Demokrasia na Maendeleo ndani ya CHADEMA

Ikiwa ni mwaka wa pili sasa baada ya Slaa kushindwa kuingia Ikulu katika uchaguzi mkuu uliopita, mbinu mpya aliyokuja nayo ni kutoa matamko yanayowatia hofu wananchi juu ya hali ya usalama wa maisha yao na mali zao...hawezi kutoa tamko kuwambia Watanzania jinsi walivyojipanga kutengeneza ajira kwa vijana na kuonyesha njia jinsi watakavyojenga uchumi bora.
 
Kujadili ujinga wa huyu bwana ni kupoteza muda!

JF kuna members zaidi 70.000 na wageni wengi tu wanapita humu JF kwa hiyo wewe unaweza kuondoka tu kwenye hii thread...JF sio mali ya Chadema ni jukwaa huru.
 
JF kuna members zaidi 70.000 na wageni wengi tu wanapita humu JF kwa hiyo wewe unaweza kuondoka tu kwenye hii thread...JF sio mali ya Chadema ni jukwaa huru.
Naamu hata ungetoa mapovu mekundu kama damu siondoki hapa, ila fahamu kuwa huna hoja ya maana uliyoiweka hapa kwa ajili ya mjadala wenye afya. Narudia tena, unatupotezea muda na huu ujinga wako!
 
Siwezi kuwashangaa wanaouliza sera za chadema maana hiyo yote ni kwa sababu hawafuatilii wao wanataka kupata kupitia mtu wa3 ambaye ameshaichakachua hiyo taarifa,nyie mnaouliza sera za chadema je mlishawahi kuudhuria mikutano au mmnasubiri taarifa za udaku?je mlishasoma malenga ya chadema?kama hujui uliza ili uelekezwe
 
Sasa mkuu hukuelewa nn kile ambacho CDM tumehaidi kwa wananchi?
Be a guy.

Tunaona kupitia vyombo vya habari mikutano ya Chadema akisimama Mbowe anasema hakuna kulala mpaka kieleweke, akisimama Slaa nae utasikia nchi imefilisika, akisimama Lema nae utasikia Mapinduzi yanaendelea wao wana pesa sie tuna mungu..hakuna kiongozi ambaye ataelezea mipango gani ya maendeleo watawafanyia Watanzania
 
zile fly-overs vipi mkuu?
 
Wanabodi.

Pamoja na CHADEMA kufanya ziara katika baadhi ya mikoa ya Tanzania na kutangaza kauli mbiu ya M4C Watanzania wanahoji kwa nini CHADEMA hawasemi wana mipango gani yenye tija kwa taifa letu na watawakomboa vipi kama wanavyojinadi kuwa wao ni wakombozi?
Moja ya kauli ya viongozi wa CHADEMA ni ile hakuna kulala mpaka kieleweke pamoja na ile tunataka kuwakomboa Watanzania, hawaelezi mambo yanayohusu maendeleo ya taifa lao.

Watanzania wanataka CHADEMA wangekuwa wanawaeleza Watanzania ni kipi watafanya wao ambacho CCM kimeshidwa kuwafanyia, waseme ni barabara zipi ambazo watazijenga na waeleze vyanzo Vya fedha watakazotumia kujenga barabara hizo.

Kwenye mikutano ya CHADEMA huwezi kusikia wanaelezea Watanzania kuwa watawajengea hospital au watafanyaje katika kuboresha elimu hiki ndio kipindi cha kuwafafanulia Watanzania juu ya utekelezaji wa sera yao waliyosema wakati wa kampeni 2010 kuwa CHADEMA watatoa elimu bure chekechea hadi chuo kikuu kwa fedha kutoka wapi na kwa uchumi upi wa nchi.

Wananchi wanasema wanaofika kwenye mikutano ya CHADEMA wanachokisikia kutoka kwa viongozi wa CHADEMAa kauli mbiu zao 'Mpaka kielekewe hakuna kulala' 'Ukombozi unakaribia' Wao wana pesa siye tu Mungu'

Nchi haiwezi kuongozwa mithiri ya kampuni ya biashara au familia ya watu wa damu moja.
Ni hivi Mpaka kieleweke maana yaakem, CCM itoke madarakani kwanza ndo maendeleo maana CCm si tu hawaleti maendeleo ila pia nim kikwazo cha maendeleo.

Ni kama unachotea maji kwenye ndoo iliyo toboka ili upate maji ziba ndoo kwanza then nenda mtoni kuchota maji lasivo unapoteza muda.Sasa CCm utaitoaje ni kwa kura za kuikataa, zina patikanaje? kwa kuwaelimisha wapiga kura juu ya umuhimu wa kuziba ndoo kuzuia upotevu wa maji ili wainyime CCm kura ambayo ni kizuizi cha maendeleo kwa kukumbatia mfumo wa wawekezaji matapeli na waizi wa mali za umma na usimamizi ovyo wa mali za taifa pamoja na ukosefu wa ubunifu kwa kuendekeza njia za mwaka orobaini na saba za kutatua matatizo.

Fedha watatoa wapi? Unaona? ndo maaana CCm haiwezi kuleta tija hujui pesa zinatoka wapi? CDM wanataka wakamate madaraka wasimamie vizuri na kwa uzalendo mali za taifa; madini; bahari; mito; misitu; kiliomo;watalii; uwindaji; bandari;rasilimali watu; utamaduni; na makusanyo ya kodi na kudhibiti mianya ya rushwa ili mali ya mtanzania afaidi mtanzania sio wachache. Pesa imejaa tele inachezewa tu au CAG report hukuielewa? So tuendelee kuzalisha kunenepesha wezi? no watimuliwe kwanza.Hatuhitaji kitu kingine ni mabadiliko ya mfumo tu mali Mungu katujaria nyingi ikiwemo gesi na makaa ya mawe bado hatuna umeme. M4C inalenga kuelewesha watu haya ili wafanye kitu rahis tu; kuibwaga CCm then usimamizi wa mali za umma then maendeleo. Ukiondoa ukungu wa CCM machoni utaelewa tu.
 
Wewe mtu wa ajabu sana.

Umewahi kusoma manifesto ya Chadema?
Umewahi kuwasikia viongozi wa Chadema wakizungumzia vision yao ya Tanzania? Kwa kuanza tu, uwekezaji utawalenga zaidi

Watanzania badala ya sera za Kikwete za kuwaleta wageni eti Watanzania anaowaita "watu wa pembezoni" nao watanufaika. Kwa Chadema Watanzania hawatakuwa watu wa pembezoni.

Chadema itapangua mikataba mibovu ya madini ili akina Sinclair wasiendelee kutuibia madini yetu na kuwafaidisha wachache kukiwa pamoja na familia ya Kikwete ambayo wanae wanaishi kimjinimjini.

Chadema imeshasema kuwa serikali yake itakuwa na baraza dogo la mawaziri jambo litakalopunguza matumizi yaliyokithiri katika serikali ya Kikwete. Sasa wewe unataka wakuambie watajenga barabara gani na hizo hela zitatoka wapi? Kwani Kikwete kazitoa wapi?CCM imeshindwa kuwaletea Watanzania wote maisha bora. CHADEMA itaweza kwa kupangua priorities zilizopotoka za CCM.

Mawaziri na Manaibu Mawaziri Vivuli​
OFISI/WIZARA​
WAZIRI KIVULI​
NAIBU WAZIRI KIVULI​
Ofisi ya Waziri MkuuWaziri Mkuu na TAMISEMI
Freeman Aikaeli Mbowe
Kiongozi wa Upinzani Bungeni
Silinde David Ernest
TAMISEMI
Sera, Uratibu na Bunge
Raya Ibahim Khamis
Vicent Kiboko Nyerere
Elimu
Uwekezaji na Uwezeshaji
Esther N. Matiko
Ofisi ya Rais Utawala Bora
Said Amour Arfi
Mahusiano na Uratibu
Rev. Israel Y. Natse
Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Suzan A. Lyimo
Ofisi ya Makamu wa RaisMuungano
Pauline P. Gekul
Mazingira
Grace S. Kiwelu
Wizara ya Fedha Kabwe Zuberi Zitto
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni
Christina Lissu Mughwai
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Godbless Lema

Wizara ya Katiba na Sheria Tundu Lissu
Mnadhimu Mkuu wa Upinzani
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ezekia D. Wenje

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Joseph Selasini
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Silvester M. Kasulumbayi

