Dawa ya migomo Tanzania hii hapa

oba

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
310
65
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na migomo ya hapa na pale na majuzi tu tumeshuhudia mgomo wa madaktari na kisha walimu ambayo madhara yake ni makubwa kwa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. ili kupata dawa ya migomo hiyo, na mingine ijayo, tujue kwa nini wafanyakazi wanagoma;

1. Maisha magumu
Hii imekuwa moja ya sababu kuu ya migomo; kitendo cha mfumuko wa bei kuwa almost 20% ukilinganisha na almost 5% miaka kama kumi iliyopita kinamaanisha kuwa mishahara ya wafanyakazi haijawahi kupanda wakati gharama za maisha zimepanda.
Chukulia mfano wa madokta, mwaka 2002 salary ya dr wa degree anayeanza kazi ilikuwa less than 200000, sasa ( last financial year) 900000 je hiyo si mara nne ya mshahara wa 2002 sawa na mara nne ya mfumuko wa bei wa sasa? hapo kuna nyongeza ya mshahara ambayo imewahi kufanywa? maisha bado ni magumu wafanyakazi wamechoka kuvumilia!

2. mgawanyo mbovu wa raslimal za taifa
Wakati wananchi na wafanyakazi wengine wanalia njaa, tabaka tawala na watu wengine walio karibu na tabaka hilo wamekuwa wakipata mgao mkubwa( ukilinganisha na wafanyakazi)wa kile kinachopatikana kutoka kwenye raslimal za taifa aidha kwa kulipana mishahara minono au malupulupu na privelages nyingine.
Tawala zilizopita ( mfano Mwl Nyerere na Mkapa) walikuwa na stratergy fulani za kugawana kilichopo
a. Mwalimu alikuwa akisema tufunge mkanda unamwona kabisa amefunga mkanda na hilo lilileta utulivu maana kila mtu aliona kuwa kama ni umaskini tunao wote, unlike tabaka tawala la sasa hivi
b. Mkapa japo utawala wake baadaye umeonekana uligubikwa na udhalimu katika maeneo kadhaa alijua namna ya kula na kipofu.....ukila na kipofu usimguse mkono... mfumko wa bei ulikuwa chini kwa kiwango ambacho maisha yalikuwa relatively fair... huku utawala huo ukifanya vitendo vya kifisadi wanachi walikuwa wanaweza kumudu maisha better than now na hilo liliwafumba macho wafanyakazi na watu wengine hata kuleta utulivu katika nchi

3. Ufisadi
Sina maana kuwa ufisadi haukuwepo katika tawala zilizopita, la hasha,...utawala wa sasa umeweka uhuru wa mafisadi kutambulika lakini umeshindwa kuwachukulia hatua wakishadhihirika, matokeo yake wanyonge wanaona wanaibiwa na watu ambao wana ubia na serikali na kuhitimisha kuwa serikali ndiyo imewatuma hao mafisadi, kumbuka; Kosa lolote lisipoadhibiwa mioyo ya watu hujawa na mbinu zaidi za kufanya kosa hilo au linalofanana nalo (MHUBIRI 8: 11)

Kutokana na maelezo hayo dawa ya mgomo ni rahisi tu;

1. Dhibiti mfumko wa bei.....hata kama watawala wabinafsi wakiendelea kuiba ( of which wataendelea tu kwa kiasi fulani hata kama mfumo utakuwa tight) maisha kama yatakuwa siyo magumu kama sasa watanzania watakuwa calm... hatujazoea fujo ni vile tu tunalazimishwa.....Simba wakati anaanza kuwinda alikuwa hajui wapi akamate, baada ya kupigwa mateke na pembe na wanyama aliokuwa akiwakamata popote akagundua kuwa sehemu sahihi ya kumkama mnyama ni shingoni penye mfumo mzima wa uhai... watanzania hawakuzoea fujo lakini mfumo mgumu wa maisha utawapelekea huko, liwalo na liwe..


2. Tatizo siyo mshahara mdogo, ni mgawanyo wa kilichopo....unafikiri kama wafanyakazi wote na watawala wangekuwa na mishahara chini ya 1,000,000 kuna lawama zingekuwepo kuwa fulani anachukua kingi? shida inakuja pale watawala wanapokuwa na mshahara ( achana na malupulup) mara kumi ya baadhi ya wafanyakazi... dawa ni kurekebisha mfumo wa mishahara hasa ya tabaka tawala ili iendane na umaskini wanaohubiri.

3. Haitoshi kumfichua fisadi kama hauwezi kumwadhibu....uwepo mfumo maalumu ulio huru na unaojitegemea wa kutoa adhabu kali kwa yeyote anayehusika kuhujumu mali na utajiri wetu, na isichukue muda mrefu mpaka watu wakasahau...instant punishment itatuliza mioyo ya watanzania wengi wanaoona kuwa wezi hawafanywi chochote.


Nawasilisha..... add or subtract anything if you want!!
 
Migomo iliyopita imeleta mafanikio makubwa sana na Mojawapo kubwa ni RAIA NA USO WA KIMATAIFA KUITAMBUA SERIKALI YA TANZANIA ILIVYO KATIRI

ISSUE YA DR ULIMBOKA IKO MPAKA UN, Mgomo baridi unaendelea raia wanazidi kuambiwa ukweli mahospitalini na wanaelewa.. Huu ni mtaji mzuri sana wa kuiondoa serikali madarakani...


NOTE: HAKUNA SERIKALI DUNIANI INAYOWEZA KUPAMBANA NA RAIA WALIOICHAGU.

MKOBA ANAHUSIKAJE WAKATI SISI WENYEWE NDO TUMEPIGA KURA? TUKIPOTEZA WEWE INAKUUMA NINI?
 
Sasbu nyingine kubwa ni uongozi mbovu... hayo uliyoyaorodhesha yanaweza kutatuliwa kwa rasilimali hizi hizi tulizonazo lakini unatakiwa uongozi mzuri tu
 
Dawa ya Migomo ni kuwa na Mwabwepande kila mkoa na kutayarisha wangoa meno wa kutosha kazi kwishney !!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Dawa pekee ya kudumu ni kuzingatia maslahi ya wafanyakazi wote nchini .Nadhani serekali na wadau wengine wana kila sababu yakuthamini MCHANGO wa Mfanyakazi katika maendeleo ya nchi.
 
Wasalaam,serikali isisubiri migomo kutatua matatizo/kero/madai mbalimbali ya wananchi ili kusikiliza/kutatua.nimeona kama vile kunatatizo la serikali kutoa majibu au ufumbuzi mbalimbali ya wananchi ukianza na la wafanya biashara,kabla halijaaisha hilo likatokea la wananchi tunduma na sasa ndio hili la madereva.katika mambo yote hayo sisi kama taifa limetuingizia hasara kubwa tu japo sio rahisi kwa sasa kuliona.kwa issue ya madereva waziri husika amelishughulikia vizuri japo nae kachelewa nampongeza sana kwa kurudisha huduma kwa njia ya mazungumzo.pia serikali iangalie utumiaji wa nguvu za polisi kuna mahala hauleti tija ,kwa mfano kwenye suala hili la madereva mabomu hayakuwa na nafasi ya kutanzua mgogoro zaidi ya kuchochea kadhalika kule tunduma.kuitikia kwa wakati kutasaidia kutatua kwa wakati na kutoa nafasi yakuendelea kujenga taifa kila mtu kwa nafasi yake. nawasilisha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom