Elections 2010 DC atokwa machozi kukosa kuteuliwa Ugombea Ubunge CCM?!

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,275
24,141
Samson Chacha, Tarime

KATIKA hali isiyo ya kawaida, mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Christopher Ryoba Kangoye ambaye alikuwa mmoja wa wagombea ubunge wa CCM kwenye Jimbo la Tarime, alijikuta akiangua kilio na wafuasi wake.

Tukio hilo lilitokea Jumamosi kwenye ukumbi wa CCM wilayani Tarime mkoani Mara baada ya mkuu huyo kuomba kuvunja makundi ndani ya chama hicho na kusababisha ukumbi huo kutawaliwa na vilio mithili ya kanisa la uamsho.


Kangoye alikuwa ameitwa katika kikao cha kamati ya siasa ya chama hicho ambacho kilivunjika baada ya tukio hilo.


Kikao hicho cha kamati ya Siasa ya CCM wilaya ya Tarime kilichofanyika juzi mchana chini ya uenyekiti wa Rashid Bogomba, kilihudhuriwa na viongozi kadhaa akiwemo katibu wa wilaya, Felex Manyama, mwenyekiti wazazi Samwel Magabe, Mchumi John Gimunta na wajumbe wengine wakiwemo wapambe zaidi ya 40 wa Kangoye.


Ajenda ya kikao hicho ilikuwa ni mkuu huyo wa wilaya kuvunja kundi lake ambalo linadaiwa kuwa ndilo limekuwa likikidhoofisha chama pale maslahi yake yanapokuwa hayatekelezwi.



Baada ya mwenyekiti wa kikao hicho Bogomba kufungua kikao, wajumbe walikokuwemo walitaka baadhi ya wajumbe watolewe nje, akiwemo katibu msaidizi wa wilaya, Adirian Moris, Mchumi John Gimunta, Maxmilian Matinde na mgombea aliyeshinda kwenye kura za maoni, Nyambari Nyangwine.


Hata hivyo, Nyangwine alishasoma alama za nyakati mapema na kukaa kwenye chumba kingine cha jengo hilo, huku wajumbe waliondolewa wakidai kuwa kikao hicho hakitafanikiwa kwa sababu pande zote zilitakiwa kushiriki katika kumaliza tofauti.


Baadayue Bogomba alimpa nafasi mkuu huyo wa wilaya kuzungumza ili awaombe wafuasi wake kuvunja makundi na kujiunga na wenzao katika kampeni zinazoendelea.


Kangoye alianza kwa kusema: "Ndugu zangu, nawaombeni muipe kura CCM ingawa tulionewa..." Alianza kutokwa machozi hali iliyofanya wafuasi wake nao kuangua kilio na kusababisha hali ya kutoeleweka kwenye chumba hicho, huku watu waliokuwa nje wakidai kuwa ukumbi huo wa CCM umegeuka kanisa la walokole.



Kutokana na hali hiyo ya vilio, ilimlazimu Bogomba kuahirisha kikao na wafuasi hao kutoka nje huku wakijifuta machozi na kuondoka maeneo hayo ya ofisi hiyo.


Wanachama wa CCM wilayani humo waliuomba uongozi wa kitaifa kuingilia kati tofauti zinazoonekana kutomalizika kwenye jimbo hilo, ambalo lilikuwa chini ya Chadema tangu mwaka 2005



Source: Mwananchi
 
akiyanani ccm wanachekesha hadi basi ..... wakati mwingine utadhani unasoma vitabu vya comed
 
Hapo hakuna sulusu, CCM waachane na jimbo la Tarime. Jamaa wa Tarime ni ngangari, ndio maana uongozi wa CCM wilaya walishindwa kutangaza matokeo ya kura za maoni. Kwa maneno mengine hata ukienda uongozi wa CCM Taifa hakuna mwenye uwezo wa kumaliza huo mpasuko.
 
Huko Mara kuna mambo na ndio maana Chambiri ameona ahamie Babati!! Sijui Gachuma atamuachia apumue au atamfuata hata huko kwa wambulu!!
 
Back
Top Bottom