DECI siri nzito: Ilisajiliwa nchini na BRELA 2007

Kaitaba

JF-Expert Member
Jun 30, 2009
916
52
DECI siri nzito
• Ilisajiliwa nchini na BRELA 2007, ina trilioni 1.038


na Edward Kinabo


HATIMAYE siri imefichuka kuwa Kampuni ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI), inayojishughulisha na biashara ya kupanda na kuvuna pesa, ilianzishwa nchini mwaka 2007, baada ya kampuni yenye mfumo kama huo kufa huko nchini Kenya na kuwadhulumu maelfu ya wanaupatu wake waliokuwa wamejiunga nayo.
Vyanzo mbalimbali vya kuaminika, vimelitaarifu gazeti hili kuwa, raia mwema mmoja, jina tunalo, ndiye anayedaiwa kufichua siri ya DECI

Aidha, taarifa za kuaminika kuhusu uchunguzi uliofanywa na kitengo cha kuzuia fedha haramu cha Kurugenzi ya Makosa ya Jinai, ndani ya Jeshi la Polisi nchini, zilieleza kuwa DECI ilisajiliwa nchini na Msajili wa Makampuni (BRELA), mwaka 2007, na kupewa namba ya usajili 61334.

“Kwa mujibu wa maelezo ya wakurugenzi wa DECI Tanzania, ni kwamba kampuni hiyo ilianzishwa kwa madhumuni ya kusaidia wajasiriamali wadogo wadogo kupitia TRF (Tushikamane Revolving Fund
 
"Kwa mujibu wa maelezo ya wakurugenzi wa DECI Tanzania, ni kwamba kampuni hiyo ilianzishwa kwa madhumuni ya kusaidia wajasiriamali wadogo wadogo kupitia TRF (Tushikamane Revolving Fund
lakini nina swali moja, DECI walifafanua namna watavyorise fund kutoka mikononi mwa masikini wa tanzania na kuzizungusha ?
Je sheria inasemaje juu ya biashara ya kuzungusha pesa....?
Kisheria naamini DECI ilikua lazima ife...! lakini kwanini GVT ilichelea kuichinja ontime mpaka ikaweza kukusanya mtaji mkuubwa hivyo.?
ila tutaka tusitake DECI ilikua lazima ife kwa kifo ambacho kingewaacha wengi midomo waazi, kuliko idadi ya waliolia mwaka jana.
 
Nakumbuka miaka ya 1995 au 1996,nililiwa pesa kama shs 100k hivi kwa kampuni design ya DECI,ya kuzungusha pesa.Hata Mrema alikuwa member wakati huo!!!!Sio mimi tu,watu wengi waliliwa pesa.

Inaonyesha Watz wengi upeo wetu wa kuelewa ni mdogo sana,ndio maana tunadanganyika kila siku.
Kama kweli BRELA waliwasajili,basi kuna corruption kubwa sana,wakati wanatoa ruksa ya DECI,kila mtu alijua what will happen.Hakuna nchi yoyoyte duniani zaidi ya Tanzania kuna ujinga,upumbavu na uroho wa aina hii,hasa scandal kama za DECI.

OH MY GOD

Nafikiri serikali
 
Shida yetu kubwa ni kwamba, tunapenda kupata pesa za chapchap, ambazo hatuzitolei jasho. Tunasahau ya kuwa, "Hakuna kitu cha bure duniani."
 
Hivi mbona hakuna mtu hata mmoja aliyelalamika kuwa kadhulumiwa na DECI?,
 
Uzi wa kitambo ina maana watu hawaja samehe? Huo mpunga ushaliwa Na wenye akili kuna Jamaa alinishawishi machale yakanicheza alivuna mwanzo awamu yapili kilicho mkuta hadi leo anatembea kwenye kivuli cha deci haja wahi inuka
 
Back
Top Bottom