Dawa.

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
49,016
54,299
Wana JF na Ma dr nawasalimu wote.

Napenda kufahamishwa kuhusu baadhi ya dawa mfano Ampiclox umeandikiwa 1x3 ikiwa na maana asubuhi kidonge kimoja,mchana kimoja,na jioni kimoja.Kuna dawa za maji kama Cophydrex nayo unaandikiwa kijiko 1x3 inakuwa kama hiyo dawa ya kwanza kuitaja.

Swali langu kwa ma dr na wataalam usiku wa huwezi endelea na dozi mpaka asubuhi?Yaani jioni ukinywa saa sita usiku unakunywa tena mpaka dozi itakapokwisha.
 
Wana JF na Ma dr nawasalimu wote. Napenda kufahamishwa kuhusu baadhi ya dawa mfano Ampiclox umeandikiwa 1x3 ikiwa na maana asubuhi kidonge kimoja,mchana kimoja,na jioni kimoja.Kuna dawa za maji kama Cophydrex nayo unaandikiwa kijiko 1x3 inakuwa kama hiyo dawa ya kwanza kuitaja. Swali langu kwa ma dr na wataalam usiku wa huwezi endelea na dozi mpaka asubuhi?Yaani jioni ukinywa saa sita usiku unakunywa tena mpaka dozi itakapokwisha.

Hii ina maana gawa siku ya masaa 24 kwa tatu na utapata masaa nane!! Kwa mantiki hii kama utaanza saa 12 asubuhi, then saa 8 mchana, then saa 4 usiku ambao ni muda mzuri kwa dawa ya TDS (Three times a Day).

Kwa mantiki hiyo if yiu choose kuanza saa 2 asubuhi then 2nd dose ni saa 10, 3rd dose saa 6 usiku kama utakuwa macho. Ndo maana nyindi za TDS anza either mchana saa 8 au saa 4 usiku, etc!! Huu ndiyo utaratibu kwa antibiotics nyingi na zingatia masaa otherwise ugonjwa unakuwa unatibika nusu nusu na mwisho waweza kuwa chronic.
 
Mkuu Kennedy,salaam
Unaaanisha kuwa baada ya kunywa jioni(mara ya tatu) uendelee kuitumia tena usiku?

Ndiyo namaanisha hivyo Mkuu,usiku unaweza endelea na dawa hata ukaweka alarm clock ikuamshe,napenda kujua utaratibu huo unakubalika kitaalam?
 
Ndiyo namaanisha hivyo Mkuu,usiku unaweza endelea na dawa hata ukaweka alarm clock ikuamshe,napenda kujua utaratibu huo unakubalika kitaalam?

Mkuu Kennedy,

Siku ina masaa 24, na dawa(dawa nyingi) daktari anaandika kulingana na uwepo wa masaa 24 katika siku.Hii ikiwa na maana anafanya hesabu(KULINGANA NA DOZI INAYOHITAJIKA) yaani dawa mtumiaji atumie kila baada ya masaa 24, au masaa 12, au 8 au 6...Hivyo basi hufanya hivi;

a)1x1 (Humaanisha kila baada ya masaa 24)
b)1x2 (kila baada ya masaa 12)
c)1x3 (kila baada ya masaa 8)
d)1x4 (kila baada ya masaa 6)

Sasa kwanini daktari anakuamvia kunywa mara tatu? anamaanisha alifanya hesabu katika masaa 24 ya siku, dawa aliyokupa unatakiwa kutumia kila baada ya masaa 8..yaani masaa ya siku nzima ukigawanya kwa masaa ya kutumia dawa YAANI 24/8= 3...so kwa wagonjwa wengine(NI NGUMU kuelewa au kukumbuka) so unapomueleza tumia asb, mchana na jioni ni nafuu.

KUJIBU SWALI LAKO:
Si vyema kutumia zaidi ya dozi(kumvuka kila dawa ina madhara)..hivyo unaweza kuathiriwa na madhara ya dawa, ongezeko la dawa mwilini, n.k

Sijui kama umeelewa mkuu?
 
Nashukuru mkuu.
 
Back
Top Bottom