Dawa za kulevya zazua utata Polisi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,266
33,039
Utata umelikumba Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kufuatia dawa za kulevya zenye thamani ya mamilioni ya fedha zilizokamatwa mpaka wa Kasumulu wa Tanzania na Malawi kupungua uzito katika mazingira yanayotia mashaka kutoka

kilo tatuzilizoripotiwa kukamatwa awali na kubakia kilo 1.8 baada ya kusafirishwa toka wilayani Kyela kupelekwa mkoani.

Dawa hizo zilizokamatwa wiki iliyopita wilayani Kyela, askari wa wilaya hiyo waliokamata walitoa taarifa kuwa kiwango walichokamata kilikuwa ni kilo tatu.

Hata hivyo dawa hizo baada ya kusafirishwa kutoka Kyela kupelekwa makao makuu ya ofisi za jeshi la polisi mkoa wa Mbeya zilipopimwa upya ilibainika kuwa ni kilo 1.8 tu.

Kamanda wa kikosi maalum wa kuzuia dawa za kulevya mkoani Mbeya, ASP Francis Mboya, alithibitisha kukamatwa kwa dawa hizo na kutokea utata huo.

Mboya alisema jana kuwa, alipewa taarifa za kukamatwa kwa dawa hizo kutoka kwa viongozi wa jeshi la polisi wilaya ya Kyelakwamba zilikuwa kilo tatu, lakini baada ya kuletwa mkoani na kupimwa upya zilikutwa zilikuwa ni kilo 1.8.
Mboya alisema inawezekana ikawa ni makosa ya kipolisi ya kukisia kiwango walichokamatwa badala ya kupima kwanza.

Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Kyela (OC- CID), Mboya, alisema tayari dawa hizo wameshazikabidhi kwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Mbeya na kueleza sababu zilizopelekea kupungua kwa uzito.

Askari wa jeshi hilo wakiongozwa na Coplo Simon wa wilayani Kyela wiki iliyopita ndio walikamata dawa hizo aina ya Cocain na mtuhumiwa Simon Kairuki kutoka Kenya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi, hakupatikana baada ya katibu muhtasi wake kueleza kuwa bado hajarejea kutoka kwenye mkutano wa maafisa wa Jeshi hilo uliokuwa ukifanyika mjini Moshi.

Hii ni kashfa ya pili kulikumba Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, ambapo mwaka juzi kilo nane za dawa za kulevya ambazo zilikamatwa Novemba 18 mwaka 2010 katika mpaka wa Tunduma mkoani hapa zilidaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha mkoani.




CHANZO: NIPASHE
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom