Dear Sir/Madame, Please find my Application Cover letter, CV and Academic Certificat

Ehud

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
2,685
337
Spika wa Bunge Mh. Anna Makinda

Na Mwandishi Wetu

Spika wa Bunge, Anna Makinda na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uratibu, Sera na Bunge, William Lukuvi wamewaonya wabunge kuhusu mavazi na kujiheshimu.

Makinda alisema kuwa katika bunge analoliongoza ni marufuku wanawake kujipodoa kupita kiasi na kuvaa sketi fupi (vimini) wakati Lukuvi alionya vikuku na kuwataka wanaume kufunga zipu za suruali.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Makinda na Lukuvi waliyasema hayo Jumanne iliyopita kwenye Semina ya Wabunge iliyochukua siku 10 na kumalizika Alhamisi iliyopita.


“Ni kanuni za kawaida kuhusu uvaaji. Unajua siyo heshima mwanamke kuvaa sketi iliyo chini ya magoti, kwa hiyo Makinda alikuwa anasisitiza,” kilisema chanzo chetu.

Chanzo hicho kiliendelea: “Kuhusu vipodozi, Makinda ametaka hizi ‘makeup’ zisizidi, wabunge wajitofautishe na wahudumu. Wasijipodoe mpaka rangi ibadilike.”

Kuhusu kauli ya Lukuvi, chanzo chetu kilisema: “Lukuvi ndiye alikuwa mwenyekiti wa semina, siku hiyo aliwaambia kwamba kuvaa vikuku (cheni za miguuni) ni kuwakwaza wanaume.

“Akasema wanaume wawe wanafunga zipu, siyo kukurupuka na kuingia viwanja vya bunge hawajafunga zipu mpaka ‘mambo ya ndani’ yanaonekana.

“Mkazo ulitolewa pia kwenye vikao vya bunge. Watu wanaweza kuvaa wanavyotaka kwenye mambo yao binafsi lakini bungeni na kwenye mikutano inayokutanisha nchi lazima wafuate kanuni.”

WABUNGE WAAMBIWA WAFUNGE ZIPU - Global Publishers
 
huwa nashindwa kuelewa utaratibu wa mavazi bungeni na hasa kwa wabunge wnawake. najua ipo mitindo mingi na wanawake wanaipenda lkini nadhani ni jambo zuri mbunge kujitofautisha na mcheza shoo
 
Your dressing stayle says a lot about you!! Hivi hata wabunge wanavaa vichicken! Job true true.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom