DCI Manumba: Mwakyembe hajalishwa sumu!

Lakini Dr Kasema kuwa anakwenda Appolo atakapo rudi ndio ataweka wazi,so tusubiri na subira huvuta kheri
 
Kwa hiyo wanataka kutuaminisha kwamba sitta ni muongo,lakini kutokana na ukaribu uliopo kati ya sitta na mwakyembe nachelea kusema kwamba polisi wetu ni wanafiki kutokana na sababu zifuatazo:

Moja: Kama kweli wao wanahusika na uchunguzaji wa tuhuma walikuwa wapi kuchunguza tuhuma za mara ya kwanza ambapo mwakyembe aliwaandikia barua poilisi na kuwatarifu kwamba kuna watu wanataka uhai wake,kama kweli walichunguza mbna hawkuweka wazi matokeo ya uchunguzi je ni kipi kilicho wasukuma kuweka wazi matokeo ya uchunguzi huu ambao ni matokeo ya uzembe uliofanywa na polisi mara ya kwanza,je ni kwann vyombo vyetu vya ulinzi vimekuwa siyo huru?

Mbili: Kama kweli wamefanya hiyo kazi kwa kushirikiana na wizara ya afya basi itakuwa wamehusika watalaam kama madaktari ili kusudi waweze kuujua ukweli,je ni kwa nini wameshindwa kuweka wazi ripoti ya wachunguzi(madaktari) ili kusudi uuma wa watanzania ujue tatizo hasa lilikuwa ni nini?
 
Hajapewa sumu Huyu kweli?! Mmmmh!
Nakumbuka few years back kuna shushushu mmoja wa cjui Ni KGB ilee Amaaa....aliingia kwny 18 za watu wakamrekebisha, end of a day jamaa alipukutika kila kile kinachoitwa unywele mwilini mwake....skin cancer! Akavuta, alionyeshwa sana CNN, BBC etal.
Sasa nijuavyo mhishimiwa sana Huyu dizaini naye aliingia kwny 18 za watu, nikirudi nyuma kidogo katika tukio linalolandana na hili ktk inji hii kuna junalist KUBENEA nae Ni mhanga wa kuingia kwny 18 za wanene wenye uozo akaambulia tindikali akaishia India Kama mhishimiwa dokta mwaEMBE.
Tunakushukuru sana DcI kwa taarifa yako, tumekusikia ILA binafsi " SIJAKUFIKIA".
 
Aisee.! Kazi ipo, ni Zamu ya Mwakyembe sasa kuweka wazi matokeo ya vipimo vya ugonjwa wake Ukweli Ujulikane.!
 
Mkuu Ngongo, the disclosure rights lies with the patient. Hivyo hilo ni jukumu la Mwakyembe mwenyewe!.
Mkuu Pasco, kwa vile tukio hili lina hisia kali na limeleta sintofahamu katika jamii nina uhakika DCI ametoa amaelezo hayo kwa sababu hizo. Maelezo yake hayajitoshelezi na yanazidi kuchochea hisia zaidi ya kufafanua.

Tungeelewa endapo DCI angetuambia kuwa Dr Mwakyembe hakuridhia kueleza kinachomsumbua. Hiyo ni haki ya mgonjwa.
Hakufanya hivyo. Kwa maana nyingine natural justice haikutendeka. Amechukua kesi, ameendesha mashitaka na ametoa hukumu bila ya kusikiliza upande wa pili.

Dr Mwakyembe atakaposimama na kutoa maelezo na endapo atasema amelishwa sumu, basi DCI na serikali hawatakuwa na pa ksuimama kwasababu 'the disclosure rights lies with the patient' nasi tutachukua 'from horse mouth'.
Unapompa right ya ku disclose tatizo lake umetupa right ya kuamini atakachosema.
Right ni yake na haina mjadala lakini mazingira lazima yatazamwe.Suala la Dr Mwakyembe ni zaidi ya right za mgonjwa

Lakini pia usisahu kuwa serikali imekuwa inatupiana mpira, na DCI ni sehemu ya serikali. Kusikia tu kutoka kwao bila kusikia kauli ya Mwakyemebe kupitia kwao ni tatizo kubwa. Tulitegemea ima waseme wamepata au wamekosa ushirikiano ili tujue natural justice imefanyika. Alichokifanya DCI ni kuchochea moto na si kuzima.
 
Hii ni kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari mchana wa leo. Katika maelezo yake, DCI anasema kwamba:

"Kutokana na uchunguzi wa kipolisi ulioshirikisha Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, hakuna ushahidi juu ya hilo".

Alipoulizwa na waandishi wa habari:

Je, Dr. Mwakyembe anasumbuliwa na maradhi gani?


DCI alijibu kwamba:

"Kazi ya Jeshi la Polisi sio kuchunguza maradhi bali kuchunguza tuhuma, na baada ya uchunguzi wake kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jeshi la Polisi limebaini kwamba tuhuma kwamba Dr. Mwakyembe amelishwa sumu hazina ukweli
."

Ni wazi kuwa Jeshi la Polisi halichunguzi maradhi, lakini hii tuhuma ni kama Polisi WAMELAZIMISHWA KUIJIBU HIVYO.
Haihitaji mtu mwenye akili sana kuunganisha mambo mawili ili kupata jibu.
1 Mwakyembe anaumwa ugonjwa usiojulikana na unaoendelea kuteketeza mwili kwa kasi kuanzia mwaka jana
2 Polisi hawa kuwahi kutoa taarifa zozote kuhusiana na hili hadi wananchi/vyombo vya habari vilipo anza kudodosa, pamoja na
vya habari kufuatilia sana.
3 Kuna tuhuma za nyuma juu ya kutishia maisha ya Dr Mwakyembe ambazo Polisi walizipuuza vile vile
4 Taarifa ya Madktari wa India haijatolewa hadharani:Dr Mwakyembe is a public figure umma unatakiwa kufahamu

Kama Srikalai kwa maana ya Wizara ya Mambo ya Ndani na Wizara ya Afya zote zina mung'unya maneno juu ya hili, basi wananchi watakuwa na conclusion zao.
COCLUSION NO 1: Aliyebuni mkakati wa kumlisha sumu Dr Mwakyembe ni lazima yupo JUU ya Wizara zote mbili!!!!
Haya wana JF endeleeni na kuchambua.
 
In a country notorious for impunity and pervaded with massive corruption like Tanzania, such facile answers from authorities are not entirely unanticipated. Whether DCI's remarks are believable or not, Sitta should equally be pinned down to elaborate and corroborate his poison allegations so that to balance things.

Umenikuna...

Sita alitusaliti watz... why alizima hoja ya Richmond bungeni!!!!!?????????????????????????????????????? Aseme sasaaaaa!!!!!!

Mwakyembe bado nampenda anayo bado harufu ya upambanaji, ila sita, Anne Kilango, Ole sendeka, yule wa kahama, sijui zambi, etc wamenitoka kabiasa... wamekuwa wasaliti siku hizi kila wanaposimama kuongea bungeni, majukwaani au popote pale,,,, wao ni kulinda maslahi yao tu...itakula kwao na imeshakula kwao kwa kujipendekeza... aaaah kuna mmoja yeye si ktk wapambanaji huyu jamaa Magufuli nilimpenda sana ila naye kajichanganya tayari...hana mwelekeo/msimamo thabiti.....

Mwakyembe aliposimama kuisoma ile taarifa ya kamti teule ya bunge kuhusu richmond sikuamini niliyokuwa namsikia akiyasoma na sikuamini macho yangu nilivyomwona alivyokuwa jasiri siku ile. Ila baada ya siku au miezi kadhaa akaniudhi sana aliposimama siku moja tena bungeni na kusema ".....kama mnataka rudisheni basi tujadili upya kuhusu richmond tuseme yale ambayo hatukusema kwa heshima ya serikali..." hapo tena akanishangaza sana, ghafla nikamchukia siku ile... lakini nikajua naye ni mwanadamu....anaudhaifu kama wengine yaani aliingiwa na woga kufanya kweli au kumaliza mchezo kama sita alivyo fanya.... ni kama vile walitusalati.

Bado nina matumaini na Mwakyembe kbu anayo nafasi ya kuweka mambo sawa na kumaliza mchezo juu ya afya yake na pa tena asitueleze mambo ya kulinda heshima ya serikali...wenzake mbona hawalindi heshima yake..;kwa kumvalisha maglove na kuharibu ngozi na nywele zake.... na kama nia pia ilikuwa kuitoa roho yake tuseme yeye alikuwa amekufa ni Mungu tu kashikilia uhai wake...sasa anaogopa nini maana kifo alichungulia/amechungulia...afanye kweli Mwakyembe kwa faida ya watanzania. Hata Yesu aliutoa uhai wake kwa faida ya ulimwengu...kila atakaye mwamini asipotee bali awe na uzima wa milele...amabye hatamwamini Yesu basi atakuwa amejihukumu mwenyewe.... ni moto wa milele>>>....kbu ya dhambi....
 
Kama hajalishwa sumu wangetoa ufafanuzi nini kinamsibu ?.

