Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa ya ngiri

Discussion in 'JF Doctor' started by Polisi, Jun 27, 2011.

 1. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,090
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Wakuu,

  Habari ya kazi. Nilikuwa Bugando kwa ajili ya kufanyiwa kipimo kinachoitwa endoscopy. Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo

  Esophagus – MILD DISTAL OESOPHAGISI 2”/HIATAL HERNIA
  Stomach - HIATAL HERNIA
  Duodenum – NORMAL
  Final Diagnosis - GERD 2” HIATAL HERNIA

  Sasa WIKI IJAYO nakwenda kuonana na daktari bingwa nimpe majibu haya. Kama mjuavyo watu ni wengi na hivyo kupata muda wa kujieleza na kudodosa vizuri kwa daktari inakuwa ni ngumu. Ndiyo maana nikaona ni bora nianzie hapa nipate mawili matatu mfano:

  - Kwa matokeo haya ya vipimo nitegemee nini kutoka kwa daktari
  - Baada ya kupitia humu jf nikagundua hiatal hernia ni ngiri, je inaweza pia kusababisha haya maumivu ya MIGUU na MIKONO?

  HALI YANGU KWA SASA

  Maumivu sehemu ya juu ya tumbo kama kuna kidonda ambayo yanapelekea maumivu hadi miguuni kwenye nyayo na mikononi. Maumivu yakipungua kifuani na miguu wala mikono haiumi. MAUMIVU PIA HUWA NAHISI MGONGONI

  HISTORIA YA TATIZO

  Ilianza mwaka 1998 baaada ya kupata stress sana. Ilitokea baada ya kuhisi kuwa msichana niliyetembea naye alikuwa ameathirika baada ya kumkuta amelazwa hospitalini na akadai anaumwa TB. Kwa kweli alikuwa amekonda sana. Kuanzia hapo mauza uza yakaanza kwa kukosa amani na mawazo tele. Mara tumbo, mara kifua mara miguu kuwaka moto nk. Hayo yote yalipelekea mimi kuconclude kwamba nimeathirika na sikutaka hata kujisumbua kupima

  Niliishi na hali hiyo kwa miaka karibu 4 yaani hadi katikati ya 2002 ndipo nilipopata ujasiri wa kwenda kupima. Nilianzia CBBRT negative, the same day nikarush ANGAZA negative. Nikamshukuru mungu. Maumivu makali yaliendelea yaani tumbo, kifua, miguu na mikono kuwaka moto n.k. Nikaenda Muhimbili na kufanyiwa kipimo cha BARIUM na kukuta nina ULCERS. Nikaanza masharti ya ulcers na dawa mbalimbali za kitalaam na zile za asili but changes zilikuwa kidogo sana. Nakumbuka nilikuja humu jf na kueleza tatizo langu na mchangiaji mmoja nadhani ni Riwa (sijui kama yupo huyu ndugu, sijamwona siku nyingi) alionesha wasiwasi wake kama kweli ilikuwa bado ULCERS kwa jinsi nilivyotumia dawa mbalimbali

  Mwaka 2011 nikarudi tena Muhimbili na kufanyiwa kipimo cha endoscopy na majibu yakawa nina oesophagistis fungus. X ray – normal na HIV negative. Nikapewa dawa awamu ya kwanza nikamaliza na dawa awamu ya pili kama aina nne hivi nikamaliza. Maumivu yakapungua kwa asilimia 50. Daktari mmoja aka-recommend tena nirudie endoscopy kwa kuwa ni HIV negative (Assumption kwamba hizo fungus huwapata walioathirika). Ndiyo maana nikaenda tena hosptali
   
 2. Chrizo

  Chrizo Senior Member

  #2
  Oct 25, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Samahani wana jf nilikuwa napenda kujua hernia ni ugonjwa gani na husababishwa na nini,pia dalili na matibabu yake ni yapi. Nawasilisha
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,053
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  kwa kiswahili wanaita NGIRI


  nadhani hukukwepa umande


  [h=3]Hernia Causes[/h]Although abdominal hernias can be present at birth, others develop later in life. Some involve pathways formed during fetal development, existing openings in the abdominal cavity, or areas of abdominal-wall weakness.
  • Any condition that increases the pressure of the abdominal cavity may contribute to the formation or worsening of a hernia. Examples include
   • obesity,
   • heavy lifting,
   • coughing,
   • straining during a bowel movement or urination,
   • chronic lung disease, and
   • fluid in the abdominal cavity.
  • A family history of hernias can make you more likely to develop a hernia

  [h=3]Hernia Symptoms and Signs[/h]The signs and symptoms of a hernia can range from noticing a painless lump to the severely painful, tender, swollen protrusion of tissue that you are unable to push back into the abdomen (an incarcerated strangulated hernia).
  • Reducible hernia
   • It may appear as a new lump in the groin or other abdominal area.
   • It may ache but is not tender when touched.
   • Sometimes pain precedes the discovery of the lump.
   • The lump increases in size when standing or when abdominal pressure is increased (such as coughing).
   • It may be reduced (pushed back into the abdomen) unless very large.
  • Irreducible hernia
   • It may be an occasionally painful enlargement of a previously reducible hernia that cannot be returned into the abdominal cavity on its own or when you push it.
   • Some may be chronic (occur over a long term) without pain.
   • An irreducible hernia is also known as an incarcerated hernia.
   • It can lead to strangulation (blood supply being cut off to tissue in the hernia).
   • Signs and symptoms of bowel obstruction may occur, such as nausea and vomiting.
  • Strangulated hernia
   • This is an irreducible hernia in which the entrapped intestine has its blood supply cut off.
   • Pain is always present, followed quickly by tenderness and sometimes symptoms of bowel obstruction (nausea and vomiting).
   • The affected person may appear ill with or without fever.
   • This condition is a surgical emergency.
   
 4. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  umetusaidia na sisi pia! eimen!!
   
 5. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,565
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Well summarized Edson...
   
 6. Chrizo

  Chrizo Senior Member

  #6
  Oct 25, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  ahsante mkubwa ubarikiwe
   
 7. God bell

  God bell JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Could u summarize is kiswahili so we can understand all of us. Thankx mkuu.
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 38,540
  Likes Received: 2,808
  Trophy Points: 280
  Kwanza niseme kuwa kwa kiswahili bado kuna mkanganyiko wa neno Ngiri. Wapo wanoiita ngiri kwa maana ya busha (hydrocele), na wengine huita ngiri (Hernia) ambayo ni sehemu ya viungo kuingia sehemu nyingine kwasababu ya kuwa l'oose'

  Kwa maelezo yako nadhani unaongelea abdomen hernia ambayo sehemu ya utumbo hutumbukia katika hasua. Hii ni kwasababu sehemu inayozuia (kiwambo) inakuwa imeachia. Utumbo huingia huko na kukuletea maumivu. Siyo maradhi yanayosababishwa na wadudu, hutokea hata kwa watoto wadogo au watu wazima ambao hufanya kazi za nguvu n.k.

  Hakuna dawa inayotibu bali zinazopunguza maumivu. Mara nyingi ukilala na taratibu kusukuma hicho unachokihisi kurudi juu, basi hali inaweza kutulia. Itajirudia tena tena kwasababu umesogeza tu lakini hujazuia.

  Matibabu yake ni operesheni ya kufunga sehemu hiyo. Matibabu hayo ni muhimu sana kwasababu inaweza kutokea kuwa utumbo umeingia ukajikunja na kushindwa kupitisha damu (strangulated hernia) hivyo sehemu hiyo itaoza na kuweza kuleta madhara makubwa zaidi tusiyotarajia.
  Hutokea nadra lakini inapotokea hujui utakuwa sehemu gani ya huduma muhimu na za haraka hapo unaweza kujikuta katika wakati mgumu sana kimaumivu na pengine kimaisha.

  Tafadhali kawaone madaktari katika hospitali kubwa kwa ushauri zaidi.
  source:
  http://www.jamiiforums.com/jf-doctor/177748-ugonjwa-wa-ngiri.html
   
 9. God bell

  God bell JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mkuu nashukuru kwanza kwa kukubali kubadilisha hiyo lugha ya kingereza kuwa kiswahili kwa faida ya wengi. Nakumbuka mwezi ulopita niliweka thread kama hii nikiwa nasumbuliwa na huu ugonjwa wa ngiri. Nimeshaonana na doctor na ameniambia nahitaji upasuaji. Hivyo ndo najiandaa kwa operation. Asanteni kwa wale walotoa mchango wao wa kunishauri.
   
 10. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,329
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Wakuu nina tatizo la kutopata choo(Nikifika chooni mzee anafika mpaka dirishani lakini hatoki ng'o) wakati wa baridi au nikipigwa na baridi kama ya ac, sometime nikinywa maji ya baridi. Ukienda hospitali wanakupa dawa za constipation. Daktari huwa wananiambia niwe nakunywa maji na kula matunda sana. Ukweli ni mlaji sana wa matunda na kunywa maji yasipongua lita 3 kwa siku.

  Katika uchunguzi wangu nimegundua kwamba tatizo hili hutokea wakati nikihisi hali ya ubaridi kama nilivyoelza hapo juu, nimegundua kwamba hii itakuwa ngiri tu ingawa sihisi chochote kuvimba kwenye mwili wangu.

  Nani anajua dawa ya tatizo hili. Kama ni ngiri je ipi ni tiba yake ya kudumu acha hizi za muda

  Nawasilisha
   
 11. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 490
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nenda Pale Eneo la Temeke Vetenary kuna kituo cha Mafuta OIL COM, next building ni msikiti, unaitwa Masjid Iman. Ukifika hapo utaona kuna kibanda kidogo geti la kuingia msikitini. Hapo kuna jamaa anauza dawa za miti shamba. Kuna dawa ya mchanganyiko wa miti mbalimbali inaitwa MIDDLE FILDER. Ukiitumia dawa hiyo naamin tatizo lako litaisha. Naomba usidharau kama kweli unatatizo hilo.
   
 12. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,329
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mkuu nashukuru sana. Tatizo lipo.Nitalifanyi akazi mkuu. Nikirudi nitakubrief
   
 13. ldd

  ldd JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 786
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Dawa yake ndgo husinywe maji na vingine vya baridi!
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 38,540
  Likes Received: 2,808
  Trophy Points: 280
  hiatal hernia.jpg


  Hiatus Hernia ni tundu linalotokea baada ya sehemu ya juu ya mfuko wa kuhifadhia chakula (tumbo) kuingia kwenye sehemu ya kifua kupitia uwazi unaojulikana kama esophageal hiatus. Kwa kawaida uwazi huu (esophageal hiatus)hupitisha mrija wa chakula kwenda kwenye tumbo yaani esophagus na si utumbo.

  Mara nyingi, tatizo hili huonekana kwa takribani ya 60% ya watu wenye umri wa miaka 50 na kuendelea, ingawa pia linaweza kuwapata wale walio na umri wa chini ya huo.

  Kuna aina mbili kuu za hiatus hernia

  • Sliding type : Kama jina lake linavyomaanisha, aina hii hutokea iwapo sehemu ya juu ya utumbo inaposukumwa juu na kuingia kwenye upenyo wa esophagus hiatus baada ya kutokea kwa ongezeko la presha katika maeneo ya tumbo(increased pressure in the abdominal cavity) na kurudi kama kawaida wakati presha inapopungua.
  • Fixing type: Aina hii hutokea iwapo sehemu ya juu ya utumbo inapokuwa kwenye maeneo ya kifua na haishuki chini.

  Vihatarishi vya Ugonjwa huu
  1. Ongezeko la presha tumboni kutokana na;

  • Kunyanyua vitu vizito au kuinama sana
  • Kukohoa sana au kukohoa mara kwa mara kutokana na sababu mbalimbali
  • Kutapika sana (violent vomiting)
  • Kupiga chafya sana (Hard sneezing)
  • Ujauzito -Kutokana na mfuko wa uzazi (uterus) kusukuma viungo kwenda juu kutokana na kuongezeka ukubwa wake.
  • Wakati wa kujifungua- Kutokana na kuongezeka kwa presha ndani ya tumbo wakati mama anajitahidi kusukuma mtoto. Si wanawake wote wanaopata tatizo hili.
  • Kujikamua wakati wa kwenda haja kubwa (straining during constipation)
  • Uzito uliopitiliza -Kutokana na kuongezeka uzito ambao unasukuma viungo kwenye maeneo ya kifua kwenda chini na hivyo kuongeza presha tumboni.
  • Kujisaidia haja kubwa wakati mtu amekaa - Kutokana na maendeleo ya binadamu, watu wengi sasa hivi wameanza utamaduni wa kutumia vyoo vya kukaa wakati wa kujisaidia haja kubwa, katika tafiti iliyofanywa na Dr Denis Burkitt (1), imeonekana ya kwamba kujisaidia wakati mtu amekaa hufanya mtu kujikamua zaidi na hivyo kuongeza presha ndani ya utumbo (Increased intraabdominal pressure) na hivyo kusukuma mfuko wa kuhifadhia chakula (utumbo) kupitia kwenye upenyo wa esophagus hiatus na hivyo kusababisha hiatus hernia.
  2. Tatizo la kurithi (Heredity)
  3. Uvutaji sigara
  4. Matumizi ya madawa ya kulevya kama cocaine
  5. Kuwa na kiwambo hewa (diaghram) dhaifu
  6. Msongo wa mawazo (depression)
  7. Matatizo ya kuzaliwa (congenital defects).


  Dalili na Viashiria

  • Maumivu ya kifua
  • Kichomi (pleurisy) ambacho kinakuwa kikali sana wakati wa kuinama au mtu anapolala chini
  • Matatizo katika kumeza chakula
  • Kupumua kwa shida Kutokana na hiatus hernia kupunguza uwezo wa ufanyaji kazi wa kiwambo hewa (diaphragm).
  • Mapigo ya moyo kwenda kasi Kutokana na mkwaruzo wa neva inayojulikana kama vagus nerve.
  Mara nyingi sana hiatus hernia haioneshi dalili zozote zile isipokuwa inapokuwa kubwa sana. Maumivu na kichomi hutokana na kurudishwa kwa tindikali ya kwenye tumbo (gastric acid) kwenye kifua. Pia tindikali aina ya bile acid na hewa huwa inasukumwa juu kwenye kifua.

  Vipimo vya Uchunguzi

  1. Barium Swallow X-ray – X-ray ya kuangalia viungo vya ndani, mgonjwa hupewa au huchomwa sindano yenye dawa maalum ambayo huonekana vizuri kwenye X-ray, na baada ya hapo hupigwa picha za X-rayakiwa amekaa au amesimama. Kawaida kipimo hiki huchukua masaa 3-6.
  2. Esophagogastroduodenoscopy (OGD) - Mpira maalum wenye taa na camera kwa mbele unaoingizwa mdomoni kwenye mpira wa kupitisha chakula (esophagus) na hutazama kama kuna magonjwa yoyote kwenye esophagus hadi kwenye sehemu inayojulikana kama duodenum.

  3. Electrocardiography (ECG)- Kipimo cha kuangalia kama kuna matatizo katika jinsi moyo unavyopiga

  4. Chest X-ray- Kuangalia kama kuna magonjwa kama homa ya mapafu (Pneumonia), kama kuna pafu lolote ambalo halifanyi kazi, madhara kwenye moyo (injury to the heart) na pia kuangalia matatizo yoyote yale.
  5. Complete Blood Count- Kipimo cha kuangalia wingi wa damu, kuangalia aina mbalimbali za chembechembe za damu kama zipo katika maumbo yao ya kawaida, wingi wao kama ni wa kawaida.

  Tiba ya Hiatus Hernia
  Kama ilivyoelezwa hapo awali, hiatus hernia mara nyingi haioneshi dalili zozote na hivyo mtu anaweza kuendelea na shughuli zake za kila siku bila madhara yoyote. Tiba ya hiatus hernia inahusisha dawa na upasuaji.

  Tiba ya Dawa

  • Dawa za kuyeyusha tindikali mwilini (antacids) hutumika kama Gelusil, Maalox nk.
  • H2 receptor antagonist –Dawa zinazopunguza kiwango cha utolewaji wa tindikali kama cimetidine, ranitidine nk.
  • Dawa ambazo huzuia utolewaji wa tindikali na kuponya tishu za esophagus (Proton Pump Inhibitors) dawa hizi ni omeprazole, lansoprazole nk.

  Tiba ya Upasuaji
  Upasuaji hufanyika kwa wagonjwa wa dharura au pale ambapo mgonjwa hajapata nafuu hata baada ya kutumia dawa na hali yake inazidi kuwa mbaya. Upasuaji huu hufanywa na daktari wa upasuaji kwa kuchana (incision) kwenye kifua (thoracotomy) au tumbo

  (laparatomy) na kuvuta sehemu ya utumbo iliyopanda juu kwenye kifua ili kuirudisha katika sehemu yake ya kawaida na kupunguza ule uwazi uliopo kwenye diaphgram, kurekebisha sphincters (nyama zinazosaidia katika kufunga na kufungua uwazi kwenye diaphragm) za

  esophagus ambazo zimekuwa dhaifu. Pia daktari anaweza kufanya upasuaji huu kwa kuchana sehemu ndogo sana kwenye tumbo na kwa kutumia kifaa maalum chenye kumsaidia kurekebisha henia hii. Aina hii ya upasuaji hujulikana kama endoscopic surgery.


  Madhara ya Hiatus Hernia
  Madhara ya hiatus hernia hutokana na kurudishwa juu kwa tindikali aina ya gastric acid na hivyo kusababisha ugonjwa unaojulikana kama Gastroesophageal Reflux Disease (GERD).

  Madhara haya ni;

  • Kichomi
  • Ugonjwa wa esophagitis
  • Barretts esophagus
  • Saratani ya kwenye mpira wa kupitisha chakula (esophageal cancer)
  • Kuoza kwa meno (dental erosion)
  • Strangulation of the stomach (kunyongwa kwa sehemu ya juu ya tumbo na hivyo kusababisha sehemu hii kukosa damu ya kutosha na hivyo tishu zake kufa na kuoza (ischemic and necrosis)
  • Kuzuia pafu kujaa hewa na hivyo kushindwa kutanuka na kusababisha mtu kupumua kwa shida sana.

  Jinsi ya kujikinga
  1. Kuacha kunywa pombe

  2. Kuacha matumizi ya madawa ya kulevya kama cocaine

  3. Kupunguza uzito uliopitiliza (soma makala ya jinsi ya kupunguza uzito wako (Diet Plan) na uzito uliopitiliza (Obesity)

  4. Kula milo midogo mara nyingi kwa siku
  5. Epuka vyakula vinavyoongeza kichomi kama chocolate, vitunguu, vyakula vikali, vinywaji venye limau, ndimu nk.

  6. Kula chakula cha usiku masaa matatu kabla ya kwenda kulala

  7. Pumzika kwa kukaa baada ya kula usilale chini.

  8. Nyanyua sehemu unayoweka kichwa chako wakati wa kulala kwa angalau 15cm (6 inches)

  9. Punguza msongo wa mawazo

  10. Acha kuvuta sigara.

  Marejeo
  1. Burkitt DP (1981). "Hiatus hernia: is it preventable?". Am. J. Clin. Nutr. 34 (3): 428–31. PMID 6259926
  2. Sontag S (1999). "Defining GERD". Yale J Biol Med 72 (2-3): 69–80. PMC 2579007. PMID 10780568
  Hiatus Hernia (Ngiri ya Kwenye Kifua)
   
 15. The Son

  The Son JF-Expert Member

  #15
  Dec 1, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 463
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Edson, unaweza kuweka 'source' ya ulichoki-post kama alivyoweka MziziMkavu?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Delvis

  Delvis Member

  #16
  Feb 13, 2013
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 77
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  jamani naombeni mnisaidie dawa ya mships wangiri, hii kitu inanitesa sana, kama kuna mtu ana uelewa kidogo juu ya hili naomba msaada wake kwanzia mudaa huu iliniweze kufanyia kazi mara moja..
   
 17. Petro E. Mselewa

  Petro E. Mselewa Verified User

  #17
  Feb 13, 2013
  Joined: Dec 27, 2012
  Messages: 4,837
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #18
  Feb 13, 2013
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 38,540
  Likes Received: 2,808
  Trophy Points: 280
  Mkuu.@DelvisKuhusu tiba ya ngiri inatakiwa ufanyiwe upasuaji Operesheni inategemea Ngiri zipo za aina 2 ya kwanza ni ya ndani inaitwa kwa kiingereza ( Hernia)


  Na Ngiri ingine ni ya Mshipa wa Kushuka ni hii hapa Mabusha kwa lugha ya kiswahili


  I
  Mabusha ni hali ya kujaa maji kwenye mfuko wa pumbu. Hali hii hutokea kunapokuwa na mkusanyiko wa maji kati ya tabaka mbili za utando unaozunguka korodani.
  Inakadiriwa kuwa karibu asilimia moja ya wanaume wote kote duniani huathiriwa na tatizo hili. Kwa hapa nchini, tatizo hili ni maarufu sana maeneo ya mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi, kiasi cha kuhusishwa na imani kadhaa.

  Mojawapo ya dhana iliyozoeleka miongoni mwa watu wa mwambao ni kuwa mabusha yana uhusiano mkubwa na unywaji wa maji ya madafu. Aidha, tatizo hili limekuwa likichukuliwa na baadhi ya watu kuwa ni hali ya kudhalilisha ingawa kwa wengine huonekana ni hali ya kuwa ‘mzee wa heshima' au ‘umwinyi'.


  Ifahamike pia kuwa, tatizo la mabusha halitokei kwa wanaume watu wazima tu. Watoto wa kiume hususani katika mwaka wa kwanza (infants) pia ni waathirika wakuu wa tatizo hili.


  Kwa kawaida mabusha hayana maumivu na wala hayaleti madhara, isipokuwa kama yatapata uambukizi kwa sababu nyingine yeyote ile, hali inayowafanya wengi wa waathirika, hasa wa mwambao, kuwa wagumu kutafuta ufumbuzi wa tiba.


  Hata hivyo, ni vyema kama mtu ana uvimbe wowote kwenye pumbu zake, kutafuta msaada wa kitabibu ili kuweza kuondoa uwezekano wa kuwepo kwa magonjwa mengine ya sehemu za siri kama vile saratani ya korodani (testicular cancer) n.k.

  Mabusha husababishwa na nini?

  Sababu za kutokea kwa mabusha hutofautiana kati ya watoto wa kiume na wanaume watu wazima.  Kwa watoto wa kiume
  Kwa watoto wa kiume, mabusha huweza kuanza kutokea kipindi cha ujauzito.
  Wakati wa ujauzito, korodani za mtoto wa kiume huwa kwenye tumbo lake kabla ya kushuka taratibu kuelekea kwenye mapumbu. Wakati wa ushukaji huo, kifuko kinachozunguka korodani kinachoitwa processus vaginalishushuka sambamba na kurodani hizo na kufanya korodani kuzungukwa na maji.

  Kwa kawaida, ndani ya muda wa mwaka mmoja, kifuko hiki hufunga na maji hayo yanayozunguka korodani yote hufyonzwa na kurudishwa kwenye tumbo la mtoto. Iwapo baada ya kifuko kufunga na maji yaliyomo kushindwa kufyonzwa kurudishwa kwenye tumbo la mtoto, mtoto hupata busha lijulikanalo kitaalamu kama busha lisilo na mawasiliano (non-communicating hydrocele).


  Hali kadhalika, wakati mwingine inawezekana kifuko kikashindwa kufunga na hivyo maji yakaendelea kujaa ndani ya kifuko kuzunguka korodani. Aina hii ya mabusha kwa watoto ujulikana kama busha lenye mawasiliano (communicating hydrocele).


  Kwa wanaume watu wazima

  Kwa wanaume watu wazima, mabusha husababishwa na mambo makuu mawili; Kwanza, kitendo chochote kinachochochea tando zinazozunguka korodani kuzalisha maji kwa wingi kuliko kawaida, na njia ya pili ni kupungua kwa ufyonzaji wa maji yanayozunguka korodani kwa sababu ya kuziba kwa mirija ya lymph (blockage of scrotal lymphatic system) au kuziba kwa mishipa ya damu inayosafirisha damu kutoka kwenye pumbu kwenda sehemu nyingine za mwili (blockage of scrotal venous system).

  Ongezeko la uzalishaji wa maji linaweza kutokana na


  • Maambukizi au/na majeraha katika korodani (testicular inflammation auorchitis) au maambukizi katika mshipa ujulikanao kamaepididymisyanayoweza kusababishwa na kifua kikuu (tuberculosis) cha makende, au maambukizi yanayosababishwa na vimelea wa filaria(filariasis) wanaosababishwa na kuumwa na mbu aina ya Culex.
  • Kujinyonga kwa korodani (testicular torsion) kunakoweza kuzifanya korodani kutenda kazi zaidi ya kiwango chake (hyperactive testis).
  • Uvimbe katika korodani (testicular tumors) ambao husababisha uzalishaji wa maji kupita kiasi.

  Kupungua kwa ufyonzaji wa maji hutokana na

  • Kufanyiwa upasuaji kipindi cha siku za nyuma katika eneo la kinena, au operesheni ya upandikizaji figo ambazo zinaweza kuathiri mfumo wa lymph na vena na hivyo kupunguza ufyonzaji wa maji kutoka kwenye mapumbu.
  • Kuwahi kufanyiwa tiba ya mionzi kipindi cha nyuma nayo uhusishwa na kutokea kwa mabusha.

  Kwa hapa kwetu Tanzania, kung'atwa na mbu aina ya Culex anayeeneza vimelea vya filaria kunaelezwa kuwa sababu kuu mojawapo inayopelekea kuwepo kwa tatizo la mabusha na matende hususani maeneo ya Pwani na mwambao.

  Dalili za Mabusha

  Katika hatua za awali, mabusha huwa hayana dalili zozote (asymptomatic).
  Hata hivyo, baada ya muda fulani, mapumbu hujaa na uvimbe huweza kuonekana hata kwa nje. Kwa kadiri uvimbe unavyozidi kuongezeka, dalili zifuatazo zaweza kujitokeza pia;

  • Muhusika kujihisi hali ya uzito na kuvuta sehemu za siri kutokana na kujaa na kuongezeka kwa uzito wa mapumbu.
  • Mgonjwa huweza kujihisi hali ya usumbufu na kutojisikia vizuri maeneo ya kinena mpaka mgongoni.
  • Kwa kawaida mabusha hayana maumivu yeyote. Hata hivyo, iwapo mgonjwa ataanza kujihisi maumivu, hiyo ni dalili ya kuwepo kwa uambukizi katika mshipa wa epididymis (acute epididymitis)
  • Uvimbe huwa na tabia ya kupungua iwapo mgonjwa atakaa kitako na huongezeka pindi anaposimama.
  • Iwapo mgonjwa atajisikia homa, kichefuchefu na kutapika, hizo ni dalili za kuwepo kwa uambukizi katika mabusha.
  • Kwa kawaida mabusha hayana muingiliano na uwezo na ufanisi wa utendaji wa ngono. Hata hivyo kuna taarifa tofauti za kitafiti kutoka bara Asia na Afrika Magharibi kuwa mabusha yanaweza kuathiri ufanisi wa ngono na kwa kiasi fulani kusababisha mhemko au msongo wa mawazo kwa muathirika.

  Uchunguzi na Vipimo

  Uchunguzi mzuri wa kitabibu (physical examination) huwezesha kugundua uwepo wa mabusha kwa kiasi kikubwa bila hata kuhitaji vipimo vya ziada. Vipimo uhitajika tu kwa ajili ya kuchunguza chanzo cha mabusha, madhara yaliyoletwa na mabusha au kujua hali ya korodani.

  Vipimo ni pamoja na

  • Kupima damu (Full Blood Count) na mkojo (Urine Analysis) kuchunguza uwepo wa maambukizi kama vile vimelea wafilaria na mengineyo.
  • Ultrasound ya kinena pamoja na mapumbu: Aina hii ya kipimo hufanywa ili kuchunguza uwepo wa matatizo mengine tofauti na mabusha. Matatizo hayo ni kama vile ngiri, uvimbe, kujinyonga kwa korodani (testicular torsion), majeraha katika korodani, damu kuvuja kwenye kwenye korodani (traumatic hemorrhage) au maambukizi.


  Matibabu ya Mabusha


  Kwa watoto wadogo, kwa kawaida mabusha hupotea yenyewe ndani ya mwaka mmoja. Iwapo hayajapotea, mtoto uhitaji kufanyiwa upasuaji kama tiba.

  Kwa wanaume watu wazima, mabusha pia huweza kupona yenyewe bila kuhitaji tiba. Iwapo mabusha hayajapotea na yanamletea mgonjwa usumbufu (discomfort) au hali mbaya ya kiumbo (disfigurement) hayana budi kufanyiwa upasuaji ili kuyaondoa.
  Njia za tiba ni

  • Upasuaji: Upasuaji wa mabusha huweza kufanyika bila ya mgonjwa kuhitaji kulazwa (outpatient). Madhara yanayoweza kutokea wakati wa upasuaji wa mabusha ni pamoja na damu kuganda (blood clots), maambukizi au majeraha kwenye korodani. Hii ndiyo njia maarufu zaidi na ya kuaminika ya matibabu ya mabusha duniani kote.  • Kunyonya maji kwa kutumia sindano maalum (Needle aspiration): Njia nyingine inayotumika kutibu mabusha ni kuyanyonya maji kwa kutumia sindano maalum (needle aspiration). Hata hivyo njia hii haitumiki sana sehemu nyingi duniani kwa sasa kwa sababu maji ya mabusha huwa yana tabia ya kujirudia baada ya muda mfupi hata kama yatanyonywa.

  Baadhi ya matabibu hupendelea kudunga dawa maalum za kuzuia maji yasijae tena (sclerosing agents) mara baada ya kunyonya na kuyaondoa maji yote.
  Njia hii ya kunyonya maji ya mabusha, hufaa zaidi kwa wagonjwa wasioweza kuhimili upasuaji. Madhara yanayoweza kusababishwa na tiba ya namna hii ni pamoja na maambukizi na maumivu kwenye korodani.
  Hata hivyo wakati mwingine, bila kujali ni tiba gani imetumika, mabusha huweza kujirudia baada ya matibabu.

  Madhara ya Mabusha

  Kwa kawaida mabusha hayana madhara yeyote. Aidha mabusha hayawezi kuathiri uwezo wa mtu kuzaa. Hata hivyo mabusha yanaweza kuleta madhara iwapo tu kama yakiambatana na magonjwa mengine kwenye korodani.
  Kwa mfano, kama mabusha yataambatana na maambukizi (testicular infection) au uvimbe kwenye korodani (testicular tumor), yanaweza kusababisha kupungua kwa uzalishaji na utendaji kazi wa mbegu za kiume (sperms) na kupelekea tatizo la ugumba kwa wanaume.

  Hali kadhalika, iwapo sehemu ya utumbo mkubwa au mdogo imebanwa katika upenyo fulani kwenye sehemu ya ukuta wa tumbo, huweza kusababisha ngiri (strangulated hernia), hali ambayo ni hatari kama isipotibiwa haraka.

  Mkuu ninakushauri utumie Asali kijiko kimoja na na pilipili mtama kijiko kidogo kunywa itakusaidia kutuliza hayo maumivu yako na uwe kila siku unakunywa maji ya uvuguvgu kila asubuhi unapo amka glasi 3 na ukae saa moja kabla ya kunywa chai na

  wakati wa mchana uwe unakunywa maji ya uvuguvugu glasi moja na ukae saa moja bila ya kula na wakati wa usiku unywe maji ya uvuguvugu glasi 1 kisha ukae saa moja pasipo kula kisha waweza kula chakula cha usiku na wakati wa kulala wa kulala unywe

  glasi moja kisha ulale fanya hivyo kila siku itakusaidia haya maji ya uvuguvugu kwa Afya yako inshallah. Na pia uende kufanya Oparesheni ya upasuaji sio kubwa ni ndogo tu.Mkuu.@
  Delvis

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Delvis

  Delvis Member

  #19
  Feb 14, 2013
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 77
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  kaka sina cha kukulipa zaidi yakusema asante sana kwa umahiri wako..
   
 20. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #20
  May 2, 2013
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 1,956
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  pole mkuu....ngoja waje hawa wataalamu...
   
Loading...