Dawa ya Meno

KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
18,711
12,067
Wakuu nina tatizo la meno kushindwa kula vitu vya baridi au vya moto.

Nimejaribu kutumia sensodyne za aina nyingi, Aloe, whitedent harbour sijui,,lakini sina afadhali, kwani ninapotumia na kuwa fresh, lakini nikiacha kwa siku mbili tu,tatizo linajirudia.

Naombeni mwenye dawa mbadala anishauri.
 
Mkuu, mimi pia ni mwathirika wa teeth sensitivity, na ninatumia sensodyne siku zote. Sipati shida as long as naendelea na dawa hiyo.

Nadhani tatizo hili ukishalipata ni vigumu likatoweka kabisa.

Hivyo dawa ya meno aina ya sensodyne (na jamii zake) inabidi ukubali kuitumia siku zote na uachane kabisa na dawa za meno za kawaida.
 
thanx nitajaribu kwani naona colgate nyingi ni feki sana hapa kwetu yani shida hii sensodyne ni ya nchi gani
 
Pia jitahidi uwe unatumia LISTERINE MOUTHWASH mara mbili kwa cku. ni nzuri sana mm huwa inanisaidia sana, i hop nawe itakufaa.

pole sana.
 
Pole sana hata mimi colgate nikiitumiia sana inanifanya meno yangu yanapata ganzi hivyo nimeiacha baada ya daktari kunishauri nibadilishe dawa hivyo colgate naitumia pale ninapokuwa nimekwama. pia pendelea kupiga mswaki mara 2 kwa siku na maji ya uvuguvugu uyachanganye na chunvi kidogo itakusaidia hata hizo mouth wash sio lazima ukitumia hayo maji.
 
Mkuu, mimi pia ni mwathirika wa teeth sensitivity, na ninatumia sensodyne siku zote. Sipati shida as long as naendelea na dawa hiyo.

Nadhani tatizo hili ukishalipata ni vigumu likatoweka kabisa.

Hivyo dawa ya meno aina ya sensodyne (na jamii zake) inabidi ukubali kuitumia siku zote na uachane kabisa na dawa za meno za kawaida.
pia mouthwash lkini si unajua nyingi feki basi kuwa na uhakika tumia maji ya vuguvugu weka chumvi ni kinga tosha kusukutulia asubuhi na jioni na kila unapomaliza kula especialy kila unapokula vitu vya sukari.usisahau kuona dentist pia
 
Wakuu nina tatizo la meno kushindwa kula vitu vya baridi au vya moto.
Nimejaribu kutumia sensodyne za aina nyingi, Aloe, whitedent harbour sijui,,lakini sina afadhali, kwani ninapotumia na kuwa fresh, lakini nikiacha kwa siku mbili tu,tatizo linajirudia.

Naombeni mwenye dawa mbadala anishauri.
Pole sana ndugu. chukua majani machanga ya mwarobaini, changanya chumvi na yakaushie ndani pasipo na jua. yakikauka kabisa saga na tumia kupigia mswaki. waweza changanya na dawa ya mswaki sio vibaya. (Tahadhari; usipende kuuma vitu vigumu kwa kutumia meno yako, ama kufungulia vitu!!

Mungu Atakusaidia
 
thanx nitajaribu kwani naona colgate nyingi ni feki sana hapa kwetu yani shida hii sensodyne ni ya nchi gani

Ufeki wa dawa ni tatizo jingine - ambalo dawa yake kwa kweli sio sensodyne mkuu.

Sensitivity ya meno ndilo tatizo linalohitaji sensodyne au dawa za namna yake. Ila hata huko pia unaweza kupambana na sensodyne feki, ukaendelea kusumbuliwa na sensitivity.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom