Dear WEWE........

Dear WEWE.S01E02

Kama unavyokumbuka nilivyokuelezea namna tulivyokutana mara ya kwanza na namna nilivyojitahidi kufanya mchakato wa kuweza kukufahamu vyema (Kumbuka episode ya kwanza ya mtiririko huu) Naomba na leo niendelee kukueleza baadhi ya mabo niliyogundua hasa kutoka kwa zile CCTV zangu ambazo nimezieleza kwa kirefu katika sehemu iliyopita.

Kuna vitu vikubwa vitatu ambavyo nimevigundua ambavyo imenichukua muda sasa kuvitafakari na kuvitafutia njia ya kuweza kuvitatua kama tu zile ndoto zangu ninazoziota kila baada ya siku moja zitatimia. Mambo hayo ni;
  1. Kwamba unapenda sana kufanya shopping hasa ya viwalo na ndio maana unaonekana nadhifu siku zote - naomba niwe mkweli kwamba hili lilinifanya ninyong'onyee moyo wangu kwani kazi ninayofanya kwa muhindi kule mjini inaniruhusu kupata mshahara usiozidi shilingi laki moja na elfu hamsini kwa mwezi lakini baada ya kukuangalia na kukufanyia tathmini kwa muda nikagundua kwamba mshahara wangu wote unatosha kununua pea 2 na nusu tu za viatu unavyovaa wewe.
  2. Unapenda sana kwenda sinema hasa siku za weekend na sikukuu - Nilipata tabu sana kufikiri hili maana mi sinema zangu huwa naenda kuangalia pale kwenye kibanda kilichoandikwa video show na mara nyingi huwa naenda kuangalia filamu za Bongo Muvi maana niliishia darasa la saba na kushindwa kuendelea kwani enzi zetu hakukuwa na shule zile wanaziita "St. Kayumba" Hii imenifanya niwe shabiki sana wa Bongo Movie maana ndizo pekee ninazoelewa. Nikawaza itakuwaje maana we unangalia zile zenu za Hollywood ambazo mi hata sijui neno moja. Mara ya mwisho nilikusikia ukiongea na simu na ukisema kuna movie mpya sijui za kina Angelina Jolie na engineo nimewasahau majina maana yalikuwa magumu. Sasa ntafanyaje wakati mi najua tu kina Kanumba, Ray, Lulu na wengineo?
  3. Mwisho nasikia we ugali huli na wala kuupika hujui - Dah mi mwenzio tangu nimezaliwa wali nimekuwa naupata siku za sikukuu tu maana ili niweze kupata baki ya mshahara wangu basi mchana huwa napiga pasi ndefu maana nikila mchana basi huenda nikabaki na 60,000 tu kwa mwezi. Sasa kama huli ugali itakuwaje na mi hicho ndicho chakula changu kikubwa!

Hata hivyo mi ni mwanaume na kushindwa ni mpaka pale nitakapokuwa nakata roho ndipo nitakubali kushindwa. Kama umegundua katika siku tatu zilizopita nimeanza kubadilika mwonekano. Nilimtembelea rafiki yangu mmoja tulimaliza naye shule ila yeye akapata nafasi ya kuendelea na akanipa viwalo vyake vya siku nyingi ambavyo naona vinanitoa kweli maana naweza hata kuchomekea. Juzi nimepiga moyo konde na kuamua kununua viatu vipya (vile vya kichina vinavyotembezwa na wamachinga" ili angalau niwe smart kidogo.

Dah lakini mabadiliko yangu haya naona sasa yanaanza kuniingiza kwenye mgogoro, hapa ninapoishi kuna binti wa baba mwenye nyumba ambaye sasa ana watoto 3 na kila mmoja ana baba yake. Siku tatu hizi ameanza kuwa ananitembelea na kudai nimpe ushauri hasa nyakati za usiku, nimekuwa nampa ushauri lakini kuna kila dalili sio ushauri anaouhitaji ila ana mengine kabisa. Hali hii sio tu kwamba inaninyima muda wa kupata taarifa kutoka kwenye CCTV zangu bali inaniweka kwenye wakati mgumu sana maana sijalipa kodi kwa miezi miwili sasa na hii ni kwasababu ilinibidi nimlipie ada mdogo wangu na huyu dada ndiye ananikingia ubavu kwa baba yake ili nisitupiwe virago nje. Hata hivyo mpango wangu ni kulipa mwishoni mwa mwezi huu kama nitapewa mshahara wangu.

Sasa si nikapata ufumbuzi wa yale mambo matatu niliyoyasema hapo kabla..............

Don't miss Episode 3
 
funguka M'Jr funguka!usikute unayemfungukia ni hkl nae atakubali tuuu!wenzangu wa PCM wamsubiri Nyani Ngabu.
 
Last edited by a moderator:
shauri zako....

Wanawake wengine hawana marafiki wa kiume..... Wana marafiki wa kike..... Uwiiiiiiiiii usikute ndo huyo sekretari
 
shauri zako....

Wanawake wengine hawana marafiki wa kiume..... Wana marafiki wa kike..... Uwiiiiiiiiii usikute ndo huyo sekretari
Yesuuuuuuuuuu! Inawezekana eeeeeh! Sa mbona unanikatisha tamaa jamani.......
 
niitie tu pacha
mi napenda maelezo bwana sijui ni hii HKL hii yani napenda kidume kijieleze sio haya mambo ya mtu unatuma sms nzuuri af kidume kijibu 'ok' yani huwa natamani mtu aone navofura kwa hasira!mi nimejieleeeza mwenye we cha kunijib mwenzio 'noted' ndo nini!hebu niitie Kaizer anipe maelezo naweza nikampa remedials leo
ha haaaaaaaaaaa mlongo wangu, kuna njemba zinaweza kukufanya nitabasamu kila ukifungua macho asubuhi, yaani nawapendaje!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
ha haaaaaaaaaaa mlongo wangu, kuna njemba zinaweza kukufanya nitabasamu kila ukifungua macho asubuhi, yaani nawapendaje!!!!!!!!!!!!!!!!!

umeona enh!jovaa kamwali!kunyumba yenu huko wazima?mngana wetu?wana?
 
umeona enh!jovaa kamwali!kunyumba yenu huko wazima?mngana wetu?wana?
voha viyumuka kamwali, kunyumba yako vijoha wuli?
naena leo wapo uwanja wako............................. zile sms za ok, yeah, later........ zinabore!
mimi nyumbani kwangi nina injinia, kila kitu ni hesabu tu, ha haaaaaaaaaaaaaaaaa, ukituma sms unapigiwa kupewa jibu, agrrriiiiiiiiii, sms nazo zina raha yake jamani
 
voha viyumuka kamwali, kunyumba yako vijoha wuli?
naena leo wapo uwanja wako............................. zile sms za ok, yeah, later........ zinabore!
mimi nyumbani kwangi nina injinia, kila kitu ni hesabu tu, ha haaaaaaaaaaaaaaaaa, ukituma sms unapigiwa kupewa jibu, agrrriiiiiiiiii, sms nazo zina raha yake jamani
mi hapa huwa natamani kulia,yani mi nimeandika sms yangu tamuuu,nongi ushawahi kuandika sma mpaka unatamani iwe inatumwa kwako!basi ndo kama zile mwenzio ndo huwa naziandika,af ukute unajibiwa kwa simu au kwa neno poa!uwiii!ahahahaahha ila jamani haya mambo yanaenda na fani sijui kha!
 
Dear WEWE.S01E03

Baada ya kujua yale niliyokutana nayo katika kipindi cha siku za hivi karibuni na yale ambayo nimeendelea kugundua kupitia vile vyanzo vyangu vya taarifa, naona bora niendelee kukueleza kwa upande wangu maana kama nilivyosema hapo awali kwamba najua hunijui na najua hukuwa na nia ya kunijua labda baada ya mtiririko huu ndio waweza taka kunijua japo kwa mbali tu.

Kama nilivyokueleza kwenye episode iliyopita kwamba nilipita kwa rafiki yangu tuliyesoma wote siku za huko nyuma na akanipa viwalo vyake za zamani ambavyo ndivyo nadundia siku hizi, sikusita pia kumpa stori nzima kuhusu wewe maana nilihisi kama ningeendelea kukaa nalo moyoni peke yangu ningeweza ota mapembe. Lakini pia niliona ni vyema nikamwambia maana ndiye rafiki yangu pekee ambaye tumebakiza mawasiliano baada ya wale wengine wote kunisahau baada ya kuwa kwenye ulimwengu mwingine wa maisha ambao mimi sipo.

Hata hivyo leo asubuhi nimestuka kidogo, baada ya lile tukio la siku ile kwenye gari niliamua kuwa nawahi kidogo kutoka nyumbani ili angalau niwe nje ya ofisi yenu nikuangalie tu kwa mbali ukifika na kuingia ndipo na mimi niende kibaruani kwangu. Ajabu leo nikiwa pale kwenye kibanda cha magazeti ambapo ndipo husimama siku zote nilishangaa kuona gari la rafiki yangu ndilo lilikupa lift leo. Nilistuka sana maana kwa bahati mbaya huyu rafiki yangu anakaa upande mwingine wa mji ambao kwa namna yoyote ile haiwezekani apite huku mitaa ya kwetu muda ule wa asubuhi na tena bila kunitaarifu maana siku zote akiwa maeneo haya hunipigia simu (huenda alipiga lakini sikupatikana maana betri ya simu yangu pia imeisha hivyo hukaa na chaji kwa muda wa saa moja tu)

Hata hivyo swali la msingi nililojiuliza ni kwanini awe amekupa lift wewe, je ni baada ya mimi kumpa ile stori juu yako au imetokea bahati mbaya tu?! Amini usiamini nilipoona hivyo niliishiwa nguvu, mwili ukapata joto la ghafla na kuanza kutoka jasho kwa wingi, nikaanza kutetemeka kwa hasira na mcahanganyiko wa woga na kukata tamaa kwani niliamini kabisa kwa namna ninavyomjua rafiki yangu yule hapo tayari sina changu.

Nilijikokota polepole mpaka kibaruani kwangu ambako nako sikukaa sana baada ya kuomba ruhusa ya kuwa naumwa na nilikuwa naenda hospitali. Hata hivyo nimerudi nyumbani na kuchukua kalamu na karatasi na kuandika waraka huu ambao naamini utakuwa unausoma sasa maana ilinilazimu kujifanya nimeagizwa kuleta mzigo kwako ili niweze kufikisha rasmi kwako waraka huu. Nashukuru nilifanikiwa maana yule mlinzi wa pale ofisini kwenu ana roho mbaya kama jambazi.

Waraka huu ni kutaka tu kukufunulia yaliyomo ndani ya moyo wangu na amini usiamini ujasiri ulionifanya nikaandika na mpaka kufikisha waraka huu kwako ni mkubwa kuliko wa kugomea urais wa nchi au kukatiza katikati ya mbuga ya Serengeti kwa miguu. Naamini kabisa wanaume wengi huwa wanaandika nyaraka kama zangu ambazo asilimia 95 huwa hawazipeleki kwa wahusika bali huinshia kuzisoma wenyewe na kisha kuziteketeza kwa kukosa ujasiri huu ambao mimi ninao leo.

Usikose episode 4
 
mi hapa huwa natamani kulia,yani mi nimeandika sms yangu tamuuu,nongi ushawahi kuandika sma mpaka unatamani iwe inatumwa kwako!basi ndo kama zile mwenzio ndo huwa naziandika,af ukute unajibiwa kwa simu au kwa neno poa!uwiii!ahahahaahha ila jamani haya mambo yanaenda na fani sijui kha!
hiyo ni fani my dear. kuna watu hawana upako kabisa wa kuandika sms, lakini ukimpa muda wa kuongea nawe tu kwisha habari yako. ila kuna watu ........................................ mkaka anatuma sms 70 kwa siku................ zote tamu na hazijirudii. sijui wanakuwa na vitabu vya mistari?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom