Dawa za mapenzi ni kweli?

@mashizo,mi nashukuru sana kwa maelezo yako..yanatia moyo na kufariji sana.
 
Pole sana Kaka, najua kama sio rahisi kukubali matokeo lakini hata ukienda kwa mganga haitokusaidia sababu itakua wewe ndio unae mpenda lakini yeye hakupendi,na raha ya penzi nikupeana umpe na yeye akupe sasa ukiwa unatoa wewe peke yako sio sahihi, na niafadhali amekwambia kistarabu kuliko ungekuta yuko na mwanamme mwengine pengine ingeuma zaidi,jikaze kiume na kubali matokeo fanya hili liwe kama fundisho kwako ili ukija kupenda tena usijimalize kwakupenda, wewe sio wa kwanza kuachwa wala hutokua wa mwisho, jaribu kujishughulisha na kazi zako na Mungu atakupa mwenye kheir na wewe.....
 
niletee sisimizi mwenye mimba,beberu lenye pu....bu moja la kushoto,maji yaliyooshea maiti ya kichanga,mafuta ya simba yaliyochukuliwa sehemu ya maini,mkia wa ng'ombe asiye na nundu,jicho la paka mweusi mwenye baka la njano na bluu kichwani pamoja na panya aliyeshika mimba ikatoka kabla hajazaa,ukinipatia vyote hivyo na jogoo jekundu ndani ya masaa 24 atakuwa amekurudia.Fanya hima jua halija kuchwa.Nakusubiri tandale kwa bi manyau.
 
Bora uyo mpenzi kakwambia ukweli kuliko angekuficha maana hakuna kitu kibaya kama kutokuwa na furaha katika mapenzi, hakuna dawa ya mapenzi maana mtu akipenda kapenda na hisia za mapenzi zikihisha ndo zimeisha hivyoo! kuna waganga wanaodai wanatoa dawa za mapenzi na wao pia wana matatizo katika mahisiano yao vile vile sasa kwa nini wasijitibu wao kwanza.
 
Utapata utapiamlo bure sababu ya mapenzi!Mapenzi hayalazimishwi na nguvu yeyote ile,kuachwa na kuacha ni jambo la kawaida katika mapenzi,,,hata WINNIE na MANDELA Ilifika mahali mmoja akaachwa.Kubali kwamba hayo ndio MAJIBU halisi na yape ruhusa maisha yaendelee kama kawaida.Itakupa tabu kwa muda fulani then uta "recover"Halafu nimeipenda style aliyotumia huyo mpenzio ya kuonyesha hisia zake!Amekuwa direct bila kufichaficha.Hiyo imekupunguzia sana matatizo tofauti na kama angekuwa anafichaficha!Mshukuru sana kwa hilo.
 
Pole ndg,jikaze ucjidhuru kwa lolote na ucjarb hata kumsogelea mganga hakuna suluhsho la kudumu huko,
hata km utafanikiwa kupata dawa ztakuwa kwa mda 2 ni lazma utakosea mashart mwisho utaachwa kwa stail mbovu zaid ya hyo,bnafc namshkuru huyo dada kwakuwa muwaz zaid kwan nik2 kzuri sn.
 
Naweza kukusaidia mkuu. Mimi ni mtaalamu wa tiba mbadala. Huyo binti kama una mawasiliano naye ya simu au ya moja kwa moja ni rahisi tu kumzindika. Fanya jambo moja; mpigie halafu akianza kuongea record sauti yake kwa simu yako. Saa 8 za usiku, amka uchi na hiyo simu yako yenye sauti yake hadi makaburini. Ukifika tafuta kaburi alilozikwa kikongwe kaa juu yake halafu fungulia sauti ya huyo umpendaye azungumze hadi amalize, akimaliza wewe uanze kunuiza jinsi unavyotaka. Halafu uanze safari ya kurudi nyumbani kwako kimya kimya bila kugeuka nyuma. Nakuhakikishia kwamba, si ajabu ukamkuta chumbani kwako akikusubiria.
 
kwanza shukuru, huo ni mwiba. mungu huwa anajibu na utafurahi mwenyewe msahau huyo
 
Achana nae, warembo wengi sana dunia hii, asikupe pressha za bureeeeeeee.
 
sio kila mapenzi lazima yadumu milele au yazalishe ndoa. wengine wapo kwa minajili ya kuburudisha mwili, wengine kuondoa tension za maisha wengine ili kuonekana tu na jamii kwamba naye anayajua mapenzi na anaweza kutoka na wanawake/wanaume wanaovutia machoni.

Kwenye mapenzi kuna kuliwa na kulika. Kwa hili lako ni kama umeliwa, ila yeye amelika. Songa mbele maisha lazima yaendelee, wewe na yeye hamkuzaliwa mapacha, unaweza kuishi maisha mazuri bila ya yeye!

Songa mbele!
 
..eeh,kwa waganga tena?hao lazima wakule na wewe maana dawa zao lazima apake kwenye nyeti yake halafu aiingize kwako!!hakuna mganga mzuri kama YESU!ok,wewe sio wa kwanza kuachwa,watu wanaacha mpk wazazi wao sembuse huyo umekutana nae ukubwani na huna hata undugu nae?acha upya,mapenzi yapo tu
 
dawa zipo.hata mm nnayo ila ya kwangu unapaka kwenye bunduki yako kabla ya kudoo nae...zen uningiza bunduki yako kunako......yaani hata iweje binti hakuachi kamwe......cjuikama utawza wktye ndo hvyo ashakuacha......huo ndo msaada wng kwa leo.
 
Habari?,rejea thread yangu yenye kichwa: JAMANI MAPENZI YATANIMALIZA NISAIDIENI PLS (nimeshndwa kuicopy hapa kwa kuwa natumia simu hvyo yeyote anaweza kunisaidia). Jaman nimembembeleza,nimeomba na kujishusha sana asiniache kwa kuwa nampenda sana lakini imeshindikana na jana kanitumia msg NISAMEHE KWA YOTE WANGU ILA BORA KILA MMOJA AWE UPANDE WAKE nilipomuuliza kwanin?,akajibu,SINA FURAHA KTK RELATION YETU NA NINAOGOPA FURAHA ISIPORUDI NTAKUWA NIMEPOTEZA MUDA WAKO. Kiukweli nimeumia sana,nmeshndwa kula toka jana asbh na sijalala usiku kucha,kiufupi nateseka sana mpaka nimefikiria kujidhuru..nikaona hapana bora nijaribu kwa hawa WAGANGA wa kienyeji pengine watanisaidia kurudisha penzi langu. Jamani hivi kweli dawa hizi zinafaa?,nisaidieni nifanye nini nateketea mwenzenu.

Kweli zinafaa unamfanya mtu anakuwa zezeta niPM nikuonyeshe mganga mzuri si unasikia Libwata?
 
Back
Top Bottom