Dena Amsi Banned!

Kwa kumbukumbu ya Baba_Enock, Pata hiki kibao cha DDC/Nico Zengekala:-

Solemba Solemba Solemba aaaaaaaa

Sitakuwa nikifika nyumbani kwako,
Aibu niliopata ni kubwa sana,
Ahadi niliyopewa ilivunjwa,
Ooo hata bila kosa.

Ulinipa ahadi tukutane kwenu,
Nikitumaini nimewahi,
Nilichopata kwako ni matusi,
Oooh oo na dharau tele,

Ungenieleza ukweli Solemba,
Kuliko kunidanganya Ooh,
Najuta kuitimiza ahadi,
Oooh ambayo si ya kweli. x 2

Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,
Ila dharau uliweka mbele Solemba.

Ulinikana mbele za watu ati hunifahamu,
Ndugu zako na marafiki walianza kutoka nje,
Waliponiona ni mimi,
Walishangaa sana mama,
Mbona hivyo Solemba x 2

Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,
Ila dharau uliweka mbele Solemba.

Nilipouliza mbona ulinitendea hivyo Solemba?,
Ulisema mimi hujipendekeza kwako tena sana,
Na kuwa hunipendi,
Nakusumbua bure mama,
Mola yupo Solemba,
Eloi yupo mamaaa

Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,
Ila dharau uliweka mbele Solemba.

Nilichomwa na jua toka asubuhi,
Mpaka saa nane Solemba,
Sababu ya kukungoja wewe,
Kumbe ulikuwa ndani,
Unachungulia dirishani,
Huna huruma Solemba,
I shall never forget you mamaa,

Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,
Ila dharau uliweka mbele Solemba.

Sikutaki tenaaa sina haja nawe,
Nimeshapata mwingine anayenipenda kwa roho moja,
Tafuta bwana mwingine utakaeyembabaisha kama mimi,
Nimeshituka Solemba,

Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,
Ila dharau uliweka mbele Solemba.
Lala lala lala lalalaaaaa
Nimeshapata mwingine anayenipenda kwa roho moja,
Tafuta bwana mwingine utakaeyembabaisha kama mimi,
Nimeshituka Solemba,
Lolo lolo lolooo mamaa

Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,
Ila dharau uliweka mbele Solemba.
 
Duh.......R.I.P Dena Amsi.

Maandishi yako bado yanaishi japo hauko nasi tena.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom