Serikali makini itamshughulikia Sitta haraka iwezekanavyo, scrap him his ninisterial positions na kumpandisha kizimbani kwa kosa la "uchochezi"!.
Sita ana kiherehere, alolishwa sumu hajasema yeye akaropoka! Hivi kweli Mwakyembe apewe sumu asiseme?. Mimi nionavyo labda alipewa kemikali fulani au anaumwa ngoma au sukari!. Kuna mgonjwa wa kisukari namfahamu ukimwona ngozi yake nayo inatoa ukurutu!.
Kwani walikuwa wanachunguza nini????Well, nadhani habari hii ndivyo ilivyotegemewa kutoka kwa 'polisi' wetu hasa kuhusiana na Mwakyembe!
mi nadhani mhusika aweke wazi kinachomsumbua,kwani anaogopa nini?si wana mafaili ya hospital wayaweke wazi! mi nafkiri mda si mrefu atajitokeza hadharani na kuzungumza
Tukubali sisi kama wananchi lazima tujue tunataka nini! Tunataka tu uthibitisho kama Mwakyembe kala sumu tu? Mbona inaweza kuja ripoti ya kupikwa mkachoka kuwa ni kweli ni sumu ila inapatikana kwenye vyakula na kama una allergy flani basi utadhurika! Then tutauliza nini? Polisi wamejibu pressure ya kwanza ili pressure ikizidi waseme hakula sumu bali allergy(may be)! Lazima tutengeneze base ya maswali ili si Polisi wala Mwakyembe wataocheza na ukweli kwa maslahi flani! All in All Mwakyembe amebaki na goli lisilo hata na kipa ni kupasia tu nyavu! Kama ni mjanja ajibu haraka kuhold pressure ya wananchi baada ya DCI kutoa ripoti!In a country notorious for impunity and pervaded with massive corruption like Tanzania, such facile answers from authorities are not entirely unanticipated. Whether DCI's remarks are believable or not, Sitta should equally be pinned down to elaborate and corroborate his poison allegations so that to balance things.
Ah! kweli kwa vile wewe ni Kasisi Rev Fr nitakuamini kabisa!Iko hivi Dr Mwakyembe ni kweli kabisa hakuwekewa sumu kwenye chakula. Sumu iliingiaje kwenye mfumo wa kimwili wa Harrison? Alikuwa akiviziwa sana na jamaa walimwekea sumu kwenye sabuni ya kunawia mikono Dodoma, mara baada ya kuitumia ile sabuni ilitoweka. Cartel ya waliohusika kufanya uharamia huo wa kumtegeshea sumu Mwakyembe inaongozwa na Mbunge wa Monduli, ambaye bunge lilimlazimisha aachie ngazi nafasi ya uwaziri mkuu. Wahusika wote waliisha lipwa kwa kazi hiyo na wana kiapo cha kutosema kwa mtu yeyote.
Manumba said:"Mwakyembe amelishwa sumu, tena kalishwa sumu mbaya kabisa ambayo inaua taratibu na kabala hujafa huifanya ngozi yako imomonyoke na uchakae uwe kama takataka, tena sumu yenyewe inahitaju ujuzi mkubwa kuigundua ikiwa mwilini kwani mtu akishakula tu chemical composition zake hubadilika hivyi si rahisi kugundua ni sumu ya aina gani.
Uchunguzi zaidi umebaini waliohusika na kumlisha ni wale vinara waliojeruhiwa katika sakata la Richmond. Kwa kuwa bado wana mihela mingi na wanafahamu siri nyingi za kaka mkubwa hao watu hawatashughulikiwa labda kama Mwakyembe na wenzake wanaojifanya wanapambana na ufisadi waendelee kupambana nao.
Lakini sisi kama jeshi la polisi tunatoa wito kwa Mwakyembe na jamaa zake kuachana na hao jamaa kwani ni hatari sana, na bila kuficha tunapenda kumwambia Mwakyembe ana bahati sana, ashukuru Mungu wake alikuwa hajalala la sivyo angekiona cha mtema kuni, hicho kilichompata ni ni sawa kuonjeshwa karanga mbili na muuza karanga mwenye kapu la kilo ishirini. Sio sisi polisi tu ambao hatuwawezi hata hii nini hii yenyewe baraza la mawaziri hawaiwezi"