Dawa ya UKIMWI yagunduliwa?

Bado ni tatizo mpaka hizo dawa zifike huku si leo wala kesho na hata bei yake sijui kama tutaiweza..
Tuendelee na kujilinda/kujikinga tu..mpaka hapo zitakapo kuja...
 
Bwana wewe AIDS is still a threat..imagine mtu maskini anayeugua AIDS kule kwetu Kayenze, pembeni mwa ziwa victoria,ambaye hata dawa za malaria tu bado ni issue, atawezaje kupata faida ya reaserch hizi zilizoko lab za Marekani? Hapa we talk something of months or years before we get the benefit.

No! For this case, they will hasten delivery. This is because AIDS affects everybody, including themselves. Had it been malaria or typhoid, they could haven't even broken the news!
 
Mimi sijaipenda dawa au kinga hii kwani ugonjwa huu kwa asilimia 99 ni wakujitakia! Sasa sample zilikuwa 200 je, hii sample ni representative? Je, kama kuna aina ya 201, itakinga au kutibu? Mungu hajaribiwi!

Jee una uhakika kila anaeuguwa ugonjwa huu amejitakia? kumbuka kuna watoto wadogo mamilioni na pia wapo ambao wamefanyiwa blood transfusion nao wameupata au hujui hilo ? Hata kama wamejitakia jee hakuna kutubu kwenye dini yako mkuu ?
 
Mimi sijaipenda dawa au kinga hii kwani ugonjwa huu kwa asilimia 99 ni wakujitakia! Sasa sample zilikuwa 200 je, hii sample ni representative? Je, kama kuna aina ya 201, itakinga au kutibu? Mungu hajaribiwi!

.
Katika hili lina uhusiano gani na kumjaribu Mungu? Hivi inawezekana binadamu kumjaribu Mungu? Maana mimi ninachoona ni Mungu akimjaribu mwanadamu kwani hujaribika kwa tamaa zake mwenyewe. Je twaweza kumjaribu Mungu kwa kumtega kwa jambo fulani hivi ambalo ataingia tamaa ili anase? Na hata kama hatanasa, dhamira yetu ndio imebeba kusudio la kumtega? Basi mungu huyu atakua sii yule wa kuujua mwisho tokea mwanzo.
Nikirudi kwenye hoja kama kweli dawa imepatikana ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kujalia akili aliyomuumbia binadamu kugundua dawa. Pia nawapongeza hao ma-Dr maana nguvu kazi ya dunia ilikua inateketea kama kichaka kilichowashwa moto.
 
Mh!, Crisipin umesikia news hizo???......nadhani ratiba za uswazi zitaongezeka maradufu!!:A S tongue::A S tongue::A S tongue:
 
Mh!, Crisipin umesikia news hizo???......nadhani ratiba za uswazi zitaongezeka maradufu!!:A S tongue::A S tongue::A S tongue:

Mkuu kwa mawazo kama haya basi hatapona mtu. Kwa kuwa malaria ina dawa basi uruhusu mbu wakuume tu enhe!. Ukimwi unaua na hauna dawa wala kinga na hata ikipatikana/imepatikana bado utaendelea kuua tu! kwani magonjwa kama malaria si yana dawa lakini still ni number one killer in tropical countries. Usidanyike kinga ni bora kuliko tiba
 
Bado ni tatizo mpaka hizo dawa zifike huku si leo wala kesho na hata bei yake sijui kama tutaiweza..
Tuendelee na kujilinda/kujikinga tu..mpaka hapo zitakapo kuja...

Waziri wa Afya Kawahakikishia wananchi wa Tz kwamba serikali itafanya kila linalowezeka ili raia wake wapate dawa hizo hata pembezoni mwa nchi
 
Mimi sijaipenda dawa au kinga hii kwani ugonjwa huu kwa asilimia 99 ni wakujitakia! Sasa sample zilikuwa 200 je, hii sample ni representative? Je, kama kuna aina ya 201, itakinga au kutibu? Mungu hajaribiwi!
ikiwa kweli inamaana mungu kashindwa, tuache unafiki wa kumwingiza mungu kwa mambo yanayowezekana na mwanadamu
 
Waziri wa Afya Kawahakikishia wananchi wa Tz kwamba serikali itafanya kila linalowezeka ili raia wake wapate dawa hizo hata pembezoni mwa nchi
Lakini Waziri wa Afya si WHO au kampuni ya utengenezaji wa dawa. Itabidi naye asubiri mpaka hizo dawa zitengenezwe na zithibitishwe na FDA Marekani.
 
Waziri wa Afya Kawahakikishia wananchi wa Tz kwamba serikali itafanya kila linalowezeka ili raia wake wapate dawa hizo hata pembezoni mwa nchi

Nani kasema dawa YA UKIMWI imepatikana? DAWA YA UKIMWI BADO.... WATAALAMU BADO WAKO KWENYE MAABARA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Inasikitisha kuona wasomi wanafanya conclusion kwa majaribio yanayoendelea maabara. Na hili li-waziri tena professor zima na uzima wake linakuwa kama li-sangoma.... Nimesoma gazeti la mwananchi walivyom-quote ... ni AIBU AIBU AIBU.....
 
Kama dawa imepatikana basi tutegemee msukosuko mwingine wa uchumi. Hivi asasi zote zinashughulika na ukimwi wafanyakazi wake watakwenda wapi? Mahospitali yanayopata misaada kwa kisingizio cha kupambana na ukimwi si kwisha kazi, TACAIDS, ni mihela mingi nchi maskini ikiwemo Tanzania inapata kupambana na ukimwi na miradi mingi imefunguliwa na kuajiri idadi kubwa na inalipa mishahara ya kufa mtu
 
Hizi habari za dawa kupatikana zinatangazwa Bongo tu au?.......

Hii dawa iliyogunduliwa ni 90% effective kiwango kilichoifanya FDA ya marekani iweze kuipasisha! Sasa waswahili wakifanya ngono zembe kwa kutegemea dawa kugunduliwa, watajikuta wanaangukia kwenye hiyo 10% ambayo dawa haitibii na itakuwa imekula kwao!!. Elimu kwa wananchi juu ya dawa hii ni muhimu.
 
Mimi sijaipenda dawa au kinga hii kwani ugonjwa huu kwa asilimia 99 ni wakujitakia! Sasa sample zilikuwa 200 je, hii sample ni representative? Je, kama kuna aina ya 201, itakinga au kutibu? Mungu hajaribiwi!
wewe hizo statistics zako umezitoa wapi?
 
ni habari njema kusikia ila twahitaji subira na umakin sikila lisemwalo ni sahihi subiri watu watumie tuone feedback UKIMWI majamen watisha.
 
sijui kwa nini nina hisia Dawa ya AIDS ipo tu wanazungusha zungusha mambo mpaka tufikie katika takwimu fulani then waje waanze kuvuna hela zetu.au wasambeze dawa kwa style ya mikopo

Hivi wanasayansi walishakubalina juu hasa ya chanzo cha HIV/AIDS?

Kuna mtaalmu 1ja alisema AIDS researches has not failed because it cant find a cure. AIDS reseaches has failed because it never found ia cause
 
Back
Top Bottom