Ngongo, DCI anasema Dk Mwakyembe HAJALISHWA sumu, kwa maneno mengine hajakanusha kuhusu sumu labda Dk Mwakyembe amejilisha sumu mwenyewe; alitaka kujinga?
 
Hivi polisi hao hao zile zile tuhuma alizotoa kwamba alshabaab wanataka kumuua walizifanyia kazi na kutoa maelezo km walivyoharakisha kukanusha hili la kulishwa sumu?
Mkuu Wambandwa, zile tuhuma zimeshindwa kuthibitishwa kutokana na kukosekana ushirikiano.

Nilipata bahati to hear from the horses mouth, kuwa watekelezaji waliconfess kwake mwenyewe na kwa vile yeye ni mwanasheria, anaelewa umuhimu wa évidence, hivyo akawachukua maelezo zao huku anawarekodi kwenye video huku wakiwa wameficha nyuso zao kuficha sura zao wasibainike.

Hiyo video ikawa duplicated to make several copies na copy ikapelekwa kwa IGP copy kwa DCI, copy Tiss, copy Ikulu na copy kwa zile balozi mbili muhimu sana hapa nchini. Police did nothing!.

Taarifa zikapatikana kuwa polisi walisema ili kuzifanyia kazi tuhuma hizo kwenye hizo video recorder confession, ni lazima polisi ndio wamuhoji huyo alieconfess na sio kuhojiwa na mlalamikaji. Jamaa aligoma kumdisclose!, na issue ikaishia hapo.

Ila from the horses mouth aligoma kumdisclose kwa sababu alimpromise ku trade in confession with a solid promise of non disclosure ili asishitakiwe kwa hayo aliyo confess!.

Kwa vile Dr. ni law professional, he knows better how this things work!. Kwa jinsi nilivyomsikia with my own ears, niliconclude its another of his sensetional crime fiction story!.
P
 
Kama Hiyo ndiyo taarifa ya kipolisi basi either Samweli sita ajiuzuru uwazili kwa uzushi ama aje mbele ya vyombo vya habari na kuweka wazi ushahidi wake na kuwaumbua polisi.

ni mtizamo wangu tu!
DCI hadi leo hajajibu malalamiko ya Dk Mwakyembe
ya awali kuhusu wageni walioingia nchini kwa ajili ya kumuua, pamoja na Dk Mwakyembe kutoa ushahidi wa jinsi walivyoingia, magari waliyotumia nk.
 
Mbona Manumba hakuna mahala kasema wameshirikiana na sitta, Mwakyembe,, je muhusika (mwakyembe) na mtoa tuhuma (sitta) hawakupaswa kushirikishwa katika uchunguzi huo?
 
Iko hivi Dr Mwakyembe ni kweli kabisa hakuwekewa sumu kwenye chakula. Sumu iliingiaje kwenye mfumo wa kimwili wa Harrison? Alikuwa akiviziwa sana na jamaa walimwekea sumu kwenye sabuni ya kunawia mikono Dodoma, mara baada ya kuitumia ile sabuni ilitoweka. Cartel ya waliohusika kufanya uharamia huo wa kumtegeshea sumu Mwakyembe inaongozwa na Mbunge wa Monduli, ambaye bunge lilimlazimisha aachie ngazi nafasi ya uwaziri mkuu. Wahusika wote waliisha lipwa kwa kazi hiyo na wana kiapo cha kutosema kwa mtu yeyote.

kwanini hukujitokeza polisi kutoa ushahid?acha ushigongo!
 
Wanabodi, tuacheni conspiracy theories, vuteni subira kwanza mkijue anachoumwa ndipo mziendeleze hizi conspiracy theories zenu!.

Serikali makini itamshughulikia Sitta haraka iwezekanavyo, scrap him his ninisterial positions na kumpandisha kizimbani kwa kosa la "uchochezi"!.

Hicho ndo kitakachofuata.
 
Hivi nyie kwa akili zenu na uelewa wenu mnadhani DCI angekuja na jibu kua nikweli Mwakyembe alilishwa sumu hata kama alilishwa?
 
Dah stori za Mwakyembe na kundi lake la makamanda feki sina uhakika kama zinatija tena kwa kwenye mijadala ya harakati za Tanzania mpya.
 
In a country notorious for impunity and pervaded with massive corruption like Tanzania, such facile answers from authorities are not entirely unanticipated. Whether DCI's remarks are believable or not, Sitta should equally be pinned down to elaborate and corroborate his poison allegations so that to balance things.
This is too Sweety Radhia.
 
Back
Top Bottom