DECI yawa kilio badala ya neema

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
24
Katika pitapita yangu jijini Dar es Salaam nimekutana na gazeti la UWAZI likionyesha mama mmoja aliyepoteza maisha baada ya kufika kwenye za DECI na kukuta kufuli kubwa mithili ya Kichwa cha ng'ombe. Mama huyo ilikuwa ni siku yake ya kwenda kuvuna mapesa kutokana na fedha au mbegu alizopanda. Ghafla alidondoka na kufariki papo hapo. Hii ni habari iliyopo ndani ya gazeti hilo la uwazi. Wanajamii forum ambao mlikuwa wanachama wa iliyokuwa DECI je habari hizo ni za kweli?

Cha kushangaza ni kwamba mama huyo ambaye kwa sasa ni marehemu alitoka home asubuhi na kusema anaenda kwenye shughuli zake za kila siku. Mume hakujua kwamba mkewe ni mwanachama wa DECI. Alijua baada ya kifo kumkuta mumewe. Kuna haja ya kuwa na mawasiliano baina ya wanandoa.
 
usione watu hawachangii hapa.
wengi humu hawana mawasiliano ktk ndoa zao ndo maana kila kukicha mashtaka hayaishi humu.

pole zangu kwa familia ya marehemu
 
Aisee!!! , watanzania tunapitia mengi.. kumbe kuna watu walipoteza na maisha kabisa!!!
 
Back
Top Bottom