DCs wapanguliwa na kustaafishwa

Nov 11, 2008
782
38
Habari zilizopatika na ni kuwa DCs wamapanguliwa na wengine kustaafishwa bila shaka tuna wanachama wa JF waliopewa SHAVU.
RAIS KIKWETE AFANYA MABADILIKO YA WAKUU WA WILAYA

RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya chini kwa kuwateua wapya 15, kuwastaafisha wengine saba na kuwabadilisha vituo vya kazi 54.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) imeonyesha pia kuwa Wakuu wa Wilaya wawili watapangiwa kazi nyingine na wengine wawili wameteuliwa hivi karibuni kuongoza Jumuiya za Chama Tawala.

Mabadiliko haya yanatarajiwa kuongeza chachu katika usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo yake, kwa mujibu wa taarifa hiyo.

Wakuu wapya wa Wilaya walioteuliwa ni Bi. Mercy Silla (Arumeru, Arusha), Bw. Norman Sigalla (Hai, Kilimanjaro), Col. Issa E. Njiku (Misenyi, Kagera), Bi. Angelina Mabula (Karagwe, Kagera), Dkt. Rehema Nchimbi (Newala - Mtwara), Francis Isaac (Mbulu, Manyara), Lt. Col. Benedict K. Kitenga (Rorya, Mara) na Lt. Col. Cosmas Kayombo (Mbarali, Mbeya).

Wengine ni Bw. Christopher Ryoba Kangoye (Kwimba, Mwanza); Bi. Queen Mwanshinga Mlozi (Ukerewe, Mwanza); Bi. Fatuma Mwassa (Mvomero, Morogoro); Bi. Fatma Ally (Nanyumbu, Mtwara); Bw. Juma Solomon Madaha (Tunduru, Ruvuma); Bw. Anatory Choya (Kishapu, Shinyanga) na Bw. Erasto Sima (Korogwe, Tanga).

Wakuu wa Wilaya waliostaafishwa na vituo vyao kwenye mabano ni Bw. Elias Maarugu (Misenyi, Kagera); Bw. Deusdedit Mtambalike (Muleba, Kagera); Bw. David Holela (Babati, Manyara); Bi. Hawa Ngulume (Mbarali, Mbeya); Bw. Mashimba H. Mashimba (Kyela, Mbeya); Col. Peter Madaha (Nyamagana, Mwanza) na Bw. Gilbert Dololo (Kibaha , Pwani).

Wakuu wa Wilaya ambao wamepangiwa kupewa kazi nyingine ni Bw. Patrick Tsere aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala (Dar es Salaam) na Bi. Doreen Kisamo aliyekuwa Uyui (Tabora).

Bw. Martin Shigela aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi (Lindi) aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM wakati Bi. Husna Mwilima aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai (Kilimanjaro) aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UWT
 
Last edited:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Bw. Martin Shigela aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi (Lindi) aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM wakati Bi. Husna Mwilima aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai (Kilimanjaro) aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UWT.
 
Attachments

  • JK_MA_DC.doc
    135.5 KB · Views: 223
Hopeful Mr Mnali ataletwa wilaya moja ya Dar maana huku tunamtaka.
 
Huyo Mercy Sila ndo mkurugenzi wa TEA? Ina maana ataachia ngazi hapo ili akautumikie ukuu wa wilaya,si ndiyo?
 
Huyu mercy silla ni kwamba kaongezewa kula au kapunguziwa? Au anaandaliwa kwa nafasi nyeti!?
 
Hawa Ngulume amestaafishwa kama ilivyokuwa inafikiriwa huku Patrick Tsere ambaye wananchi walianza kumpigia kelele Ilala akienda kupangiwa kazi nyingine, Tsere anaweza kupelekwa ubalozini.
 
RAIS KIKWETE AFANYA MABADILIKO YA WAKUU WA WILAYA

RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya chini kwa kuwateua wapya 15, kuwastaafisha wengine saba na kuwabadilisha vituo vya kazi 54.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) imeonyesha pia kuwa Wakuu wa Wilaya wawili watapangiwa kazi nyingine na wengine wawili wameteuliwa hivi karibuni kuongoza Jumuiya za Chama Tawala.

Mabadiliko haya yanatarajiwa kuongeza chachu katika usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo yake, kwa mujibu wa taarifa hiyo.

Wakuu wapya wa Wilaya walioteuliwa ni Bi. Mercy Silla (Arumeru, Arusha), Bw. Norman Sigalla (Hai, Kilimanjaro), Col. Issa E. Njiku (Misenyi, Kagera), Bi. Angelina Mabula (Karagwe, Kagera), Dkt. Rehema Nchimbi (Newala - Mtwara), Francis Isaac (Mbulu, Manyara), Lt. Col. Benedict K. Kitenga (Rorya, Mara) na Lt. Col. Cosmas Kayombo (Mbarali, Mbeya).

Wengine ni Bw. Christopher Ryoba Kangoye (Kwimba, Mwanza); Bi. Queen Mwanshinga Mlozi (Ukerewe, Mwanza); Bi. Fatuma Mwassa (Mvomero, Morogoro); Bi. Fatma Ally (Nanyumbu, Mtwara); Bw. Juma Solomon Madaha (Tunduru, Ruvuma); Bw. Anatory Choya (Kishapu, Shinyanga) na Bw. Erasto Sima (Korogwe, Tanga).

