Tatizo lake nadhani alikuwa anasema sana na kuitetea serikali lakini hakufikiria kuiba, angeiba asinge omba msaada wa serikali angejitibia mwenyewe....
Alimpiga makofi mtendaji mmoja kule Mbarali...labda haya ndio malipo yenyewe...si aliolewa na kaka wa JK huyu?Na mbona Sheikh wa CCM hamsaidii ?
2006-10-13 08:45:49
Na Nico Mwaibale , PST Mbarali
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, Bi. Hawa Ngulume, amemzaba kibao usoni, Mwenyekiti wa Wakulima wa Kijiji cha Kapunga baada ya wakulima hao kuuzuia msafara wa Kamati ya Bunge ya Kilimo na Ardhi.
Baadhi ya wabunge wa Kamati hiyo waliofuatana na Bi.Ngulume ni Bw. Fred Mpendazoe Tungu(Kishapu- CCM), Mwadini Jecha(Wete- CUF), Bw. Castor Ligalama (Kilombero- CCM) na Shally Raymond( Viti Maalum- CCM).
Wananchi hao waliuzuia msafara wa kamati hiyo, wakitaka wapewe ufumbuzi wa manyanyaso, waliyodai kuyapata kutoka kwa mwekezaji kampuni ya Export Trading Limited na kuwaondoa kwenye makazi yao.
Kitendo hicho kilisababisha mvutano mkubwa kati ya wakulima hao na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Bi. Hawa Ngulume.?
Mvutano huo ulidumu kwa takriban dakika 10, ndipo Bi. Ngulume alipopandwa na jazba na kumzaba kibao cha usoni Mwenyekiti wa Wakulima hao, Bw. Ofred Mkemwa.
Mbali na kumnasa kibao Mwenyekiti huyo pia Bi. Ngulume, aliwaniga kabali baadhi ya wananchi waliokuwa kimbelembele katika kufunga barabara hiyo, wakitaka kuzungumza na Wabunge wa Kamati hiyo.
Kwa mujibu wa wananchi hao, kampuni hiyo ya Export Trading Ltd, imewazuia kutumia mfereji wa maji, waliokuwa wakiutumia kwa matumizi mbalimbali ya nyumbani na kumwagilia mashamba.
Walisema kitendo cha mwekezaji huyo ni kinyume na maelezo yaliyotolewa awali na viongozi wa Serikali, ambao walisema mwekezaji huyo atawasaidia wananchi na wakulima wadogo wanaoishi karibu na shamba lake.
Waliongeza kuwa mwekezaji huyo amewafukuza walimu wa Shule ya Msingi Kapunga kwenye nyumba walizokuwa wakiishi, zilizopo ndani ya shamba lake.
Walisema mwekezaji huyo ametaka walimu hao waende wakatafute makazi mengine, nje ya eneo la shamba, licha ya kwamba shule hiyo ni ya Serikali, ambayo ilijengwa kwa ajili ya watoto wa watumishi wa shamba hilo na wananchi wa jirani.?
Juhudi za Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Christopher Chizza za kujaribu kuwasihi wananchi hao kutulia, ziligonga mwamba kutokana na wananchi kupandisha jazba.
Hali hiyo pia ilimfanya Mkuu huyo wa Wilaya, kuwafokea na kuwasukuma wananchi hao wakati wakizuia njia ili Wabunge wateremke na kuzungumza nao.?
Katika kikao cha majumuisho kilichofanyika kwenye ukumbi wa shamba hilo, Bi. Ngulume aliwaeleza Wabunge hao kuwa, wasiwe na wasiwasi na maneno ya wananchi kwa kuwa yote ni majungu ya kupikwa na baadhi ya watu na yasiyokuwa na ukweli wowote.?
SOURCE: Nipashe
malipo ya Mungu ni hapahapa duniani,wakati ananguvu alikuwa anatoa maneno machafu mdomoni hakujua siku moja ataijua taabu,Eeeeeeeeeeee Mungu libarikiwe jina lako.
Wewe ni Mungu wa Kisasi.AMEN
Kagemuro,
Chembe ndogo tu ya utu inahitajika. Umeenda mbali mno. Mungu si wa kisasi ni mwingi wa huruma please!
