DECI DECI wazuiwa kukusanya mamilioni ya watz

NgomaNzito

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
559
26
Kuna tetesi kuwa ile Kampuni ya DECI (T) ltd imenyimwa kibali na Central Bank (BOT) cha kuanzisha Scheme nyingine inayoitwa Elimika Scheme inayohitaji mwanachama kutoa Sh milion tano upate sh. Milion 12.5 ndani ya wiki 22.
Tetesi hizi zinadai pia Deci inaweza kuingizwa kwenye adminstration na central bank very soon baada ya kuonekana mabosi wake wanafuja fedha za wanachama kwenye scheme yao ya TRF ambapo mwanachama anapaswa atoe kati ya sh laki mbili apate laki tano. Kwa mwenye taarifa zaidi amwage hapa tuwajadili kwa watz wengi wamewekeza kwenye huu mfuko......
 
Hii thread inaweza kuwa mwendelezo wa thread kama hii siku za hivi karibuni.Basically DECI is a PYRAMID SCHEME na nitashangaa kama Benki Kuu itawaruhusu wasajiliwe, maana hakuna uzalishaji mali pale ni ujanja ujanja.
Na njia rahisi kwa scheme kama hii kufa kabisa ni wanachama wote wadai fedha zao kwa mkupuo.
Wanachama wanaweza kudai fedha zao kama hivi sasa ambapo kuna tetesi za ubadhirifu na ufujaji wa pesa za wanachama.
Schemes za aina hii zimekuwepo siku nyingi na hazina mwisho mzuri-watu wanaishia kulia.
 
Kuna tetesi kuwa ile Kampuni ya DECI (T) ltd imenyimwa kibali na Central Bank (BOT) cha kuanzisha Scheme nyingine inayoitwa Elimika Scheme inayohitaji mwanachama kutoa Sh milion tano upate sh. Milion 12.5 ndani ya wiki 22.
Tetesi hizi zinadai pia Deci inaweza kuingizwa kwenye adminstration na central bank very soon baada ya kuonekana mabosi wake wanafuja fedha za wanachama kwenye scheme yao ya TRF ambapo mwanachama anapaswa atoe kati ya sh laki mbili apate laki tano. Kwa mwenye taarifa zaidi amwage hapa tuwajadili kwa watz wengi wamewekeza kwenye huu mfuko......

Mbona sijaifahamu scheme hii inaonekana ni poa kwa wajasiliamali kama ipo sustainable. Lakini sijaelewa unato milion 5 unapata milion 12 ndani ya 22 weeks. Wao wanawekeza wapi kuweza kuzalisha pesa ya kumlipa mteja pesa zote hizo. Inaonyesha wanakulipa riba 30% kwa mwezi, hata treasury bills hazina interest yaaina hiyo. Wanapaswa kuchunguzwa ili kujua machanics ya biashara yao.
 
Kibali wlichonacho DECI ni kwa mwanachama kupanda si zaidi ya Sh laki mbili kwa mwanachama lakini wao wanawashurutisha wanachama wapande zaidi ya fedha hiyo na hapo ndio kilio kitakapotokea kwa wanachama wadanganyika

Habari ndio hiyo.....
 
Mh inatisha maana mimi nawafaham baadhi ya watu ambao wamejiunga na hiyo kampuni na wanasema wanavuna pesa ila mimi niliogopa kujiunga maana security yake siijui
 
kusema ukweli mtu hawezi kuanzisha kitu kama hiki kama yeye hatajiriki nacho kwa hio kama watu ambao wamewekeza na wanasema kuwa wanavuna basi mabosi wa hio DECI watakuwa wavuna zaidi yao!
 
Kuna habari kamii juu ya umri wa DECI Tz?
Maana hicho kitu nimekisikia kwa mara ya kwanza wiki iliyopita pale nilipojiwa na mtu akiniambia kuna habari njema Tz (DECI) panda kidogo vuna kingi.

Tuambieni wana umri gani tangu waanze biashara?
 
Mnakumbuka miaka ya 90 kulikuwa na SPA (Self Pregressive Association)?
 
Hata mwaka jana au mwaka juzi kulikuwa na scheme kama hiyo ikiitwa WOMEN EMPOWERMENT ambayo iliwahusisha wanawake vigogo wengi[ Mmoja wao ndio sasa mwenyekiti wa mkoa UWT DSM] mwisho wa yote ikabidi wafikshane kwa Tibaigana!! Hizi pyramid schemes hutumika kuwadhulumu masikini kwahiyo wananchi lazima waelimishwe against this type of fraud.
 
Hakuna kitu hapa, mimi niliwastukia hawa jamaa toka mwanzo, WIZI MTUPU! Kama unamjua mtu amewekeza mwambie akaondoe pesa zake haraka kabla jamaa hawajaishia na kulala mbele!
 
Kuna tetesi kuwa ile Kampuni ya DECI (T) ltd imenyimwa kibali na Central Bank (BOT) cha kuanzisha Scheme nyingine inayoitwa Elimika Scheme inayohitaji mwanachama kutoa Sh milion tano upate sh. Milion 12.5 ndani ya wiki 22.
Tetesi hizi zinadai pia Deci inaweza kuingizwa kwenye adminstration na central bank very soon baada ya kuonekana mabosi wake wanafuja fedha za wanachama kwenye scheme yao ya TRF ambapo mwanachama anapaswa atoe kati ya sh laki mbili apate laki tano. Kwa mwenye taarifa zaidi amwage hapa tuwajadili kwa watz wengi wamewekeza kwenye huu mfuko......

Hii ni sawa na PONZI SCHEME,ndugu Madolff (USA) Investors, anaanzisha kampuni anapata pesa nyingi toka kwa Investors wa Kwanza na kutengeneza mahesabu ya uwongo, Investors wa kwanza wanapata faida kubwa, wanaingia investors wa Pili, na watatu, pesa zinazotolewa na Investors wa tatu anawalipa investors wa Pili, wa tatu analipwa na wanne, mwisho zinafika 50billion usd, zote ninapotea kwa sababu ya financial crisis.

Watch out hii ni kama ponzi scheme.

"Ponzi" Schemes
http://www.nytimes.com/2008/12/12/business/12scheme.html?_r=2&partner=rss&emc=rss
 
Duh! This sounds like a deal to me. Ila kwa hali hii ya global credit crunch, hao jamaa wasije kuingia mitini na fedha za watu. Watu wawe makini kidogo. Hasa wale wenye kipato kidogo kama changu.
 
hawa deci deci jamani vyanzo vyao vya mapato ni nini?naomba waeleze ili wateja wajue na wawe na uhakika na fedha na riba zao.
 
hawa deci deci jamani vyanzo vyao vya mapato ni nini?naomba waeleze ili wateja wajue na wawe na uhakika na fedha na riba zao.
 
Naona bado kidogo watu waanze kulia. Nakumbuka ile hadithi ya nyani na wanunuzi wa nyani! Sasa wameshaanza kuadimika sasa
 
Back
Top Bottom