Dawa za kulevya: Viongozi wa dini sasa wajisalimisha; Wakiri kufanya biashara hiyo muda mrefu

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Viongozi wa dini sasa wajisalimisha

*Wakiri kufanya biashara hiyo muda mrefu
*Watoa ushuhuda mbele ya kamati ya maadili

Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi, Zanzibar

VIONGOZI sita wa madhehebu ya dini ambao wanajihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya nchini, wamejitokeza mbele ya Kamati ya Maadili ya Viongozi wa
Dini na Haki za Jamii na kukiri kujihusisha na biashara hiyo kwa muda mrefu sasa.

Ofisa Uhusiano wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Inspekta Mohammed Mhina, amesema baada ya viongozi hao kuhojiwa, waliiomba kamati hiyo kutowataja hadharani au madhebebu yao wakihofia kubezwa.

Akizungumza mwishoni mwa ziara yao visiwani humo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mchungaji William Mwamalanga wa Kanisa la Pentekosti Tanzania, alisema orodha hiyo na wengine 18 wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wanasiasa ambao wanajihusisha na biashara hiyo, itafikishwa kwa Mkuu wa Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Dawa za Kulevya nchi.

Mchungaji Mwamalanga alisema ongezeko la dawa za kulevya nchini pia linazihusu nchi mbalimbali duniani ambapo kamati hiyo itakutana na kamati nyingine kama hizo za nchi za Maziwa Makuu kuzungumzia ufumbuzi wa tatizo hilo.

"Mkutano huu pia utapendekeza wabunge wa nchi hizo na Bunge la Afrika ya Mashariki, kutunga sheria za kuwafilisi wale wote waliojilimbikizia mali kutokana na biashara ya dawa za kulevya kwa nchi wanachama," alisema Mchungaji Mwamalanga na kupongeza juhudi za Jeshi la Polisi kukabiliana na ongezeko la dawa hizo.

Akizungumzia kero ya dawa za kulevya visiwani hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, ACP Aziz Juma Mohammed, alisema kuwa jeshi hilo limekuwa likiwakamata wafanyabiashara na watumiaji wa dawa hizo na kuwafikisha mahakamani.

Kamanda Mohammed ametoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali wa usalama, kusaidiana na jeshi hilo kwa kutoa taarifa za wale wanaojihusisha na mtandao wa dawa hizo.

Wiki iliyopita watu wawili wakazi wa Dar es Salaam, walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar kwa nyakati tofauti wakitokea nchini Brazil ambapo kila mmoja alipatikana na kiasi kikubwa cha madawa ya kulevya aina ya Cocaine.

Well, Wakati wa Nyerere kulikuwa hakuna dini nyingi kama sasa hivi especially PENTECOSTE this is a group of christian religion in which is new in our country and to survive some of the members are involved in those kind of things; but it is not all christian religion, established those established long time ago like Catholics, Lutheran etc - WE HAVE TO BE VERY CAREFULL

Religious factions will go on imposing their will on others unless the decent people connected to them recognize that religion has no place in public policy. They must learn to make their views known without trying to make their views the only alternatives.
 
Ofisa Uhusiano wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Inspekta Mohammed Mhina, amesema baada ya viongozi hao kuhojiwa, waliiomba kamati hiyo kutowataja hadharani au madhebebu yao wakihofia kubezwa.

Hapo kwenye nyekundu ndio tatizo langu mimi yaani wao wako above the law au? Na kweli walikubaliana nao kwa misingi ipi? kwa kutowataja kutalete faida gani katika taifa letu?.

Kweli hatuna Serikali.
 
Litakuwa ni jambo la kusikitisha sana kama kweli hao watu hawatatajwa hadharani.jambo ambalo litafanya vita dhidi ya wazungu waunga kuwa haina maana kabisa.nibora hiyo kamati ifutwe.
 
Ofisa Uhusiano wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Inspekta Mohammed Mhina, amesema baada ya viongozi hao kuhojiwa, waliiomba kamati hiyo kutowataja hadharani au madhebebu yao wakihofia kubezwa. Hapo kwenye nyekundu ndio tatizo langu mimi yaani wao wako above the law au? Na kweli walikubaliana nao kwa misingi ipi? kwa kutowataja kutalete faida gani katika taifa letu?.Kweli hatuna Serikali.
Sasa ukiambiwa hii habari ni ya kutengenezwa na ni yakizusha bado utakataa tu! Kama ndo hivyo basi tunahari ngumu na tete katika taifa letu
 
Sasa ukiambiwa hii habari ni ya kutengenezwa na ni yakizusha bado utakataa tu! Kama ndo hivyo basi tunahari ngumu na tete katika taifa letu
Mmmmhh!! Ina maana hii hbr ni ya ku2ngwa? Humu ndani tumevamii kama hii THREAD ni ya upupu. Ngoja tuwasubiri wadau!
 
hamna kitu hapa wote wanajaribu kuwaaminisha wananchi kauli ya jk, hatutaki siasa hapa hayo maneno ya sijui kuna wabunge, vigogo wa serikali wanahusika na madawa tumeanza kuyasikia miaka 15 iliyopita na halijawahi kutajwa jina, tusipotezeane muda
 
Aisee kumbe hizi habari za viongozi wa dini kijihusisha na madawa ya kulevywa ni za kweli?? Sasa JK alikuwa anaogopa nn kuwataja? Halafu yule kionozi wa dini aliyempinga JK hadharani kwamba awataje la sivyo amejivunjia heshima alikuwa ana maana gani? Kaaazi kwelikweli!!!!
 
Ndiyo maana tunaona Makanisa mengi yanajengwa, shule nyingi za St. zinajengwa; kumbe sasa tunapata ukweli wa hizo hela zinapotoka. Sasa sijui kwa nini hizo shule zao bado zinaitwa Saint!!?
 
Wauza madawa wapo na serikali inawajua lakini mambo yaleyale nchi itatikisika na mkuu wa kaya anaogopa kuwataja. Mkuu wa kaya aliombwa sana na kiongozi mmoja wa dini kwamba awatae la sivyo anajivyunjia heshima yeye aliamua KUJUVUNJIA HESHIMA. Kwa kweli mimi simwelewi either ana udini sana anaogopa ataleta atalaumiwa na wafuasi wa hizo dini ama hakuna kidhibiti. Ukilishikia bango sana yaleyale ya mafisadi utaambiwa upeleke kidhibiti au kawashitaki wewe.

Haya hivyohivyo hadi 2015 ifike arudi ikulu ndogo Bagamoyo.
 
Habari ya hovyo sana, yani wanafanya siasa juu ya siasa.

Sasa hapo siasa juu ya siasa ipo wapi? JK aliposema ukweli kuhusu viongozi wa Kanisa wanafanya biashara ya madawa ya kulevya, watu wa hiyo dini walimuona anaowaonea, sasa ukweli ndiyo huo. Leo tunajua hela za kujenga shule za Saint zinapotoka.
Lakini bado nashangaa kwa nini hizo shule zinaendelea kuitwa Saint wakati zimejengewa na hela za madawa ya kulevya!!
 
Aisee kumbe hizi habari za viongozi wa dini kijihusisha na madawa ya kulevywa ni za kweli?? Sasa JK alikuwa anaogopa nn kuwataja? Halafu yule kionozi wa dini aliyempinga JK hadharani kwamba awataje la sivyo amejivunjia heshima alikuwa ana maana gani? Kaaazi kwelikweli!!!!
Si chochote si lolote usanii mtupu. Ulisikia wapi polisi kujadiliana na mhalifu oo!? usinitaje jina. Lakini sawa "Ukimwaga mboga, ...." yaani nawaanika ViGoGo wa unga.
 
Si chochote si lolote usanii mtupu. Ulisikia wapi polisi kujadiliana na mhalifu oo!? usinitaje jina. Lakini sawa "Ukimwaga mboga, ...." yaani nawaanika ViGoGo wa unga.

Teh teh teh, damn i like your quote, so it is obvious, the question here is, serikali inahusika kwa kiasi gani kwa sasa kwenye hiyo global business? Siyo jipya hilo hata serikali za nchi kubwa zinahusika sana na hii business. Sasa what is fight against drug kwa bongo? ni uzushi tu! cabinet members wanasafiri with a diplomatic immunity wanayabeba sana madawa mpaka kwenye msafara wa rais mwenyeye! sasa atawataja lini hao jamaa zake?
 
Hao siyo viongozi wa dini bali ni matapeli wa kimataifa walikuwa wanakula dili na viongozi wa Serikali baada ya kukosa mgao wakaamua kulisanua. Tusubiri tuone seleka lake kama viongozi wa serikali hawajatajwa kwenye hii skendo.
 
Lakini wanatumia njia ya dini kuuza hayo madawa ya kulevya.
 
Wauza madawa wapo na serikali inawajua lakini mambo yaleyale nchi itatikisika na mkuu wa kaya anaogopa kuwataja. Mkuu wa kaya aliombwa sana na kiongozi mmoja wa dini kwamba awatae la sivyo anajivyunjia heshima yeye aliamua KUJUVUNJIA HESHIMA. Kwa kweli mimi simwelewi either ana udini sana anaogopa ataleta atalaumiwa na wafuasi wa hizo dini ama hakuna kidhibiti. Ukilishikia bango sana yaleyale ya mafisadi utaambiwa upeleke kidhibiti au kawashitaki wewe.

Haya hivyohivyo hadi 2015 ifike arudi ikulu ndogo Bagamoyo.

Sasa udini hapa upo wapi? JK anajaribu kuwapa heshima hao viongozi wa dini ili wasiaibike ktk jamii. Kama akiwataja majina unafikiri hali yao itakuwaje? ni aibu tupu kwa dini hiyo.
 
Sasa udini hapa upo wapi? JK anajaribu kuwapa heshima hao viongozi wa dini ili wasiaibike ktk jamii. Kama akiwataja majina unafikiri hali yao itakuwaje? ni aibu tupu kwa dini hiyo.

Hakuna cha viongozi wa dini hapa, Wanasiasa wanahusika kwenye sakata hili, viongozi wa dini wanatumika kama pazia la kuwakinga wanasiasa na wafanyabiashara walio karibu na watawala. Ndio maana hutasikia wahusika wamepelekwa mahakamani!!! Huwezi kunyamazia wauza madawa ambayo yanaangamiza taifa kila kukicha kwa kisingizio cha 'VIONGOZI WA DINI" Ni wapi kikatiba viongozi wa dini wamewekwa juu ya sheria.

Viongozi hao wa dini kama wangeisiwa kula njama za kuipindua serikali ingekuwaje? Wangeachwa ili isiwe aibu kwa dini hiyo? Hata kama ni Kard.PENGO sheria ichukue mkondo wake hata leo hii.

HAKUNA VIONGOZI WA DINI WANAOHUSIKA NA BIASHARA HII, HAO WALIOJITOKEZA NI WAHUNI TU WANAOTUMIA NENO 'VIONGOZI WA DINI''.
 
Back
Top Bottom