Dawa za Kichina kuongeza makalio, bikira, matiti, hips, kukuza uume zateketezwaw Dodoma

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
01_12_g27h11.jpg

Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati, Florent Kyomo
akimwaga bidhaa ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu kabla ya kuchomwa
katika dampo la Mbwanga katika Manispaa ya Dodoma mwishoni mwa wiki.

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) Mkoa wa Dodoma mwishoni mwa wiki iliteketeza bidhaa mbalimbali zenye thamani ya Sh milioni 26 ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu. Miongoni mwa bidhaa hizi ni dawa za Kichina za kuongeza ‘heshima kwenye ndoa’. Kaimu Meneja wa TFDA, Florent Kyombo alisema bidhaa hizo zina uzito wa tani sita na zilikamatwa
wakati wa ukaguzi uliofanyika Novemba 14 hadi 28, mwaka huu. Ukaguzi huo ulihusu maduka 104 ambapo kati yake, maduka 33 yalikutwa na bidhaa mbalimbali ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu.

Kabla ya kuteketezwa kwa bidhaa hizo eneo la Mbwanga, wakazi wanaokaa karibu na dampo hilo, walifika kushuhudia huku wengine wakiomba wapewe bidhaa hizo. “Mimi naomba mafuta hayo hata kama yameharibika nitayachemsha sana,” alisema mama moja wa makamo ambayo hata hivyo alibakia kushuhudia bidhaa hizo zikiteketea na kuamua kuondoka huku watoto wengi wakiomba kupewa juisi zilizolundikwa kabla ya kuteketezwa.

Bidhaa zilizoteketezwa ni dawa za Kichina za kuongeza makalio, kurudisha bikira, kukuza matiti, kuongeza hips, kukuza uume na kahawa ambayo hutumika kuongeza hamasa kwa wanawake.

Pia, vipodozi vya aina mbalimbali, dawa za binadamu, mipira ya kiume, dawa za meno, sabuni na vifaa vya maabara ambavyo havina taarifa za utengenezaji wake pamoja na vyakula mbalimbali ikiwemo mafuta ya kupikia, juisi na soda za kopo. Kyombo alisema bidhaa hizo zinateketezwa kwa gharama za mmiliki wa bidhaa ambaye husaini
fomu za kuteketeza bidhaa hizo na kuongeza kuwa bidhaa nyingi zinatoka nje ya nchi na ni vigumu kuwakamata watengenezaji.

Alisema jambo la msingi ni kuwasisitiza wadau kufanya biashara kwa misingi ya utaratibu na kanuni za vyakula dawa na vipozi. “Watanzania wakitilia shaka bidhaa zozote watoe taarifa ili hatua zichukuliwe,” alisema na kuongeza kuwa dawa za Kichina zinazouzwa kila kona zimekuwa na athari kubwa kwa maisha ya binadamu na baadhi zimekuwa zikiongeza shinikizo la damu.
 
Yaani hapo hayo makemikali yanachomwa moto tunaachiwa ma-fumes yanaenea tu bila mpangilio.
 
sku hizi kila mdada umuonae anariverse minikawaga nawapa sifa mabinti wa kibongo kumbe hamna lolote
 
Matatizo hatuna quality check when these things are brought into TZ soil. Kuchoma moto sio preventive measure, it should be at the time of clearing these items at our borders or ports.
 
Matatizo hatuna quality check when these things are brought into TZ soil. Kuchoma moto sio preventive measure, it should be at the time of clearing these items at our borders or ports.

Madawa mengi yamezagaa kila kona na watu wanaumusha makalio miili inaonekana mizuri kwa sura lakini ukiishika imekakamaa kama mpira wa kucheza uwanjani, hawajui ladha ya uzuri aliotuwekea Muumba wetu.
 
Back
Top Bottom