DC nusura awalize madiwani wa CCM

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,781
5,205
DC nusra awalize madiwani wa CCM

na Victor Eliud, Geita
MKUU wa Wilaya ya Nyang'hwale, Ibrahimu Marwa, nusura awatoe machozi baadhi ya madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kugomea hoja zao za kutaka daktari wa mifugo wa Wilaya hiyo, atimuliwe kwa madai ya kufunga minada yote ya mifugo.


Daktari huyo, Thobias Kiputa, alifunga minada hiyo inayodaiwa kuwa chini ya uzabuni wa baadhi ya madiwani na watendaji wa umma, baada ya kuibuka kwa ugonjwa wa miguu na midomo mwanzoni mwa Mei mwaka huu, wilayani Geita na Nyang'hwale.


Kufuatia hali hiyo madiwani hao walimtaka mkuu huyo wa wilaya kuagiza minada hiyo kufunguliwa mara moja ikiwa ni pamoja na kumwajibisha daktari huyo kwa walichodai hakutenda haki hasa ikizingatia kuwa wakazi wa maeneo hayo wanategemea kuendesha maisha yao kwa kuuza mifugo.


Hoja ya kutaka daktari huyo aondolewe kwenye wilaya hiyo ilianzishwa na Diwani wa Kata ya Nyijundu, Jackob Nyanda, ambaye alimtaka mkuu huyo wa wilaya kumwajibisha kabla wao hawajamkataa kwenye vikao vyao.


"Mkuu hapa Nyang'hwale minada yote ya mifugo imefungwa na daktari wa mifugo kwa masilahi yake binafsi na sasa wananchi wanashindwa kuendesha maisha yao kwa kukosa kipato, maana wengi hutegemea kuuza mifugo, hivyo tunakuomba kabla sisi hatujamkataa, uagize afungue minada na umwajibishe mara moja," alisema na kuungwa mkono na wenzake.


Hata hivyo katika hali ambayo hawakuitegemea, baada ya kusimama kujibu hoja zao, mkuu huyo aligeuka mbogo ambapo mbali na kupinga hoja hiyo aliwataka madiwani hao kutochanganya siasa na kazi za kitaalamu iwapo wanataka kuwaletea wananchi maendeleo.


"Ndugu zangu nimewasikia na wote madiwani karibu watano mliosimama mmezungumzia kuhusu daktari kufunga minada na mnataka serikali imwajibishe kabla ninyi hamjamkataa kwenye vikao vyenu. Ninachotaka kuwaeleza ni kwamba nchi hii haiendeshwi hivyo," alisema.


Alisema ifike mahala siasa ibaki kuwa siasa na masuala ya kitaalamu waachiwe wataalamu, vinginevyo watamfukuza kila mtu wanayetaka afanye kazi kisiasa na kuacha kutekeleza majukumu yake kama taaluma yake inavyomuelekeza.


Mkuu huyo wa wilaya alikuwa akizungumza na watendaji wa kata na vijiji, madiwani pamoja na viongozi wa dini katika wilaya hiyo kwa ajili ya kuweka mikakati ya kuijenga wilaya hiyo mpya ili kuwaletea wananchi maendeleo.


 
Kama wana uhakika kwamba huyo daktari amefunga minada kwa sababu binafsi basi wakajenge hoja kwenye baraza la madiwani na watoe tamko la kumkataa.
Lakini kama wanatafuta kumharibia kazi kwa chuki zao binafsi watambue kwamba laana itawatafuna.
 
Huyu Ibrahim Marwa ni mtu jasiri sana toka enzi zake akiwa mbunge wa Musoma Mjini; it was very unfortunate that he lost during that election!! He is who I can call a progressive leader, sio mnafiki kama magamba wengine.
 
Back
Top Bottom