Wataje au ondoa uchafu jamvini. Akina RACHEL wanateswa sana. Kila mmoja ana haki yake hakuna cha kiongozi wa--------Viongozi wa dini sasa wajisalimisha
*Wakiri kufanya biashara hiyo muda mrefu
*Watoa ushuhuda mbele ya kamati ya maadili
Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi, Zanzibar
VIONGOZI sita wa madhehebu ya dini ambao wanajihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya nchini, wamejitokeza mbele ya Kamati ya Maadili ya Viongozi wa
Dini na Haki za Jamii na kukiri kujihusisha na biashara hiyo kwa muda mrefu sasa.
Ofisa Uhusiano wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Inspekta Mohammed Mhina, amesema baada ya viongozi hao kuhojiwa, waliiomba kamati hiyo kutowataja hadharani au madhebebu yao wakihofia kubezwa.
Akizungumza mwishoni mwa ziara yao visiwani humo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mchungaji William Mwamalanga wa Kanisa la Pentekosti Tanzania, alisema orodha hiyo na wengine 18 wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wanasiasa ambao wanajihusisha na biashara hiyo, itafikishwa kwa Mkuu wa Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Dawa za Kulevya nchi.
Mchungaji Mwamalanga alisema ongezeko la dawa za kulevya nchini pia linazihusu nchi mbalimbali duniani ambapo kamati hiyo itakutana na kamati nyingine kama hizo za nchi za Maziwa Makuu kuzungumzia ufumbuzi wa tatizo hilo.
Mkutano huu pia utapendekeza wabunge wa nchi hizo na Bunge la Afrika ya Mashariki, kutunga sheria za kuwafilisi wale wote waliojilimbikizia mali kutokana na biashara ya dawa za kulevya kwa nchi wanachama, alisema Mchungaji Mwamalanga na kupongeza juhudi za Jeshi la Polisi kukabiliana na ongezeko la dawa hizo.
Akizungumzia kero ya dawa za kulevya visiwani hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, ACP Aziz Juma Mohammed, alisema kuwa jeshi hilo limekuwa likiwakamata wafanyabiashara na watumiaji wa dawa hizo na kuwafikisha mahakamani.
Kamanda Mohammed ametoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali wa usalama, kusaidiana na jeshi hilo kwa kutoa taarifa za wale wanaojihusisha na mtandao wa dawa hizo.
Wiki iliyopita watu wawili wakazi wa Dar es Salaam, walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar kwa nyakati tofauti wakitokea nchini Brazil ambapo kila mmoja alipatikana na kiasi kikubwa cha madawa ya kulevya aina ya Cocaine.