DC Mbozi aingilia kati sakata la walimu

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
DC Mbozi aingilia kati sakata la walimu


na Moses Ng'wat, Mbeya


amka2.gif
HATIMAYE sakata la walimu 12 wa Shule ya Msingi Chindi iliyoko wilayani Mbozi kuacha kazi kwa madai ya hofu ya kufanyiwa ushirikina limechukua sura mpya, baada ya mkuu wa wilaya hiyo, Gabriel Kimoro, kuamua kuitisha mkutano wa hadhara kati ya wazazi na viongozi wa mila (machifu). Akizungumza kwa njia ya simu kutoka wilayani Mbozi, Kimolo alisema lengo la mkutano huo ni kutaka kujua kwa undani tatizo hilo kwa kuwa licha ya kuleta hofu kwa watumishi wa umma, vitendo hivyo vinaweza kusababisha pia uvunjifu wa amani ndani ya jamii.
Alisema mkutano huo unatarajiwa kufanyika leo Desemba 28 katika ofisi za mtendaji wa kata ya Msangano ambapo uongozi wa elimu wilaya na kata utatoa taarifa ya sakata la walimu hao kuacha kazi na baada ya hapo wazazi wanaotupiwa lawama ya kuhusika na vitendo watatoa taarifa zao.
Alisema licha ya serikali kutoamini mambo ya ushirikina, masuala hayo yatajadiriwa kwa muongozo maalumu bila kuhatarisha usalama wa upande wowote; hata hivyo serikali bado inasubiri majibu ya kitaalamu kutoka kwa madaktari wanaowatibu walimu wawili waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya Vwawa.
Habari kutoka shuleni hapo iliyoko kata ya msangano na kuthibitishwa na diwani wa kata hiyo, Omary Sinkara, zinaeleza kuwa walimu hao wameondoka shuleni hapo katika kipindi cha miezi saba.
Mmoja wa waathirika wa vituko hivyo mwalimu Elia Ngaya ambaye ni miongoni mwa walimu walioamua kuacha kazi baada ya kufanyiwa vitendo hivyo vya ushirikina alisema tatizo hilo limedumu kwa zaidi ya mwaka mmoja licha ya wao kutoa taarifa kwa uongozi wa wilaya ya Mbozi.
Ngaya alisema kuwa wanapokuwa katika mazingira ya shule hupokea vitisho kutoka kwa baadhi ya wakazi wa kata hiyo hasa inapotokea kutoa adhabu kwa wanafunzi, miongoni mwa matatizo ni kuanguka na kupoteza fahamu, kujisikia vibaya wakati mwingine kujikuta macho yakipata giza wakiwa wanafundisha darasani.
Kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Vwawa, Dk. Nicolaus Mbilinyi ,alikiri kupokea walimu wawili ambao wamelazwa hapo na majibu ya vipimo vyao bado yanafanyiwa uchunguzi.
Aliwataja walimu hao kuwa ni Betty Chalamila na Levis Simkonda ambao wote wawili walifikishwa hospitalini hapo wakiwa wamepoteza fahamu na kwa muda mwingi wameonekana kuweweseka.
 
Alisema licha ya serikali kutoamini mambo ya ushirikina, masuala hayo yatajadiriwa kwa muongozo maalumu bila kuhatarisha usalama wa upande wowote; hata hivyo serikali bado inasubiri majibu ya kitaalamu kutoka kwa madaktari wanaowatibu walimu wawili waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya Vwawa.
Kama kweli serikali haiamini ushirikina sasa vikao hivyo ni vya nini?

let us be real and frank with each other that the government is under the leash of covens, witch-doctors...................and seance.......
 
Back
Top Bottom