DED anataka kunifukuza kwenye nyumba ya umma

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Nov 7, 2012
1,976
3,122
Habari wana JF

Miezi kadhaa iliyopita nilikuja kwenu na thread "Msaada mkuu huyu wa shule " kwenye bandiko hilo nilieleza mengi juu ya mgongano uliyojitokeza kati yangu na mkuu wa shule moja ikiwa ni madai yake kuwa nitoke kwenye nyumba ya shule eti anataka akae mwalimu wa malezi, kiujumla niliona si haki nikalipeleka jambo hilo ngazi ya kata likaamuliwa kuwa nikae hadi nitakapo pata nyumba nyingine nitakayoona inafaa ama mkuu wa shule anitafutie, huku nyuma kumbe hakuridhika kaandika barua kapeleka kwa DED ikisema mimi nimekaidi maagizo yake.

Leo ghafla nashangaa ugeni kituoni, mara naitwa.... kumbe eti mkurugenzi katuma watu (afisa utumishi, tsd na afisa taaluma ) wamenieleza kuwa wametumw juu ya jambo hilo na kutaka eti niandike barua kuw nitakabidhi nyumba ndani ya siku saba......... kimsing nikasem hawawezi kunipa agizo hilo bila kunisikiliza........ nikawaeleza hali halisi ilivyo ki ukweli wamekili kuwa taarifa zimeenda kwa DED tofauti but wakaniomba niandike hiyo barua nimepiga chenga kuandika nimesem nitaandika na kupeleka kesho kwani,

(a ) hakuna barua yoyote niliyoipata inayonitaka nitoe maelezo juu ya jambo hilo na kama mimi mwalimu sistahili kuishi kwenye nyumba ya umma nijue navunja sheria ipi.

(b ) naona kuandika barua ni kujitengenezea kesi je hizo siku saba nisipopata nyumba si ntakuw nimekaidi?

(c ) sioni sababu ya kunitimua kwenye nyumba Kwan bado ni mtumishi halali.

Maswali ni mengi kuliko majibu but mwisho nimeamua kwenda kesho kwa afisa elimu nimueleze na ikibidi niende kwa mkurugenzi hapa naona ile misemo ya walimu tunaonewa nauona ukweli dhahiri. but nakaribisha michango kwani penye wengi pana mengi!

Nb. Najua kuna watakao ona jambo hili kwa namna tofauti naomba busara si matusi na kejeli.
 
Hivi kwanini mnapenda vya bure? Si uende ukapange kwani lazima ukae shuleni?
 
Katika maelezo yako hiyo nyumba unayoishi inatakiwa akae mwalimu mlezi wa wanafunzi wanaokaa bweni. Sasa kama wewe sio mwalimu mlezi na huna sababu ya kuishi karibu na shule ni busara umuachie mwenzio ambaye anahitajika kuwa karibu na shule. Jitahidi upate nyumba nyingine uendelee na maisha kuliko kuleta mgongano usio kuwa na maslahi isipokuwa kuoneshana umwamba.!!
 
Mkuu nataka nisaidiwe yafuatayo,

(a ) Je shule ya sekondari ya kutwa mwl. wa malezi hasa ni yupi?

(b) Je kuna mwl. asiyekuwa wa mlezi?

(c) Je kutoka kwenye nyumba hiyo katika mazingira hayo ni busara au ni kanuni? kama ni busara je jambo hili kufika hadi kwa mkurugenzi hiyo ni busara?
 
Mwakabanje....shule ina nyumba ngapi? Hio nyumba unayoishi uliipata au ulipewa kwenye mazingira gani? Je ni walimu wangapi ambao mnaishi kwenye nyumba za shule? na kuna mgogoro wowote ama mgongano wa kimaslahi baina yako na huyo mkuu wa shule? Kama utaweza kunijibu haya nione namna ya kukupa ushauri mkuu.
 
Asante mkuu,

(1) shule ina nyumba tatu, moja anakaa mkuu wa shule, nyingine anakaa mwl. wa kike ambaye pia amepew jukumu la malezi

(2) Mimi nilipanga before but baadye nilifanikiw kumshawishi jamaa yangu aliyekuw kapangiwa ajira mpya ili aje asaidie somo la hesabu, hapo ndo nikaombwa na mkuu huyohuyo nimpatie jamaa huyo hiyo nyumba mimi anipe ya shule.

(3) Mgongano na mkuu upo ulitokana na mimi kuomba kuacha kumsaidia majukumu ya umakamu baada ya kuona ananilazimisha kumfanikishia michezo hatari ambayo niliona inaweza kunihatarishia kazi yangu kupitia nafasi hiyo, tangu hapo ni fitna tu!
 
DR. MWAKABANJE katika utumishi kuna HAKI za mfanyakazi, lakini pia kuna UTII kwa mamlaka ya uongozi uliopo. Kiongozi anapokuja mahala na kukosa kiti huwa twamwachia kiti kwa sababu ya utii (heshima) na sio haki. Mkurugenzi wa Muhimbili alimtoa mfanyakazi aliyekuwa akiishi kwenye nyumba ya wafanyakazi (tena aliikarabati kwa pesa zake mwenyewe) japo alibisha awali lakini baadaye akatii. Unaweza ukafanya sana kazi, ukawa mwalimu mzuri, lakini usipokuwa na heshima kwa viongozi wako hata promotion hupati.
Uongozi wa shule una mamlaka ya kumweka mwalimu mpya au kubadirisha matumizi ya nyumba ya shule. Wewe unachopaswa kufanya ni kutii. Acha kiburi kama cha watu wa Kyela. Hakitakusaidia kazini. Wenzako ambao hawana nyumba mbona wanadunda. Kwanza hiyo nyumba itakudumaza.
By the way, mimi nilijua wewe ni daktari wa binadamu au PhD holder kumbe ni mwalimu wa sekondari!!! Huo udokta umeupata wapi au zilikuwa ndoto zako kuwa dokta?
 
Hahaha imenibidi nicheke kwa sababu mkuu wangu ni mtu wa kyela, pia huo udokta ni ndoto tu mkuu wala hazijafa but thanks
 
Katika taasisi kama shule, ni mkuu wa shule pekee ambaye yuko entitled kupata nyumba hilo lieleweke hivyo. Hakuna logic kwamba shule ya kutwa mwl wa malezi ni lazima apewe nyumba, kwa shule za bweni inaleta logic siyo kwa shule ya kutwa. Niliwahi fundisha shule x Njombe yule mkuu alikuwa anatoa nyumba kwa seniority, the long you have served the more you deserve, na mtu unapewa nyumba kwa barua rasmi.
 
DR. MWAKABANJE katika utumishi kuna HAKI za mfanyakazi, lakini pia kuna UTII kwa mamlaka ya uongozi uliopo. Kiongozi anapokuja mahala na kukosa kiti huwa twamwachia kiti kwa sababu ya utii (heshima) na sio haki. Mkurugenzi wa Muhimbili alimtoa mfanyakazi aliyekuwa akiishi kwenye nyumba ya wafanyakazi (tena aliikarabati kwa pesa zake mwenyewe) japo alibisha awali lakini baadaye akatii. Unaweza ukafanya sana kazi, ukawa mwalimu mzuri, lakini usipokuwa na heshima kwa viongozi wako hata promotion hupati.
Uongozi wa shule una mamlaka ya kumweka mwalimu mpya au kubadirisha matumizi ya nyumba ya shule. Wewe unachopaswa kufanya ni kutii. Acha kiburi kama cha watu wa Kyela. Hakitakusaidia kazini. Wenzako ambao hawana nyumba mbona wanadunda. Kwanza hiyo nyumba itakudumaza.
By the way, mimi nilijua wewe ni daktari wa binadamu au PhD holder kumbe ni mwalimu wa sekondari!!! Huo udokta umeupata wapi au zilikuwa ndoto zako kuwa dokta?
Kwenye hii kada "utii" huwa unatufanya tuonekane waoga
 
Kisa cha mgogoro wenu ni kitendo chako cha kukataa nafasi ya makamu mkuu wa shule. hapa naona tatizo kwa sababu barua yako ya ajira uliambiwa kufundisha na majukumu mengine utakayopewa na mkuu wako wa kazi, ukikataa majukumu maana yake hauko tayari kufanya kazi kwenye hiyo shule. Hapo mwajili wako anaweza kukuhamisha au vinginevyo aonavyo kwa vile umekiuka masharti ya mkataba. Na kama ungekuali hiyo nafasi na ukafanya kazi kwa kufuata sheria basi hujuma zozote za mkuu wako zingemshushia heshima yeye.
 
Asante kwa mchango wako but naomba nielewa kuwa sikukataa hiyo nafasi bali niliachia ili kunusuru kazi na maisha yangu kwenye uzi wa kwanza nilieleza baadhi ya sababu, ndugu mambo ni mengi sana na mengine hata hayapaswi kuandikwa.
 
Mwombe Afisa Elimu au Mkurugenzi akuhamishe
kwanini unang'ang'ania mahali ambapo pata-cost maisha yako
inaelekea hayo maeneo ya nyumba zenu unaleta matatizo wakaona bora akae mwenzako wa Malezi kwani wewewameona huendani
 
Katika maelezo yako hiyo nyumba unayoishi inatakiwa akae mwalimu mlezi wa wanafunzi wanaokaa bweni. Sasa kama wewe sio mwalimu mlezi na huna sababu ya kuishi karibu na shule ni busara umuachie mwenzio ambaye anahitajika kuwa karibu na shule. Jitahidi upate nyumba nyingine uendelee na maisha kuliko kuleta mgongano usio kuwa na maslahi isipokuwa kuoneshana umwamba.!!
Well said!!
 
Inawezekana huyo mkuu anataka kuleta kimada wako akae hapo kwa mlango wa mlezi.....komaa nao kama una uhalali wa kukaa hapo hao wapuuzi muda mwingine huwa wanatumia madaraka yao kuwakandamiza wenzao tu......
 
Back
Top Bottom