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Kulikoyela Kahigi
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Halima James Mdee

Wizara ya Maliasili na Utalii Rev. Peter Msigwa
Wizara ya Nishati na Madini John John Mnyika

Wizara ya Ujenzi Eng. Salvatory Machemuli
Wizara ya Uchukuzi Mhonga Saidi Ruhwanya

Wizara ya Viwanda na Biashara Lucy F. Owenya
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Christowaja Mtinda

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Mbasa Gervas
Wizara ya Kazi na Ajira Regia Mtema

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Naomi A. Kaihula
Wizara ya Habari, Vijana na Michezo Joseph O. Mbilinyi

Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mustapha Akunaay
Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Opulukwa Meshack

Wizara ya Maji Highness S. Kiwia

Hawa ni Mawaziri Kivuli huu ni mfano sasa hili Baraza ni dogo?
 
nilivyokuwa nasoma hoja yako nimekuwa makini mstar baada ya mstar nikdhani umehudhuria kwenye mkutano wowote.... nakuja tena kutahamaki unajbu mmoja wa wanajamvi kwamba unafuatilia vyombo vya habar japo pia hujaeleza ni vyombo gani pengne Tbc, uhuru, mtanzania na the like...kibaya zaidi unasema "watanzania wanauliza" shwali hapa ni wapi hao watanzania? Pengne wanaoendekeza hadith za kusadikika za udini na ukanda, pengne wanaojaza tumbo zao kwa mema ya nch huku wengne tukifa kwa utapiamlo, pengne ni wale uwezo wa kupambanua mambo umeshawapaa. Ni watanzania wapi hao unaowasemea???
 
Ni hivi Mpaka kieleweke maana yaakem, CCM itoke madarakani kwanza ndo maendeleo maana CCm si tu hawaleti maendeleo ila pia nim kikwazo cha maendeleo.

Ni kama unachotea maji kwenye ndoo iliyo toboka ili upate maji ziba ndoo kwanza then nenda mtoni kuchota maji lasivo unapoteza muda.Sasa CCm utaitoaje ni kwa kura za kuikataa, zina patikanaje? kwa kuwaelimishawapiga kura juu ya umuhimu wa kuziba ndoo kuzuia upotevu wa maji ili wainyime CCm kura ambayo ni kizuizi cha maendeleo kwa kukumbatia mfumo wa wawekezaji matapeli na waizi wa mali za umma na usimamizi ovyo wa mali za taifa pamoja na ukosefu wa ubunifu kwa kuendekeza njia za mwaka orobaini na saba za kutatua matatizo.

Fedha watatoa wapi? Unaona? ndo maaana CCm haiwezi kuleta tija hujui pesa zinatoka wapi? CDM wanataka wakamate madaraka wasimamie vizuri na kwa uzalendo mali za taifa; madini; bahari; mito; misitu; kiliomo;watalii; uwindaji; bandari;rasilimali watu; utamaduni; na makusanyo ya kodi na kudhibiti mianya ya rushwa ili mali ya mtanzania afaidi mtanzania sio wachache. Pesa imejaa tele inachezewa tu au CAG report hukuielewa? So tuendelee kuzalisha kunenepesha wezi? no watimuliwe kwanza.Hatuhitaji kitu kingine ni mabadiliko ya mfumo tu mali Mungu katujaria nyingi ikiwemo gesi na makaa ya mawe bado hatuna umeme. M4C inalenga kuelewesha watu haya ili wafanye kitu rahis tu; kuibwaga CCm then usimamizi wa mali za umma then maendeleo. Ukiondoa ukungu wa CCM machoni utaelewa tu.

Mkuu tulizana kidogo.
 
Watanzania wanataka CHADEMA wangekuwa wanawaeleza Watanzania ni kipi watafanya wao ambacho CCM kimeshidwa kuwafanyia.
Sema hivi wewe unataka siyo Watanzania Wanataka! Siyo vizuri kuwasingizia Watanzania!
 
Ritz, tulia unyolewe. Vipi mbona tunasubiri fuso huku Tanga, kwa mkutano kesho? (chadema square) Tupo 20. au v8 pia poa.
 
