DC Geita amtishia maisha mwandishi wa Tanzania Daima

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Nimeikuta hii nikaona niwashushie wadau hapa. Inaonyesha Ma-DC wa JK wana ka-ugonjwa kichwani maana alianza yule wa Korogwe kumtusi mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya.

DC amtishia mwandishi

MKUU wa Wilaya (DC) ya Geita, Manzie Omari, ametangaza kupambana kufa na kupona na mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, Victor Eliud, kwa madai ya kumchafua.

Pia, amemtishia maisha mwandishi huyo akisema atakiona cha moto ikiwa ni pamoja na kumfikisha mahakamani kama hatakoma kile alichokiita kuandikwa vibaya katika baadhi ya tuhuma zinazomkabili.

Mkuu huyo wa wilaya alitoa kauli hiyo siku chache baada ya gazeti la Tanzania Daima kuchapisha habari iliyokuwa na kichwa kisemacho “CUF wamshitaki DC kwa RC”, ikinukuu barua ya chama hicho kwenda kwa RC Magalula kuelezea namna ya utawala wa mkuu huyo wa wilaya ulivyo wa kibabaishaji, hivyo yeye kusema ililenga kumchafua.

Katika mazungumzo ya njia ya simu Agosti 23 mwaka huu, yaliyodumu kwa zaidi ya dakika 20, mkuu huyo wa wilaya hakutaka kumpa nafasi ya kuzungumza mwandishi huyo isipokuwa kumshambulia moja kwa moja.

“Hivi wewe Victor unanitafuta nini? Unadiriki kutumia kalamu yako kunichafua siyo? Unatumiwa na huyo kiongozi wa CUF kunichafua mimi. Nataka kukueleza nimekuwa DC kwa muda mrefu wala sikuanzia hapa (Geita). Mwambie huyo Malugu kwamba ofisi yangu haina muda wa kujibu barua zake.... “Na kama huyo Malugu ana ndoto za kuwa DC, mwambie hataupata hadi anaingia kaburini. Hakuna rais wa kumteua akae akijua,” alisema.

Mbali ya hayo, DC huyo alimweleza mwandishi huyo kuwa kuanzia sasa, ni adui yake na kwamba hataki kushirikiana naye kwa namna yoyote ile.


Source: wavuti - wavuti
 
Kila mmoja anayo himaya yake. Je wewe unajua himaya yako? Kama ndiyo, je unaweza kuitetea.
Mimi sina kitu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom