OPTIMUS TZ
JF-Expert Member
- Jan 30, 2012
- 391
- 65
Bado sitta! Uraisi mchezo 2015 sina hamu mungu uniweke hai; ikiwezekan tuhairishe miaka ilitufanya huo uchanguzi
Mkuu Nguruvi3, kumsababishia maumivu binadamu yoyote ni kosa la jinai, hivyo kumpiga mkeo pia ni kosa la jinai. Jirani yako kasikia kelele ya mkeo anakula kichapo na kusikia sauti yako ukisema "leo nitakuua wee mwanamke"!. Jirani katoka mbio kukuripoti polisi kuwa kuna jinai inatendeka jirani kwake!. Polisi na defenda mbio nyumbani kwako ili kuzuia jinai!.Mkuu Pasco, kwa vile tukio hili lina hisia kali na limeleta sintofahamu katika jamii nina uhakika DCI ametoa amaelezo hayo kwa sababu hizo. Maelezo yake hayajitoshelezi na yanazidi kuchochea hisia zaidi ya kufafanua.
Tungeelewa endapo DCI angetuambia kuwa Dr Mwakyembe hakuridhia kueleza kinachomsumbua. Hiyo ni haki ya mgonjwa.
Hakufanya hivyo. Kwa maana nyingine natural justice haikutendeka. Amechukua kesi, ameendesha mashitaka na ametoa hukumu bila ya kusikiliza upande wa pili.
Dr Mwakyembe atakaposimama na kutoa maelezo na endapo atasema amelishwa sumu, basi DCI na serikali hawatakuwa na pa ksuimama kwasababu 'the disclosure rights lies with the patient' nasi tutachukua 'from horse mouth'.
Unapompa right ya ku disclose tatizo lake umetupa right ya kuamini atakachosema.
Right ni yake na haina mjadala lakini mazingira lazima yatazamwe.Suala la Dr Mwakyembe ni zaidi ya right za mgonjwa
Lakini pia usisahu kuwa serikali imekuwa inatupiana mpira, na DCI ni sehemu ya serikali. Kusikia tu kutoka kwao bila kusikia kauli ya Mwakyemebe kupitia kwao ni tatizo kubwa. Tulitegemea ima waseme wamepata au wamekosa ushirikiano ili tujue natural justice imefanyika. Alichokifanya DCI ni kuchochea moto na si kuzima.
Je itakapokuja kujidhihirisha kwamba kinachomsumbua Dr. Mwakyembe ni Sumu awe amelishwa au aliwekewa kwa njia yoyote ile, atakuja kusemaje! Mijitu mingine bwana, itakuja kupelekwa The Hague bure kwa makosa ya watu wengine kutokana na ujinga wao!
Mkuu Ngongo, the disclosure rights lies with the patient. Hivyo hilo ni jukumu la Mwakyembe mwenyewe!.
Mwosha HUOSHWA.Kwa wanaharakati Mwakyembe ni traitor so anavuna alichokipanda
Well said! Anavuna alichopanda. Polis wamfungulie mashitaka Sita kwa kuhatarisha amani ya nchi na kutoa maneno ya uchochezi.
Hivi waziri mkuu alishindwa nn kusema kwamba mwakyembe hajalishwa sumu.?
unategemea dci asemeje,kwanza intelligensia yake sufuri,mtu ataingiaje na radioactive material nchini bila yeye kujua si bora tuishi hivyo hivyo,hawezi sema kwa sababu au anajua game nzima au kuna uzembe mkubwa kiutendaji.MBONA REPORT ZINGINE ZA INTELIGENSIA WAKATI WA MAANDAMANO ZINATANGAZWA AU NI KUPIKAhii ni kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari mchana wa leo. Katika maelezo yake, dci anasema kwamba:
"kutokana na uchunguzi wa kipolisi ulioshirikisha wizara ya afya na ustawi wa jamii, hakuna ushahidi juu ya hilo".
Alipoulizwa na waandishi wa habari:
je, dr. Mwakyembe anasumbuliwa na maradhi gani?
dci alijibu kwamba:
"kazi ya jeshi la polisi sio kuchunguza maradhi bali kuchunguza tuhuma, na baada ya uchunguzi wake kwa kushirikiana na wizara ya afya na ustawi wa jamii, jeshi la polisi limebaini kwamba tuhuma kwamba dr. Mwakyembe amelishwa sumu hazina ukweli."
Mwenye uwezo wa kusema kuhusu jinai au laa ni DCI tuu. Na kama wangekuta jinai then wangepeleka kwa DPP ndiye pekee mwenye kuamua aendeshe mashitaka au la. Na DPP angeamua kuendesha mashitaka, bado mahakama ingesikiliza ushahidi wa DPP na kuamua kama kuna kesi ya kujibu au laa!.hivi huu ni uchunguzi au kuchukua taarifa kutoka wizara ya afya? Hivi waziri mkuu alishindwa nn kusema kwamba mwakyembe hajalishwa sumu.?
Mkuu Pasco, nikukumbushe kuwa kuna mtu aliwahi kueneza tuhuma kuhusu wewe nadhani unakumbuka. Yeye alisema pasco ..... kwa kutumia vigezo na hisia.Mkuu Nguruvi3, Walipofika wakakuta ugomvi umeisha wakauliza kama kuna tatizo, wewe ukasema hakuna tatizo, unadhani polisi watafanya nini?. Hawata fanya lolote kwako wala kwa mke wako, bali huyo jirani yako aliyeripoti tukio, watarudi nae kituoni kumchukua maelezo!.
Aliyewekewa sumu ni Mwakyembe hajaripoti polisi kuhusu kuwekewa sumu. Aliyepayuka hadharani kuhusu jinai ya sumu ni jirani (Sitta). Polisi wamechukua maelezo ya Sitta na kufanya uchunguzi, wakakuta hakuna jinai ya sumu!. Mwakyembe mwenyewe wala familia yake hawajalalamikia sumu!. Sasa kinachofuatia ni Jirani kushitakiwa kwa kuisumbua polisi na kwa case ya Mwakyembe sio tuu kuisumbua polisi bali uchochezi ili wananchi waichukie serikali yao kwa kuiona ni serikali ya wauaji!.
Mwakiyembe anaumwa, hajalalamikia kupewa sumu. Jirani ndio anae eneza uvumi wa simu ili kuwanyooshea kidole mahasimu wake wa kisiasa!. Sasa kwa vile issue ilikuwa ni kupewa sumu, imethibitika sio sumu!. Mwambieni jirani sasa na atoe uthibitisho, ila its high time Dr. akirudi toka matibabu ya India awaambie Watanzania ukweli wa anachoumwa!.