DC Bukoba aamuru walimu wachapwe mboko!

huyu DC anapaswa kurejeshwa kazini mara moja haya ndo majembe tunayataka.
 
Hata kwa kamba hujanichapa fimbo....sheria ipi inayoamuru nichapwe viboko.

Kana umeona nimefelisha watoto fata procedure za utumishi wa umma kuniadhibu na sio viboko.
 
nigefurahi kama angekuwa amewachapa wazazi wa hao watoto wa hizo shule maana mzazi ni number moja katika kuleta maendeleo ya mototo na shule
 
Nimesoma kwenye gazeti la mwananchi. Kuna walimu 32 wamechapwa. Mkuu wa wilaya aamuru polisi kucharaza bakora walimu 32. Ni kutokana na matokeo mabaya ya mtihani darasa la saba. MKUU wa Wilaya ya Bukoba, Albert Mnali aliamuru polisi mmoja kuwachapa viboko walimu katika shule tatu za msingi zilizo Bukoba, kutokana na wilaya hiyo kuwa ya mwisho katika matokeo ya darasa la saba.

Jamani tumefika huko?
Nimemkumbuka shujaa wangu huyu. Hii nchi watu wanalala sana. Uko wapi Mzee Mnali??
 
Kuna watu wengi mtaani wanadai aliyewacharaza walimu Bukoba ni MR PM wa sasa! Tafadhali watu warejee huu uzi kupata ukweli wa aliyewacharaza walimu
 
Kuna watu wengi mtaani wanadai aliyewacharaza walimu Bukoba ni MR PM wa sasa! Tafadhali watu warejee huu uzi kupata ukweli wa aliyewacharaza walimu
Sio PM ila naye alikuwa wa kusini.
Yule anafaa kurudishwa kwenye system. Anaweza kwenda sawa Na spidi ya Magufuli
 
Albert mnali, ndiye DC aliyecharaza walimu bakora huko bukoba.
Kwa sasa ni Mwenyekiti Wa CCM mkoa wa rukwa.
 
Lakini wale jamaa si walilipwa fidia na kuhamishwa juu baada ya kushitaki mahakamani?
Awalipe nani? Wale walimu walikuwa wakifika shule wanasaini register kisha wanaondoka kwenda kufanya biashara ya bodaboda...wkt huo bodaboda ndo zimeingia sokoni na zinalipa..
 
As a leader you have to use simple convert techniques to line up the ruled indivuduals to the right amalgamated channels besides the forces acts which may results the societies repellants.By the way force is not rule.
 
Back
Top Bottom