Defining, Refining and Understanding Zitto Kabwe

Zitto - who is Zitto! Made to think by rev and all of you. Who are my friends? Ninaanzia hapo. Kila la kheri

Thanks much mkuu, ni kweli kabisa mtu hutambulika kwa kutokana na waliomzunguka!!! once we answer this question, tutakuwa tumefika japo 60% ya kukufahamau...
 
mimi nashauri angepumzika kidogo siasa!naona ujana unamsumbua mshkaji
 
Uwezi kuwa Chadema ukawa perfect! Utakuwa una matatizo tu, tena makubwa!

Na uwezi kuwa CCM ukawa perfect! Utakuwa FISADI na MNAFIKI tu. Angalia wanavyolia baada ya Edward Hosea kuwaumbua wanavyo fisadi posho na kuziita takrima!
 
- Maoni yangu ni kwamba on Zitto, mazingara ya siasa Tanzania hayaruhusu wanasiasa wa aina yake kushamiri, yuko mbele sana na wakati miaka 50 ijayo ndio anaweza kuwa kiongozi anayefaa kwa taifa letu lakini sio sasa, he is way too far ahead of the times.

- Zitto, hana tofauti kubwa sana na Mkapa, (wanatofautiana kwenye ufisadi tu) lakini otherwise, nawaona wakifanana sana, maana Mkapa alipoingia kwenye power alikuwa na nia ya kufanya kweli sio siri, lakini mazingara ya siasa yetu kitaifa ndiyo yaliyomkatisha tamaa, mwisho akakubali kufuata ya viongozi wenziwe wengi yaani ya ufisadi, ingawa simtetei na ufisadi wake ni fisadi anyways!

- Kwa kifupi, Zitto yuko mbele sana ya wakati na akijaribu tu ku-adjust ili a fit-in na mzingara ya siasa Tanzania, basi ndio mwisho wake politically sasa hivi anahitaji kufanya a very careful navigation, infact anaweza kujisaidia zaidi, iwapo atakaa pembeni na siasa kwa muda na kurudi siku za mbeleni, otherwsie he has the right attitude kiuongozi, tatizo ni time bado kufikia.

Respect.

FMEs!


Time will tell!!
 
kama mwanasiasa kijana anajitahidi sana ukizingatia hali ya siasa zetu. mapungufu ni kawaida sana, vijana wengi tupo kimaslahi binafsi mno na hatujitoi kwa ajili ya nchi na wengine, kina Zitto ni wachache walioamua kufanya kazi kwa ajili ya wengine.

AKubali kasoro na ajaribu kuzirekebisha otherwise he is doing fine.
 
Kibunango,

Kisiasa Zitto yuko juu sana zaidi ya wana sisi m wengi tu ndugu. Niambie unaweza mlinganisha na nani? Wassira? au nani?

Najua Zitto pamoja na kuwa juu ana madhaifu yake kidogo tu anayotakiwa kujilekebisha na mengi niliyaona wakati wa uchaguzi wa Chadema.

Hata hivyo namkubali kuwa ni kiongozi makini.

Huwezi mlinganisha na makanjanja wa sisi m.
 
mimi nashauri angepumzika kidogo siasa!naona ujana unamsumbua mshkaji

Kwa hiyo ni vijana wote wapumzike? au kuna mwanasiasa kijana ambaye hana kasoro?(kama ipo)?

Na akipumzika, nani unafikiri atachukua nafasi yake? jamani ufisadi si kuiba tu , hata mawazo ya kifisadi ni ya kuyaogopa sana!
 
namsifu Mr.Zitto Kabwe kwa sababu ni muwazi na angalau anajali zaidi ya hayo ni jasiri, ni viongozi wachache wa ngazi yake wanaokuja hapa JF au kwenye mitandao mingine mikubwa ya siasa kuchangia mawazo yao na kusoma mawazo ya wengine wakiwa katika majina yao halisi...bila kujali kujadiliwa kulaumiwa, kuwa defined, refined etc...

I wish wote wenye madaraka mazito ktk nchi hii wangekuwa na ujasiri kama wake...
 
Uwezi kuwa Chadema ukawa perfect! Utakuwa una matatizo tu, tena makubwa!
Kama unapokuwa kwenye Chama cha kuongozwa na Makamba kama katibu Mkuu,matatizo uliyonayo ni makubwa zaidi na mbaya zaidi huwezi kuelewa kama una matatizo hayo!
 
Namwomba Zito azingatie yafuatayo akitaka:
1. Msimamo usioyumba. Bado anapungukiwa hili na limekigharimu sana CHADEMA kwenye chaguzi za Mitaa zilizopita. Angechaguliwa yeye kuwa Mwenyekiti wa Taifa hadithi ingekuwa nyingine sasa hivi kwa siasa za Nchi hii.
2. Umimi. Anajiimarisha yeye zaidi kuliko chama chake. Hili halitamfikisha popote zaidi ya kupata UMAARUFU. Awaulize akina Mrema waliotumia staili hii walikofikia.
 
1. Msimamo usioyumba. Bado anapungukiwa hili na limekigharimu sana CHADEMA kwenye chaguzi za Mitaa zilizopita. Angechaguliwa yeye kuwa Mwenyekiti wa Taifa hadithi ingekuwa nyingine sasa hivi kwa siasa za Nchi hii.
Mkuu naomba nitofautiane na wewe hapa. Zitto ninaye mfahamu mm tangia tukiwa naye pale UDSM, hicho ulicho kisema hakimhusu au si hulka /tabia yake kabisa. Zitto anamisimamo thabiti sana kwenye mambo anayoyaamini yeye kwamba ni sahihi, huwezi kumyumbisha kwenye suala hili, na huwa hayupo tayari kubadili msimamo wake labda sir. God ashuke duniani! Mfano...Sakata la viongozi wa DARUSO....miaka hiyo -kutokana na kutokubali kwake kusurrender, ilipelekea yeye na baadhi ya wenzio kusimamishwa masomo, pili Sakata la Buzwagi...u all know what happaned, tatu....issue ya HOVYO HOVYO, kila mmoja anajua, Issue ya DOWANS....etc just to mention machache!

2. Umimi. Anajiimarisha yeye zaidi kuliko chama chake. Hili halitamfikisha popote zaidi ya kupata UMAARUFU. Awaulize akina Mrema waliotumia staili hii walikofikia
Yes, Wilcard hapa tupo pamoja......hii ni mmoja wapo ya kasoro za mheshimiwa..... he needs to do something here!
 
Uwezi kuwa Chadema ukawa perfect! Utakuwa una matatizo tu, tena makubwa!

Nani perfect dunia hii? Nitajie mtu aliye perfect, kutoka chama au dini yoyote duniani. Tujifunze mawasiliano jamani.

Kwenye kiingereza tutasingizia lugha ya kigeni, sawa.Hata kiswahili nacho?
 
Nani perfect dunia hii? Nitajie mtu aliye perfect, kutoka chama au dini yoyote duniani. Tujifunze mawasiliano jamani.

Kwenye kiingereza tutasingizia lugha ya kigeni, sawa.Hata kiswahili nacho?
Mkuu c unajua tena kipendacho roho huwezi mwelimisha huyo!
 
NL,
DOWANS, Zitto katoa misimamo miwili; kwanza alitaka TANESCO iinunue mitambo ile, pili kwenye press conference yake ya hivi karibuni akataka itaifishwe!
Buzwagi hakuna alichofanikisha pale. Mkataba umebaki uleule uloosainiwa London. Raisi alipounda ile tume ya Jaji Bomani na yeye akawemo. Wakawa wanalipwa Shs 350000/= kwa siku. Ripoti yao imefanyiwa kazi kiasi gani sijui.
 
I beg to differ gents. I do not trust the guy, yes he is charismatic, energetic and may be pro-development. Lakini alivyoiyumbisha Chadema ameonesha kuwa he is somekind of an opportunist and somekind of self centred politician.

Mtu kama huyu akipewa kiti kikubwa anaweza kuburuzwa na kuyumbishwa, au anaweza kufanya mengi ya ajabu ambayo ni unpredictable.
 
Kwamba Zitto ana msimamo dhabiti, hilo halina mjadala. Lakini mara nyingine kauli zake zimekuwa zikileta utata sana kwa wanaomsikiliza kijuu juu. Nadhani kisiasa anakosea kama kweli anataka kuaminika na watu wasioelewa. Ila Kisomi huwa-ga yuko sahihi.
 
naona kichefuchefu kuona watu wa ccm wanajitokeza hadharani na ku-argue!!!!

Hawataki kuelewa nchi hii haitapiga hatua , namkumbuka Jerry rowlings yeye aliamua kuwafungia kazi mafisadi
 
Back
Top Bottom