Wakuu wa Wilaya waliostaafishwa na vituo vyao kwenye mabano ni Bw. Elias Maarugu (Misenyi, Kagera); Bw. Deusdedit Mtambalike (Muleba, Kagera); Bw. David Holela (Babati, Manyara); Bi. Hawa Ngulume (Mbarali, Mbeya); Bw. Mashimba H. Mashimba (Kyela, Mbeya); Col. Peter Madaha (Nyamagana, Mwanza) na Bw. Gilbert Dololo (Kibaha , Pwani).

Wakuu wa Wilaya ambao wamepangiwa kupewa kazi nyingine ni Bw. Patrick Tsere aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala (Dar es Salaam) na Bi. Doreen Kisamo aliyekuwa Uyui (Tabora).

Bw. Martin Shigela aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi (Lindi) aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM wakati Bi. Husna Mwilima aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai (Kilimanjaro) aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UWT

UPDATES FROM HALISI
 
...Yuko wapi Betty Mkwasa? naona wilaya yake ya Korogwe kapewa mtu mwingine! Fatuma Mwassa ni huyu ambaye mpaka juzi juzi ni muandishi wa habari sijui wa Majira ama kule kwa Mafisadi?? Tujuzeni....
 
Atakuwa kahamishwa kituo kama habari inavyosema kuna waliohamishwa wilaya zingine.
 
Huyu Fatma Mwassa aliyeteuliwa kuwa DC Movomero namfahamu vizuri.

Siku za karibuni alikuwa msaidizi wa mama masuala ya Jamii. Sina hakika kama kweli waliomteua wanajua wamefanya nini. Kwasababu she is seriously nothing in terms of ability to perform. Ni kama wameamua kumtoa Ikulu baada ya kuona ni mzigo. Sasa mzigo wamekabidhiwa wananchi wa mvomero waubebe. Kweli tutafika?

Mwingine ni huyu kijana wa Makete Mapembelo Va Vene Norman mume wa bibi Pindi chana aka Mjumbe wa kamati Kuu na Mb. Huyu naye is some sort of mR. Show off. hawezi hata siku kuleta lolote katika suala zima la kusimamia mabadiliko ya msingi vijijini. Hivi sasa amekuwa akipita pita mitaa ya ipelele, mwalusa, madihani, utengule na lupila akitafuta kura mwakani.

Tusubiri tuone au ndiyo mwanzo wa ngoma nyingine mpaya ya kuisukuma ccm mwambani. More to come kwa sababu pindi chana mke wa DC Mteule yupo ludewa akijaribu kuwalaghai wapangwa kuwa yeye ni mzaliwa wa huko wakati ni chotara wa kisingasinga. namhurumia Prof. Mwalyosi Bingwa wa masuala ya mazingira. Darry rwegasira mama mwenye msimamo thabiti asiyepindishwa kwa vijisenti amehamishwa kupisha Mulla adhulumu mashamba ya walupembe.

Mr. Mbwilo kama kawaida yake ni bwana Sindbad au Marco Pollo bingwa wa kuvumbua wilaya mpya kila kukicha. Ameshahama zote mtwara ni ya mwisho itabidi waunde mpya na hana jipya. Wamemsahau Dr. Mfutakamba msanii maarufu wa Kilolo. Uhahula Mhhh! Sasa tunasubiri RCs nao itakuwaje.

Bila shaka Mwakipesile aliyewshindwa kumlinda Rais wakati wa ziara yake Mbeya atasalia. Njolay ataondolewa kwakuwa anapenda kujituma, Parseko Kone mteule wa Mr. White Hair ataongezewa mikoa mingine miwili ili adhulumu mashamba ya watu na Bibi Hajjat Amina Mrisho Said msemakweli daima atapumzishwa ili kweli isitawale tena.

Oh! nilisahau Mzee suti smart boy kalembo yeye ataendelea kutawala moro kwasababu ya sifa yake ya usafi wa suti na uvivu wa kazi. Asiishie hapo mzee wa kaya hawa watendaji wake walioamua kumzunguka mzee wa kuangua kilio bungeni kwa kupiga unafiki wa kukataa kongomano huku wameamua kujimwaga mikoani kwa kisingizio cha kukagua miradi ili watafune hazina ya umma. Hebu fikiri vikundi tofauti 10 kutoka TUNAWASEMA(TAMISEMI) kila wiki vinakagua shamba moja la mfano mahindi.

Wizi mtupu.

Naambiwa watakuwa na ziara nyingine nyandaza juu kusini kwa wiki mbili kutafuna vizuri. this wanakuja 68 kwa makundi manne ambayo yatasambaa kwenye mikoa hii. Wooh wooh
 
Mnali je??ukute nae amehamishwa tu...maana ana back up kubwa ya wazalendo wenzake hahahh ....heri ngulume apumzike maana duu nashangaa hata hapo alipofika...mpika chai wa uwt leo mkuu wa wilayaa hahaha sio karne hii....
 
haki ya Mungu nchi hii tabu tupu!, sasa lazima aseme hao aliowastaafisha kwa manufaa ya umma aseme sababu nini.kila siku abadiliko na hakuna maendeleo ila unafiki tupu na wizi.
 
Back
Top Bottom