephat Isango
Tanzania Daima


SIKU moja baada ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Wiliam Mgimwa, kuwataka wananchi wasiwe na wasiwasi licha ya deni la taifa kuzidi kuongezeka, Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe na Profesa Ibrahim Lipumba, wamesema kauli hiyo inatia mashaka.

Waziri Mgimwa juzi alikaririwa akiwaasa Watanzania kuwa pamoja na ukuaji wa deni hilo linalofikia sh trilioni 20 kwa sasa, wasiwe na wasiwasi kwani serikali imejikita katika kuboresha huduma za maji na umeme wa gesi kuanzia Mtwara kuja Dar es Salaam.
Hata hivyo wakati Mgimwa akieleza hayo, wataalamu wa uchumi wamehofia kasi ya deni hilo kuzidi kukua.

Akizungumza na gazeti hilo jana kwa njia ya simu, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), alisema kuwa Watanznia wanapaswa kuwa na wasiwasi na deni hilo.

Zitto alirejea kauli yake aliyoitoa bungeni na kuitaka serikali ifanye ukaguzi maalumu kubaini uhalali wa deni hilo.

Alisema kuwa ukaguzi ukifanyika utawezesha kujulikana kama miradi iliyotekelezwa imefanyika kama inavyotakiwa au kuna mazingira yenye utata.

Zitto ambaye alishangazwa na kauli ya Mgimwa, alisisitiza kwamba wananchi wana haja ya kuwa na wasiwasi wala wasidanganywe na kauli hiyo.

Alifafanua kuwa mwaka 2007 baada ya msamaha, deni hilo lilifikia kiwango cha dola za Marekani bilioni 3, lakini wakati huu wa kuelekea mwishoni mwa mwaka huu, limefikia dola za Marekani bilioni 14 sawa na ukuaji wa asilimia 400.

"Waziri wa Fedha anaposema kuwa wamewekeza katika sekta ya gesi na maji, hili suala si kweli, kwani bomba la gesi toka Mtwara hadi Dar es Salaam serikali imewekeza si zaidi ya dola bilioni moja," alisema.

Alisema uwekezaji huo hauna tija kwani baada ya miaka mitano mradi wa kusafirisha gesi toka Mtwara hadi Dar es Salaam utakuwa hauna maana," alisema.

Zitto aliongeza kuwa ni kwa utaratibu huo wa kukuza deni la taifa ndio hujitokeza watu wachache wakajinufaisha kwa kuiba kwa kutumia deni hilo, na kwamba ndiyo maana mwaka huu zimetumika trilioni 1.9 kama riba tu kwa ajili ya kulipia deni hilo.
"Inasikitisha kuwa tunalipa zaidi kuliko tunavyotumia hata katika kujenga madaraja, shule au vitu vingine. Hatutaki deni liendelee kukua kwa ajili ya mikopo ya matumizi ya kawaida ya posho, kusafiri, magari ya kifahari," alisema.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), ambaye pia ni mchumi kitaaluma, Prof Lipumba, alisema kuwa miaka ya 80 deni lilikua kwa kasi hadi Tanzania ikashindwa kulipa.

Nchi ikaanza kuomba msamaha isamehewe deni, lakini msamaha wa madeni hayo ulitumika vibaya ukaleta migogoro na wizi kama wa EPA na mengine yanayofanana nayo.

Prof. Lipumba aliishauri serikali iache kukopa katika masoko ya biashara ya nje ambayo yana riba za juu bila sababu, kwani kwa kufanya vile kunaendelea kukuza deni la taifa.
Pia aliitaka serikali ipunguze kukopa, ikusanye kodi na iache kutoa misamaha mingi ya kodi na itumie vema fedha za wananchi.

Aliungana na Zitto akisema kwamba wananchi wana kila sababu ya kuwa na wasiwasi wanapoona deni la taifa linakua siku hadi siku na kuwataka wasiwe kimya kutokana na kauli ya Mgimwa.
 
Na hii inatokea kwenye nchi ambayo GDP yake ni USD 23bn!