DC wa zamani hoi kitandani Send to a friend Monday, 08 November 2010 01:13 0diggsdigg
Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbalali, Mkoani Iringa Hawa Ngurume, akizungumza na waandishi wa habari wa gazeti hili, nyumbani kwake Goba Kinzidi, Dar es Salaama jana, kuhusu maradhi ya figo yanayomsumbua. Picha na Venance Nestory
Raymond Kaminyoge
ALIYEKUWA mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Hawa Ngulume yuko katika hali mbaya nyumbani kwake, Goba Kinzudi jijini Dar es Salaam akisumbuliwa na ugonjwa wa vichomi na mapafu.
"Nimeona nitumie chombo cha habari kufikisha ujumbe (wa ugonjwa) kabla sijafa," alisema mkuu huyo wa zamani wa alipoongea na Mwananchi.
Akizungumza na Mwananchi nyumbani kwake jana, Ngulume alisema kwa miezi mitatu sasa yuko hoi na hawezi kutembea bila kusaidiwa na hivyo anaiomba serikali imsaidie aweze kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Alisema ameamua kutumia gazeti hili kufikisha ujumbe kwa serikali na CCM kuhusu maradhi yanayomsumbua baada ya njia nyingine kushindikana.
"Nilipeleka taarifa kwnye chama changu kwamba ninaumwa nahitaji msaada, lakini sikujibiwa; pia nimefanya juhudi za kutaka kumwona Waziri Mkuu ili anisaidie, lakini juhudi hazikuzaa matunda. Nimeona nitumie chombo cha habari kufikisha ujumbe kabla sijafa," alisema.
Ngulume, ambaye ni kada maarufu wa CCM aliyetumikia nafasi ya ukuu wa wilaya kwa miaka 18, alisema maradhi hayo yalianza kumsumbua baada ya kumalizika kwa mchakato wa kura za maoni za chama hicho.
Alisema aliomba ridhaa ya chama hicho kimsimamishe kuwa mgombea ubunge katika Jimbo la Singida Mjini.
"Katika mchakato ule Mohammed Dewji alishinda, na mimi nikawa mshindi wa pili. Niliporudi Dar es Salaam nikaanza kujiandaa kwenda kumpigia debe mshindi kama ulivyo utaratibu wa chama chetu, ndipo nikaanza kuumwa ghafla," alisema.
Mkuu huyo wa zamani wa wilaya ambaye amewahi kushika wadhifa huo kwenye wilaya mbalimbali zikiwemo za Bagamoyo, Ilala na Kibaha, alisema amekuwa akitibiwa katika hospitali za Lugalo, IMTU na Ocean Road
"Kuna kipimo ambacho nilitakiwa kuwekewa kwenye kinywa katika Hospitali ya Ocean Road ili kiweze kubaini kama kwenye mapafu kuna maji au la, lakini ilishindikana kwa sababu ya kukosa pumzi, na hawana kipimo cha aina nyingine," alisema.
Alishauriwa kwamba aendde India ambako kuna vipimo vya aina nyingi ambavyo havihitaji kuwekwa katika kinywa na kwamba vipimo hivyo vingemfaa kutokana na matatizo yake ya pumzi.
Alisema katika kuhangaika alifika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, lakini cha kushangaza alikaa kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 11.00 jioni bila kuhudumiwa.
"Ndipo mtu mmoja anayenifahamu aliyekuwa akipita nilipoketi, akanisalimia kwa kuniita mheshimiwa. Muuguzi mmoja jina ninalihifadhi akaja kutaka kunihudumia, nikamwambia ina maana siwezi kupata huduma hadi niwe mheshimiwa, nikaondoka kwa hasira," alisema.
Alisema baada ya kutelekezwa na kunyanyapaliwa Muhimbili, amekuwa akipata matibabu kwenye hospitali za binafsi kwa ajili ya kutuliza maumivu.
"Maumivu ninayoyapata ni makali sana, nina vichomi utadhani kuna msumemo unaokata viungo vyangu ndani ya tumbo. Ninalia usiku kuchwa kwa maumivu, wanaonisaidia ni majirani tu ambao hufika kila mara kunijulia hali," alisema.
source:mwananchi
hili limenishtua ..lakini hii ndio picha halisi