Mawaziri na Manaibu Mawaziri Vivuli​
OFISI/WIZARA​
WAZIRI KIVULI​
NAIBU WAZIRI KIVULI​
Ofisi ya Waziri MkuuWaziri Mkuu na TAMISEMI
Freeman Aikaeli Mbowe
Kiongozi wa Upinzani Bungeni
Silinde David Ernest
TAMISEMI
Sera, Uratibu na Bunge
Raya Ibahim Khamis
Vicent Kiboko Nyerere
Elimu
Uwekezaji na Uwezeshaji
Esther N. Matiko
Ofisi ya Rais Utawala Bora
Said Amour Arfi
Mahusiano na Uratibu
Rev. Israel Y. Natse
Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Suzan A. Lyimo
Ofisi ya Makamu wa RaisMuungano
Pauline P. Gekul
Mazingira
Grace S. Kiwelu
Wizara ya Fedha Kabwe Zuberi Zitto
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni
Christina Lissu Mughwai
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Godbless Lema

Wizara ya Katiba na Sheria Tundu Lissu
Mnadhimu Mkuu wa Upinzani
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ezekia D. Wenje

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Joseph Selasini
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Silvester M. Kasulumbayi

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Kulikoyela Kahigi
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Halima James Mdee

Wizara ya Maliasili na Utalii Rev. Peter Msigwa
Wizara ya Nishati na Madini John John Mnyika

Wizara ya Ujenzi Eng. Salvatory Machemuli
Wizara ya Uchukuzi Mhonga Saidi Ruhwanya

[TR="bg

maana yake ni kwamba kuna wizara zitachanganywa, mkuu wao wa mipasho yeye anazitenganisha ili ajue atakula rushwa vipi,kila akiteua mawaziri na wizara zinaongezwa, sasa tunataka kuziunganisha tupate wizara chache,
 
Ikiwa ni mwaka wa pili sasa baada ya Slaa kushindwa kuingia Ikulu katika uchaguzi mkuu uliopita, mbinu mpya aliyokuja nayo ni kutoa matamko yanayowatia hofu wananchi juu ya hali ya usalama wa maisha yao na mali zao...hawezi kutoa tamko kuwambia Watanzania jinsi walivyojipanga kutengeneza ajira kwa vijana na kuonyesha njia jinsi watakavyojenga uchumi bora.

Siyo kuwatia hofu wananchi bali mafisadi,bongo mgando kama we**
 
Ritz amewashika pabaya, huu ukweli ulio wazi kabisa na ndio maana mnabaki kurusha matusi. Tanzania sio gari la kufanya test drive. Jamaa wanataka wapewe nchi wakati hata mkoa wameshidwa kuuendesha.
 
Ritz amewashika pabaya, huu ukweli ulio wazi kabisa na ndio maana mnabaki kurusha matusi. Tanzania sio gari la kufanya test drive. Jamaa wanataka wapewe nchi wakati hata mkoa wameshidwa kuuendesha.

tupewe nchi na nani?

nchi ina wenyewe hii, wenyewe ni sisi watanzania, na ni sisi watanzania ndo tumeamua kufanya mabadiliko. mmetunyonya sana bana. inatosha.
 
tupewe nchi na nani?

nchi ina wenyewe hii, wenyewe ni sisi watanzania, na ni sisi watanzania ndo tumeamua kufanya mabadiliko. mmetunyonya sana bana. inatosha.
Hii nchi ya CCM na itabaki kuwa ya CCM, nyie mko kuturahisishia kupata hela za wazungu tu.
Matokeo ya uchaguzi wa 2015 yanajulikana,sasa wala usisumbuke kupanga mstari kupiga kura
 
Sikumbuki kama niliwahi kukutana au kusoma mada za mtu mvivu kufikiri kama huyu, yaani unaipinga chadema wakati hujui ina mkakati gani? Jaribu kutumia busara mkuu, huu umati wa watz wanaokihama chama chenu na kukimbilia cdm ina maana wanakwenda kwa mkumbo tu? Come on you can't be serious. Kwa kukusaidia soma hotuba mbadala ya wizara kivuli ya fedha mwaka jana ndo uelewe mpango mkakati wa chadema, kama itakuwia vigumu basi subiri hotuba mbadala ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara kivuli ya fedha itakayo wasilishwa na waziri kivuli. Hii nchi bwana!!!!!
 
Back
Top Bottom