DCI Manumba: Mwakyembe hajalishwa sumu!

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
Hii ni kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari mchana wa leo. Katika maelezo yake, DCI anasema kwamba:

"Kutokana na uchunguzi wa kipolisi ulioshirikisha Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, hakuna ushahidi juu ya hilo".

Alipoulizwa na waandishi wa habari:

Je, Dr. Mwakyembe anasumbuliwa na maradhi gani?

DCI alijibu kwamba:

"Kazi ya Jeshi la Polisi sio kuchunguza maradhi bali kuchunguza tuhuma, na baada ya uchunguzi wake kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jeshi la Polisi limebaini kwamba tuhuma kwamba Dr. Mwakyembe amelishwa sumu hazina ukweli."
---
MKURUGENZI wa Mashtaka (DPP), Eliezer Feleshi, amelirudisha kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), jalada la kesi ya waliodai ugonjwa wa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Mwakyembe, umetokana na kulishwa sumu.

Katika mahojiano maalumu na gazeti hili juzi, DPP Feleshi alisema , baada ya kulipitia jalada hilo, ameona alirudishe tena polisi ili likafanyiwe kazi zaidi.

Ofisi ya DCI ilikuwa imelipeleka jalada hilo kwa DPP ili atoe baraka za kupeleka kesi hiyo mahakamani.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba alipotakiwa kueleza hatua ambazo ofisi yake inachukua baada ya kurejeshwa kwa jalada hilo alisema “Mimi sina usemi (na kukata simu).”
Manumba alilipeleka jalada hilo kwa DPP baada ya kuzungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, mwezi uliopita akisisitiza atawapeleka mahakamani wote waliotoa taarifa kuwa ugonjwa uliokuwa unamsumbua Dk Mwakyembe unatokana na kulishwa sumu.

Manumba alisema , uchunguzi uliofanywa na polisi pamoja na kupata taarifa kutoka hospitali ya Appolo nchini India, ambako Dk Mwakyembe alikuwa akipatiwa matibabu, zinaonyesha kuwa ugonjwa wake hautokani na kulishwa sumu.

Wakati DCI alipopeleka faili hilo kwa DPP, Dk Mwakyembe alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akisema: “Napata tabu kuamini kama DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matibabu yangu au walisoma taarifa ‘nyingine’ na kama waliisoma taarifa hiyo wenyewe au ‘walisomewa!’

“Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba kwa waandishi wa habari, hakifanani kabisa na picha iliyoko kwenye taarifa halisi ya Hospitali ya Apollo.

Mkakati huo wa DCI ulizua malumbano na misimamo iliyoashiria kuwapo kwa kauli zinazokinzana na kuzihusisha wizara nne tofauti iwamo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mambo ya Ndani ya Nchi, Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Ujenzi.

Kuna wakati Waziri Sitta alinukuliwa akisisitiza kwamba hisia zinaonyesha ugonjwa huo unatokana na kulishwa sumu wakati Wizara ya Afya ilionyesha kushangaa ripoti hiyo huku Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsa Vuai Nahodha akisema kuwa hajui zilikopatikana taarifa hizo na kuamua kuunda tume ya kuchunguza kwa undani kuhusu suala hilo.

Hata hivyo baada ya kurejea nchini Ijumaa iliyopita akitoa India alikoenda kwa matibabu, Dk Mwakyembe alisema, kwa sasa amepona kabisa na anaendelea na kazi za kulijenga taifa pasipo na wasiwasi wowote.

Alizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juzi, alisema ugonjwa uliokuwa ukimsumbua unafahamika kitaalamu kwa jina la Popular Scleroderma.

Dk Mwakyembe amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi ambayo yaliifanya Serikali kuamua kumpeleka Hospitali ya Appolo, Oktoba 9 mwaka jana na kurejea Desemba.

Dk Mwakyembe alisema anachoshukuru hadi sasa ni kwamba afya yake imeimarika kutokana na shinikizo la Rais Jakaya Kikwete ambaye aliagiza Serikali kumpa kipaumbele wakati wote akiwa nchini na India hatua ambayo imemwezesha kufika hapo alipo.

Mtaalamu auzungumzia
Mtaalamu wa afya ambaye hakutaka kutajwa gazetini alisema ugonjwa huo wa ‘Popular Scleroderma’ unasababishwa na chembechembe hai nyeupe kushambulia kitu kigeni kilichoingia kwenye mwili na kusababisha magonjwa ya ngozi.

Alisema chembechembe hizo zinaweza kusababisha ngozi ya mwili kuharibika… “Ni magonjwa yanayosababishwa na chembechembe hai nyeupe kujikataa zenyewe na kusababisha ugonjwa wa ngozi na mifupa.”

Pia Soma:
- Mwakyembe ndani ya kanisa la Gwajima; ashukuru kwa maombi akiri kulishwa sumu!

- Samwel Sitta asisitiza: Dkt. Mwakyembe kalishwa sumu, asema kuna polisi majambazi

- Siri ya waraka wa Mwakyembe yafichuka; Kisa ni kifo cha ghafla cha mhudumu ofisini kwake

- Dkt. Mwakyembe mambo mazito: Ripoti ya ugonjwa wake yaivuruga Serikali

- Kumbe Polisi na Serikali waongo!? Walisema Mwakyembe hakupewa sumu, leo Magufuli anasema alipewa sumu ili wamuue cha ajabu hawajakamatwa
 
Hii ni kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari mchana wa leo. katika maelezo yake, DCI anasema kwamba kutokana na uchunguzi wa kipolisi ulioshirikisha wizara ya afya, hakuna ushahidi juu ya hilo.
Taarifa za kiinteljensia!!!
 
niliwai kuwaza kwamba wanaweza bisha kama watakuwa na ushahidi wa daktari kwamba jamaa anaumwa ugonjwa mwingine, nadhani mpaka wamekataa basi ushahidi watakuwa nao, Mwakyembe ndio imetoka tena, either huwe nao watunze wanachojuwa ama wakane wamwage kila kitu. siasa kweli ni mchezo mchafu.
 
Hilo ni jibu ambalo nilitegemea serikali ingetoa, katika hali ya kawaida hawawezi kukubali hat akama ni kweli alilishwa sumu. God knows
 
Mkuu Pasco,

Nilitegemea ungesema hivyo hasa kwakuwa mhusika mkuu ni Rais wako mtarajiwa 2015 ingawa alama za nyakati zinazidi kumtenga.


Nadhani huu ndio ikweli wenyewe!. Kibarua sasa kimebaki kwa Mhe. Mwakyembe mwenyewe ku disclose anaumwa nini!.

Get well soon Mwalimu Mwakiyembe na achana na michezo michafu, rudi darasani ukaiendeleze fani ya kufinyanga wakombozi wa mahakamani.
 
Kama Hiyo ndiyo taarifa ya kipolisi basi either Samweli sita ajiuzuru uwazili kwa uzushi ama aje mbele ya vyombo vya habari na kuweka wazi ushahidi wake na kuwaumbua polisi.

ni mtizamo wangu tu!
 
Jamaa atakuwa alikula sumu.elewa kiswahili alikula sumu hivyo hakulishwa sumu huyo Disihai Kanumba angesema hivo tungemwelewa kibongobongo.

senzi wakina 6 muache kulalama sasa au na nyie kodini private dic achunguze
 
Hii ni kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari mchana wa leo. katika maelezo yake, DCI anasema kwamba kutokana na uchunguzi wa kipolisi ulioshirikisha wizara ya afya, hakuna ushahidi juu ya hilo.
Hili si la ajabu kwa mtu mwenye uchambuzi na utambuzi wa hali ya mambo yanayoendelea tangu kiongozi mkuu wa nchi alipochaguliwa kwa ushabiki wa kiwango cha mpira wa miguu.
Waliompigia kampeni waliwekeza na wakati wanaanza kupata ritani kupitia Richmond,meremeta na madudu mengine akina Mwakyembe wakapiga kelele za kuamsha wenye mali.
Kwa bahati mbaya wezi waliwanyamazisha kwa ahadi ya mgao kidogo lakini kumbe ulikuwa ni mtego wa kuwamaliza bila wao kujitambua na hali sasa ndiyo hivyo.Ila cha ajabu baadhi yao sasa wanapita Makanisani na Miskitini ambako hatujui kama wanatubu dhambi zao.
 
kwa hiyo wanataka kutuambia kwamba ,gonjwa hajuiamegua nini mbona wakuwa waajabu sana kweli bongo hadi tujekuendelea yahitaji moyo sana tena wa kikatili..
 
Back
Top Bottom