Dawa za Kuongeza Ufanisi wa Mwanaume Kitandani Zazinduliwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108
2518934.jpg

Thursday, July 16, 2009 6:21 AM
Tatizo la wanaume kuwahi kufika kileleni mapema ambalo huzua hofu kwa wanaume wengi sana duniani kiasi cha wengine kwenda kwa waganga kutafuta tiba limepatiwa ufumbuzi baada ya dawa ambayo inasemekana inaongeza ufanisi mara tatu zaidi kuzinduliwa nchini Ufaransa. Tatizo la wanaume kuwahi kufika kileleni mapema wakati wa kujamiiana ambalo huwatia hofu mamilioni ya wanaume wengi duniani limepatiwa dawa kwa mara ya kwanza.

Tatizo hili huwanyima raha wanaume wengi kwani mwanaume anapowahi kufika kileleni mapema kabla ya mpenzi wake humwacha mwanamke akiwa bado hajafikia hitimisho la raha ya kujamiiana.

Wanaume wenye tatizo hili ili wasiaibike kitandani mbele ya wapenzi wao wamekuwa wakihaha kutafuta dawa za kuwafanya waweze kuwaridhisha wapenzi wao, kuna wanaume wengine hufikia hatua za kwenda kwa waganga kutafuta tiba.

Dawa za kutibu tatizo hilo zimezinduliwa kwenye kongamano la tatu la matibabu ya magonjwa ya jinsia linalofanyika nchini Ufaransa.

Dawa hizo mpya ambazo zimepewa jina la "Priligy" zimetengenezwa kwa kutumia madawa ya Dapoxetine ambayo yamegundulika kuonyesha ufanisi mkubwa katika kuchelewesha mwanaume kufika kileleni mapema.

Wanaume waliotumia dawa hizo wakati wa majaribio ufanisi wao kitandani unasemekana uliongezeka kwa mara tatu zaidi.

Dawa hizo zimethibitishwa rasmi ufanisi wake na vyombo vya afya nchini Austria, Finland, Ujerumani, Italia, Hispania, Sweden na Ureno.

Prof. Jacques Buvat wa taasisi iliyovumbua dawa hizo alisema kuwa dawa zinaweza zikatumiwa na wanaume wenye umri kati ya miaka 18 na 64 na hazina madhara yoyote katika kusimama kwa uume.

Prof Buvat alisema kuwa wanaume wengi hufika kileleni kati ya dakika moja na dakika kumi. " Kwa wastani muda unaokubalika ni kati ya dakika nne na tano, wanaume wanaofika kileleni ndani ya dakika moja au chini ya dakika moja huhesabika wana tatizo la kufika kileleni mapema".

"Tatizo la wanaume kuwahi kufika kileleni mapema huwatokea wanaume wengi zaidi kuliko tatizo la kusimama vyema kwa uume".

"Wanaume wengi huwa hawapendi kuzungumzia tatizo hili na asilimia 40 ya wanaume hutumia pombe kama njia ya kutatua tatizo hilo" alisema.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2518934&&Cat=7
 
Back
Top Bottom