DECI DECI wazuiwa kukusanya mamilioni ya watz

hawa deci deci jamani vyanzo vyao vya mapato ni nini?naomba waeleze ili wateja wajue na wawe na uhakika na fedha na riba zao.

Its a Ponzi or Pyramid scheme. Inatumia pesa za wawekezaji wapya kuwalipa wawekezaji wa zamani, sooner or later kutakua hakuna wawekezaji wapya hapo ndo mambo yanapoharibika. hizi scheme zote in the end lazime zife kwa sababu lazima wawekezaji wapya wataisha na watu lazima wapoteze pesa zao.
Link:
What Is A Pyramid Scheme?
 
bado sijaelewa mwananchi anazurumiwa vipi? yaani kuna hasara gani kwa mwanachama maana naona maelezo tu kwamba DECI haifai kivipi?
 
bado sijaelewa mwananchi anazurumiwa vipi? yaani kuna hasara gani kwa mwanachama maana naona maelezo tu kwamba DECI haifai kivipi?

Soma Link hiyo liniyotoa juu hapo.
The fraud lies in the fact that it is impossible for the cycle to sustain itself, so people will lose their money somewhere down the line. Those who are most vulnerable are those towards the bottom of the pyramid, where it becomes impossible to recruit the number of people required to pay off the previous layer of recruiters. This kind of fraud is illegal in the Unites States and most countries throughout the world. It is estimated that 90% of people who get involved in a pyramid scheme will lose their money.
 
bado sijaelewa mwananchi anazurumiwa vipi? yaani kuna hasara gani kwa mwanachama maana naona maelezo tu kwamba DECI haifai kivipi?

Kuna thread nyingine inayoongelea hili. Katika thread hiyo Mwanakijiji ameeleza vizuri, lakini pia kuna michango mingi mizuri.

Nenda kwenye link hii: DECI DECI.

Cha muhimu ni MSINGI wa mchezo huu.

Unapoweka fedha Benki, Benki wanazalisha pesa hiyo kwa miradi inayofahamika, na benki wanatutangazia ripoti zao za fedha waziwazi hadharani. Benki wanaweza kukopesha watu kwa riba kubwa kuliko wanazolipa wateja wa akaunti za akiba. Lakini pia Benki wana vitega uchumi ambavyo huzalisha fedha wanazopokea toka kwa wateja. Hii ndio hulipa faida wateja. Lakini faida hiyo mara nyingi haizidi asilimia 10 kutokana na hali halisi za kibiashara.

Lakini Schemes kama za DECI, hakuna uzalishaji wowote unaofanyika kwa fedha zinazokusanywa. Wanachofanya ni kupata wanachama wapya, na fedha za wanachama wapya ndizo wewe uliyepanda zamani unavuna. Sasa mwendelezo wa mchezo huu unategemea kupata wanachama zaidi ili uendelee kulipa faida.

Lakini kadri scheme inavyopata wateja zaidi, ndio jinsi inavyoelemewa na kuwajibika kupata fedha ambayo hawa wapya watavuna. Hatima ya scheme hii ni kuelemewa na kushindwa, ikiwa inadaiwa mamilioni ya pesa na "wawekezaji" wa scheme hiyo.

Charles Ponzi alianzisha scheme hii USA mwaka 1920, ikapata watu wengi sana. Lakini baadaye alishindwa kuwalipa wapya na akakamatwa na kufunguliwa mashtaka tarehe 12/8/1920.

Hivi sasa kama unasikiliza BBC au CNN yuko Bernard Madoff ambaye alijikusanyia mabilioni ya dola kwa mfumo kama huo, na sasa mwenyewe anakiri kuwa ni wa udanganyifu. Watu wengi wamepoteza mamilioni katika mfumo huo wa Madoff ambao msingi wake ni kama wa Ponzi.

Soma hapa kwa maelezo zaidi link Ponzi
 
Nadhani wote mmesikia na kuona kwenye vyombo vya habari kwamba BERNARD MADOFF, ambaye aliishi kwa uendeshaji wa shughuli kama ya DECI, alikiri kosa mahakamani na amehukumiwa kifungo kirefu ambacho atamaliza maisha yake yote jela.

Waendeshaji wa DECI Tanzania waangalie, hatima yao yaweza kuwa hiyo.
 
Ningependa kutoa maoni yangu kuhusu swala hili. DECI wanaonekana kama ni kampuni ya uwekezaji lakini kitu kinachonitatiza au kinatatiza wengi ni wapi wanakowekeza hayo mamilioni ili wapate mamilioni? Kuna uwazi kwa hilo? Kama hakuna uwazi tunaanzia kuwashakia hapo.Kama hakuna maelezo ya wazi kuna uwezekano ikawa Pyramid scheme kwani itakuwa inategemea michango ya wanachama kulipa wanachama wengine. Kwa kuwa wanaodai ni wengi na fedha zinazodaiwa ni nyingi kuliko zinazokusanywa mwisho wasiku watu wataliwa fedha zao.
CHARLES NAZI
Mshauri wa biashara
Blogu ya Mshauri wa biashara Charles
 
Nimesoma maoni kuhusu hii, kila inavyoelezewa ndivyo inavyozidi kuleta maswali. Naomba kama kuna watu bado wana mashaka, wafanye reference kwa Benard Madoff na PONZI scheme yake. Watalia watu siku si nyingi, mark my words!!!!
 
Yap! You are talking!
 
Kuna habari kamii juu ya umri wa DECI Tz?
Maana hicho kitu nimekisikia kwa mara ya kwanza wiki iliyopita pale nilipojiwa na mtu akiniambia kuna habari njema Tz (DECI) panda kidogo vuna kingi.

Tuambieni wana umri gani tangu waanze biashara?
Na hata hivyo je, kuna baraka zozote za viongozi wa kitaifa au wazawa kwenye scheme hii? Receipt zao zinaonyesha kwama mapato wanayopata yanalipiwa kodi nchini? Makao makuu ya deci yako wapi? Tuchunguze mafanikio ya deci popote duniani kama ilishaoperate na hasara ilizoingia ukiachilia umri wake hapa kwetu tangu imeanzishwa. Tunakokwenda sasa naona hata wana JF tunaweza kutengeneza scheme yetu wenyewe tukawa kama POWER CLUB ili tuwe matapeli wa dau kubwa kimataifa. TAFAKARI!!!!!!!
 
Yap Jimba kweli tunatakiwa kufahamu makao yo makuu, lakini kwenye form zao wanadai ni wanapatikana kwenye jumba la mama Kiwia kule Mabibo lakini pia tunapaswa kuwafahamu Kiongozi wao Mkuu na wale viongozi wakuu wenye hisa kubwa pale, mie kuna mmoja nayemfahamu kidogo anaitwa Ole kama kuna mwenye taarifa zaidi ya majina ya Kiongozi wao Mkuu abandikwe hapa JF tuwadodose zaidi ili ikitokea ya Bernard Madoff tujue wa kumkamata ni nani
 
Mmmh hii investment inatisha lakini mmmh inavutia.
Wajua tumekua na njaa sana kiasi cha ikitangazwa fursa yoyote inayotamka hela basi utaona kila mtz anataka kukimbilia huko.
Mmmh hata wakina ..... wanakodolea macho huko lakini wanaogopa huko.
ITS BETTER KAMA MTU UNAENDA WEKA HELA ZAKO HUKO UJUE KUA KUNA SIKU jamaa watazimadoffai hivyo ubaki miayo aaaaaaaaaaah yaaaaaaaaaa ooooh
 
Makao makuu yao yapo Mabibo Mwisho kwenye numba ya mama Kiwia. Company registration ni 61334 iliyotolewa 25/7/2007. Wanayo barua ya BOT wanayodai inawatambua na kuwaruhusu kukusanya fedha yenye Ref. DBS/B20/100/Voll. II/6. Simu za BOT zilizoonyeshwa kwenye barua hiyo ni 2110036, 2118021 na 21398161. Hii ya mwisho inaonekana imekosewa na hizo nyingine ukipiga unajibiwa ' namba hiyo haipo'.
Nimejaribu kufuatilia BOT lakini kote nimekuwa directed sehemu mbalimbali, mara piga simu hii mara ile, hakuna aliyekiri kutoa barua hiyo.
Kwa kufuatilia kumbukumbu (REF) ya barua hiyo, nadhani DBS stands for Director of Banking Supevision. Kwa kuwa ndani ya kitengo hiki kuna Deputy director - nonbanks supervision; nadhani ofisi hiyo au kitengo hicho ndicho kimetoa barua hiyo. Wanapaswa wauleze umma kuhusu DECI. Namba za simu kutoka kwenye website ya BOT (Bank of Tanzania (BOT): Home Page : Benki Kuu ya Tanzania) zinaonyesha kuwa ni 2235528/9 na 2235552/3.
Naomba wana JF walio BOT watuhabarishe zaidi.
Nimeona pia registration yao ya TRA lakini sikujishughulisha nayo kwa kuwa wao TRA wanachojali ni kuwa unalipa kodi. Kwao source of income whether legal or illegal is irrelevant (ukisoma Income Tax act utaona wazi kuwa taxable income is icome derived from whatever source).
TUHABARISHANE
 
Back
Top Bottom