Ni dawa gani ya usingizi wanayoitumia wezi kupuliza madirishani?

Kupitia huu uzi na wachangiaji wa mada wanavyodadavu wengine tunajifunza jinsi ya kujihami na wezi. Kwa mfano, mimi nimejifunza mbinu ya kuacha maji wazi ili kujihami na wezi wanaotumia Kloroform wengine tulikuwa hatuijui.
Exactly! Hii ndiyo nguvu ya akili kubwa & positive minded people. Siyo wale ambao wanaangalia negatives tu eti oh wezi watapata mbinu....
 
Kweli mkuu. Watu wapo tayari kuyumia gharama yoyote kuweka alarm kwenye gari lakini uhai wake haujali kabisa. Maana mwizi kuingia ngani ukiwa fofo nisawa na kumkabidhi uhai wako maana anaweza kuganya chochote na akatokomea bila hata kuacha alama. Tubadilikeni jamani, zipo alarm za bei chee kabisa. Ukigusa tuu ni kama king'ora cha ambulance au gari za police. Hadi majirani wataamka
Za bei chee kama kiasi gani?
 
Hii ya kutolea mafuta pikipiki/gari usiku alikuwa ananikumbusha sana mzee ila sikujua maana yake hadi siku majambazi walipotutembelea usiku wakata nyaya ili wawashe kitu waondoke ikagoma wese hamna na ndo ikawa salimika ya huo mchuma ilikuwa 1997
Yaani Ni kwikwi babuu
 
Nilikuwa nawaza kwa sauti hii mbinu ya maji...
Lakini nikawa najiuliza kuwa litaulizwa swali uhusiano uliopo baina ya hiyo dawa na maji, kwa nini maji yakiwepo haiwezi kufanya kazi!!

Cloroform ni solube kwy maji kwa iyo inapoteza ile concentration yake eventually haiwezi kukuletea madhara yake ya usingizi,kutosikia,nk! Huwa ina harufu flan nzuri ivi na ni nyepesi sana kuivuta km hewa! Inatokana na mchanganyiko wa chlorine na methane!nchi za wenzetu huinunui kienyeji mpk uwe na vibali kutoka kwy malaka husika za dawa na chakula etc
 
Sio mwanamke tu mkuu hata kidume wanaweza legeza marinda.ukiona wamesepa na zagazaga na wewe wamekuacha salama unscathed ni jambo la kushukuru mungu.
aisee inabd uwashukulu maana unakuwa kama umekufaa
 
Tehe tehe tehe hayo majamaa yaliyokunywa mpaka chai ni 'noma', ukweli lazima tuyapongeze kwa umafia walioufanya kwa sababu huwezi kwenda kwenye nyumba ya mtu kuiba halafu ukanywa mpaka chai ni 'noma'.

Nakumbuka wakati naishi Kunduchi, jirani yetu mmoja alikuwa mfugaji wa bata. Alikuwa na bata wengi kama utitiri. Kumbe basi wazee wa kazi siku nyingi walikuwa wanawamezea mate wale bata.

Siku ya siku wazee wa kazi wakatia 'maguu', nafikiri walitumia hiyo dawa ya usingizi kwa maana siku hiyo usingizi ulikuwa mtamu balaa! Wazee wa kazi kama kawaida yao, wakachukua bata wote hawakuacha hata manyoa...watu tunaamka asubuhi tunakuta banda leupe, dah siku hiyo nilicheka sana kwa sauti ya chini chini kwa sababu wazee wa kazi walikuja na 'kiroliroli'... tuliona tu alama za matairi ya gari, yani wazee wa kazi kwa jeuri walikuja mpaka na gari, ule mngurumo wa gari watu hatukusikia tunakoroma tu, ha ha haa ni 'noma!'
hawakupika supu mkuu wakashushia na viroba?
 
Ipo dawa ya spry pia ipo dawa ya asili yapo majani jina siyajui ila kw macho nawajua hayo majani yakiwa mabichi ukiyapikicha hutoa harusi ya kinyesi basi ukitaji yatumia huyakausha kisha yakikauka mwezi akija huyachoma nnkurusu ule moshi upenyeze ndani yani ukivuta tu ile harusi unakuwa nusu kaput ndani ya masaaa mawili

Ili kuepuka wizi wa namna hii unashauriwa kuwa na maji ndani either kwenye jagi au kikombe maji yawe wazi kwani inasemekana spry yoyote ile au moshi wowote ule ukifulizwa sehemu ambapo maji yapo wazi ile dawa hukimbilia kwenye maji kwanini miye sijui ila nimepata huu uzoefu kwani tuliishi maeneo ambayo wizi wa namna hiyo ulikuwepo mkubwa sana na kina pekee ilikuwa kulala na maji ndani
JF GREAT THINKER

MODS PELEKA HII JUKWA LA INTELLIGENCE ALAFU IWE STICKY.
 
Kaka kuna watu na shunguri zao aisee. Mie nlikuwaga mbishi kama wewe, kuna mzee mtaan aliibiwa bajaj kwake aisee. Wezi walikuja ucku wakafungua get wakaiba bajaj.

Yule mzee hakwenda kushtak hata polisi. Ila baada ya siku kama mbili hivi wale wezi walirudisha bajaj huku wanaikokota.

Yule mzee hakushtuka aliwafungulia geti wakapak bajaj akamwambia mkewe awape naul wakaenda. Hata hawakuguswa wale wezi.

Kuna watu na shughuri zao
upo sawa kabsaa mkuu sio kila mtu anaibiwa kijinga
 
Thubutuuu wameniibia mara mbili Samsung inch 40 na mifeni yangu miwili ikiiunguruma ndani. Yaani siku hizi pamoja na kuweka mlinzi bado nikitaka kulala nabeba Tv naingiza chumbani. Maana kila nikinunua wanakuja kuchukua kama zao, ya pili waliifungua ukutani kabisa.
Siyo siri nawachukia sana wezi, mwaka jana walivunja mlango wakaingia mpaka chumbani kwangu nilipokuwa nimelala na kubeba kila kitu, wakabeba na chupa ilikuwa na chai na maandazi wakasepa nayo
Mnanivunja mbavu jama
 
Ukiibiwa njoo PM nikuunganishe na wataalaam, vifaa vyako utavipata bila shaka.
 
Naona hii ya beseni la maji iko passed
Mkuu kuwa makini na kitu wenye kizungu wanachoita ''myth''. Ni kitu kibaya sana. Mimi nimepitia maelelezo yooote hapa lakini kila nikijaribu kuunganisha kwa kutumia sayansi naona nyota nyota. Kwa mfano chukulia mwizi amekuja na hiyo dawa wanayosema inakufanya ulale. Akaipulizia dirishani. Wewe umeweka maji kwenye karai chini ya dirisha lako. Sasa jiulize: Yale maji yana nguvu ya uvutano ya kuvuta ile dawa ielekee kwenye karai lenye maji na isielekee puani kwako? Katika hali ya kawaida itakimbilia puani kwenye nguvu ya kuvuta au kwenye beseni? Huoni hapa kuna maswali mengi kuliko majibu? Hii ya maji kwenye karai ni hadithi ya kusadikika na mimi sitaiamini kwa namna yoyote. Wengine wamefikia hatua ya kusema wanakuja na chloroform hivyo ukiweka maji yanai-netralize! Kweli mtu aliyesoma chemistry hili linaingia akilini?
 
Back
Top Bottom