Umewahi kujiuliza kuhusu fedha ulizo nazo zinatoka wapi, na hizo zimetoka na mwendelezo unaofanana na huo? Bila deni hakuna fedha -- ni lazima kama nchi tukope! Deni kwa nchi yeyote halikwepeki, namna ambayo fedha zilizoleta deni zilivyotumika ladba ndio swala la kujadili.
Deni la taifa limefikia zaidi ya Sh. Trilioni 20 mwishoni mwa mwaka huu, lakini Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa amesema hakuna sababu ya kupaniki kwa kuwa sehumu kubwa ya deni hilo limewekezwa kwenye miradi ya nishati na maji.
Dkt. Mgimwa amesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja ulioyopita, Tanzania ilipata mkopo wa karibu sh. trilioni moja kutoka China kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar Es Salaam.
Amesema kuwa mradi huo ukikamilika utazalisha nishati zaidi na kwa gharama nafuu. Mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 18 ijayo.
Pia amesema Tanzania imepokea dola za Kimarekani 178.2 kwa ajili ya mradi wa maji Ruvu, kwa hiyo hakuna haja kuogopa kuongezeka kwa deni la taifa.
kutoka 5trillion hadi 20 trillion kwa kipindi kisichozidi miaka saba. je,kwa kasi hii hadi 2015, deni litakuwa shillingi ngapi?