Miradi ya umeme - I have lost count! Kila kukicha utasikia 'tuna mradi x,y,z na mara utakapo kamilika gharama za kuzalisha nishati zitakuwa bei nafuu"!!!

Hilo bomba la gesi/mkopo wa mchina: Kuna mkataba wa mgodi wa makaa ya mawe ambao Tanzania wamewapa wachina 80% na sisi tukabaki na 20% (umangungo - maoni yangu). na Makataba huu wa mgodi uligusia ujenzi wa bomba la gesi, sasa, hili deni tunaloambiwa linaingiaje kwenye deni la taifa, na mkataba wa makaa ya mawe unakuwa wapi?

hatujafikia ukubwa huo bajeti yet ni trilioni 15, 23bil usd ni sawa na zaidi ya trillioni 30 ambayo hatuna mkuu.
Mbali na hapo deni kuwa juu watanzania mjiandae mwaka 2013 mchele kununua zaidi ya sh elf 3,sukari na yenyewe hukuhuko inshort bidhaa zitapanda bei kama ambavyo marekani wanataka kukifanya sa hv.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Sijui kama kuna tatizo ela zimekopwa na zimetekeleza miradi ya maendeleo..nchi kubwa duniani zinakopa itakuwa tz ...
 
Dkt. Mgimwa hawezi kusema chochote tofauti na Kikwete. Kabla ya kusema kitu hadharani lazima ampigie simu rais na kumpa habari then rais kama ana chake anamwambia Dkt. Mgimwa adanganye kwa niaba yake. Wengi tumesoma na tunajuwa procedures za utawala wa rais na mawaziri wake. Huu ni wizi tu, wao wanakopa pesa kwa ajili ya kugawana wao kwa wao huku watanzania wakimenyeka na maisha duni. Si halali hata kidogo. Jeshi la wananchi mpoo?
 
Sijui kama kuna tatizo ela zimekopwa na zimetekeleza miradi ya maendeleo..nchi kubwa duniani zinakopa itakuwa tz ...

Uliza matatizo ya Ugiriki yametokana na nini? Na umesikia Obama anavyoangaika na fiscal cliff and government borrowing ceil au ndio kazi zenu kusoma magazeti ya kiu na ijumaa wikienda.
 
Sijui kama kuna tatizo ela zimekopwa na zimetekeleza miradi ya maendeleo..nchi kubwa duniani zinakopa itakuwa tz ...

Miradi gani hiyo? Kama ni maji na umeme...madeni yakikopwa miaka kibao iliyopita bila kuleta mafanikio yeyote hapa nchini. Zilikopwa pesa kwa ajili ya kujenga barabara mikoani hapa Tanzania lakini bado barabara zile zile ni mbovu na sasa ni miaka 6 imepita. Dar Es Salaam tu hapa barabara mbovu kibao hazijatengenezwa na viongozi wanapita humo humo kila siku wao wanaona ni sawa tu. We need a change of government hii CCM inatufila.
 
Uliza matatizo ya Ugiriki yametokana na nini? Na umesikia Obama anavyoangaika na fiscal cliff and government borrowing ceil au ndio kazi zenu kusoma magazeti ya kiu na ijumaa wikienda.

Point well taken, na usishangae ukakuta huyu aliyeandika vile ni mtangazaji wa Clouds ama Radio 1. Tatizo la kupachika watu mtandaoni ili usevu hela lina madhara yake, utakuta watangazaji wengi hapa Bongo ni wachakachuaji na ndiyo maana hata utangazaji wao unabeza sana vitu vya kijinga toka nje na kusahau kuhamasisha umma wa Tanzania. Utakuta mtu anatangaza anatumia kiingereza wakati asilimia kubwa ya wasikilizaji wake wanaongea Kiswahili, sasa huu ni ujiko ama ujinga? Tusipende kutetea ujinga bila sababu, haya madeni yatatupa majonzi siku zijazo kwani kama tujuavyo pesa karibia ya 80% zitakwenda mifukoni mwa viongozi wetu huku wauza madafu na wakulima wakiteseka.
 
Kikwete atatuachia deni kubwa mnoooo......wasaidizi wake wanasema hashauriki....anasema atakopa hadi mwisho kutumiza ahadi......watakaokuja watajiju!......lakini akumbuke alipewa nchi deni la Taifa likiwa chini Zaidi ...,na yenye Akida Nzuri ya fedha.......
Ukiacha madeni ya nje .....madeni ya ndani ni marudufu kuliko wakati Woote kwenye historia ya nchi.....mshirika ya hifadh za jamii na bima ya afya yanaidai serekali Zaidi ya Trilioni 3 tzs..

Nilikua kwenye briefing ya world bank ...na kwenye pitio la Hali ya uchumi ....wachumi wa WB walionya Tanzania kwa kuwa na deni kubwa la Taifa kuliko wakati Woote ule.....walishauri hawangekuwa na taabu Kama miradi iliyokopewa ingekuwa kwenye sekta zinazoongoza uchumi...Kama ,miundombinu na kipimo ....wasi wasi wao ni vipaumbele vyetu...na usimamizi wa miradi inyoendelea ie rushwa, na ufisadi
 
Nishati na maji ambayo ni kizungumkuti kikubwa mwaka hadi mwaka katika kila kona ya nchi yetu. Tungekuwa na mikataba halali yenye maslahi kwa Tanzania na Watanzania na makampuni toka nje ya uchimbaji wa madini nchini deni hili lingefutwa kirahisi sana, lakini kutokana na mikataba ya kifisadi litazidi kuongezeka kwa kasi ya kutisha na kuongeza ugumu wa maisha kwa Watanzania walio wengi.
yeah! umesema vema maana kila mtanzania atalipa deni hili, tajiri na masikini. masikini ataumia kwa kuwa tayari hana uwezo lakini matajiri itakuwa kawaida tu tena wao watakuwa wakinufaika na fursa zitakazokuwepo. masikini ataendelea kuwapeleka wanae shule za kayumba na zahanati dhoofu...
 
Hapa ndiyo swala la bunge kuisimamia serikali linapokuja mezani.

Kutoka Tsh 13.6 Trilioni on June 2010 mpaka Tsh 20 Trilioni on Dec 2012 ambapo kwa sasa kila Mtanzania anadaiwa karibia Tsh 487,805, wakati Kipato cha Mtanzania kimefikia tu Dola za Kimarekani 545, sawa na Shilingi 770,464 kwa mwaka.

Inanishangaza, sijui kama nchi tungekuwa wapi kwa sasa kama siyo Highly Indebted Poor Countries (HIPC) initiative and Multilateral Debt Relief Initiative (MDRI).

Ni cha kusikitisha sana pale tunapokuwa na bunge lisilofanya kazi yake kwa makini (kuisimamia serikali) badala yake linakuwa lipo tu katika kufungana magori ya kisiasa (partisan interests)

Sitegemei sana kelele kutoka kwa wabunge wa CCM kama historia inavyoonyesha lakini cha kusikitisha pia, hata wabunge wa upinzani nao wamekuwa kama wabunge wa CCM.

Hakuna hata mmoja anayeongea na kuhoji juu ya Tanzania ya miaka kumi ijayo kutokana na impact ya deni kama hili ambalo kwa baadaye litakuwa unsustainable pamoja na kwamba kwa sasa debt distress is low regardless chama au serikali gani itakuwa madarakani.


Sijasikia wanasiasa wa upande wa pili wakipiga kelele majukwaani kuhusu athari ya kuwa na hali kama hii nchini in ten or twenty years to come zaidi ya ajenda moja tu ambayo imekuwa ndiyo wimbo kila kukicha. Wanasiasa wetu ni mashujaa wa ajenda za vichocholoni ambazo zinageuka kuwa kama ni mipasho tu badala ya ajenda ambazo really matter to the public.
 
Back
Top Bottom