Mba kichwani (Dandruff): Fahamu Chanzo, tiba na jinsi ya kuepukana nazo

Jaribu mafuta ya morgan,yanatibu mba wa kichwa kwa uzuri kabisa na yanapatikana kwa urahisi kwa maduka ya vipodozi.
 
Nilikua na sumbuliwa na tatizo kama hlo nikashauliwa nitumie mafuta ya nywele yanayoitwa Kuza.....now nashukuru umepeungua japo bado nipo kwenye dozi
 
Nilikua na sumbuliwa na tatizo kama hlo nikashauliwa nitumie mafuta ya nywele yanayoitwa Kuza.....now nashukuru umepeungua japo bado nipo kwenye dozi

Sakasaka, hayo mafuta ya Kuza upatikanaji wake ni mkubwa? na bei yake je?
Asante sana.
 
Habari JF Doctors?
naomba msaada wa kuhusu dawa sahihi ya mba au utangotango kwenye ngozi, hauwashi ila unanikera sna uko mgongoni na kwenye mabega.
 
Ndugu wana JF,

Nimekuwa nikisumbuliwa na mba (dandruff) za kichwani (scalp) kwa muda mrefu sasa na nimetumia dawa kila aina bila mafanikio. Nilianza kwa kupaka mafuta ya Whitefield lakini sikuona mabadiliko. Kisha nikameza vidonge aina ya grasiofulvin bado sikuona ahueni yoyote. Baadaye nikashauriwa kumeza vidonge aina ya ketoconazole, baada ya kushauriwa na daktari kwamba hivi vidonge ni vikali kuliko grasiofulvin nilivyotumia mwanzo. Bado tatizo liliendelea kuwepo, tena safari hii likazidi kuwa sugu zaidihata ukiwa mbali ukinitazama kichwani utadhani nimepaka ungahii ni kwa sababu ya ukoko wa mba unaochomoza kutoka kwenye ngozi ya kichwa (scalp).

Baada ya kuona tatizo limezidi ikabidi nimuone daktari wa magonjwa ya ngozi, ambapo huyu daktari alinitengenezea dawa kali kwa kuchanganya alcohol na dawa fulani ya mba. Sambamba na hii dawa aliniandikia dawa ya ketoconazole shampoo ambayo niliipaka kwa muda usiopungua mwaka mmoja. Nilitumia hadi dawa ikasiha laki bado tatizo liko palepale.

Hivi karibuni nimerudi tena hospitali daktari akaniandikia vidonge. Nilipogundua kwamba vidonge alivyoniandikia ni glusiofulvin (vidonge ambavyo vilishindwa kunitibu awali), nilivitupa vidonge hivyo jalalani. Sasa hivi nanyoa nywele kila baada ya wiki moja, tofauti na awali ambavyo nilikuwa nanyoa kila baada ya wiki mbili. Hii hali imenichanganya sana. Sijui nifanyeje. Niliwahi kwenda hadi hospitali ya St Benard kule Kariakoo nikachomwa dawa yenye mchangayiko wa salicylic acid lakini sikupata ahueni yoyote.

Wandugu, naomba mnisaidie. Anayefahamu tatizo hili naweza kuliondoaje au daktari anayeweza kulitibu naomba anielekeze. Natanguliza shukrani.
------
MAONI YA MDAU
Pole sana mkuu. Hili tatizo hata mm limenisumbua kwa muda mrefu sana pamoja na kupaka kila aina ya mafuta yakiwamo hayo ya MOVIT. Mafuta ya movit sio kwa ajili ya tiba bali ni kwa ajili ya kinga na urembo kwa akina mama (yame-contain a little amount of sulphur ambayo haiwezi kutibu mba). Ukiona mtu amepaka haya mafuta amepona, basi huyo hakuwa na mba ila harara tu.

Baada ya kuteseka na mba za kichwani (dandruff) kwa muda mrefu, hatimaye nimepata tiba kutoka Hospitali/Clinic ya Doctor's Plaza iliyopo Kinondoni Morocco, jirani na makao makuu ya Airtel. Ukifika Airtel, elekea upande wa Mashariki sambamba na barabara ya kuelekea Posta, vuka Furaha Medical Centre, kisha vuka hilo ghorofa jipya unaloliona hapo mbele, kwa mbele kidogo utaona ghorofa fupi ina maandishi yameandikwa LANCET LABORATORIES...ndani ya jengo hili (Second Floor) ndimo ilimo Clinic ya Doctor's Plaza inayofanya kazi chini ya mwavuli wa LANCET LABORATORIES yenye makao makuu Afrika Kusini.

Siku nilipoenda pale sikumkuta daktari wa ngozi lakini niliomba kuonana na daktari wa kawaida ambaye alini-prescribe dawa ya kupaka inaitwa BEPROSALIC OINTMENT na vidonge vya kumeza vinaitwa TERBIFIN. Hizi dawa zimefanikiwa kuponya tatizo langu lililonisumbua kwa zaidi ya miaka 20!

N.B: Beprosalic ointment ni dawa muhimu sana na haipatikani kwenye maduka ya dawa ya kienyeji. Kwenye maduka ya kienyeji utauziwa Beprosalic cream ambayo haina uwezo wa kutibu kama ointment. Na wafamasia wengi hawajishughulishi kuzinagtia hilo, kwa hiyo unapaswa kuwa makini wewe mwenyewe mnunuzi.
 
mkuu hilo tatizo nami limenisumbua tangu utoto lakini ghafla mwaka huu nimepona tafuta mafuta ya kupaka kichwani yanaitwa Movit mimi ndio yamemalizia tatizo langu.
 
mkuu hilo tatizo nami limenisumbua tangu utoto lakini ghafla mwaka huu nimepona tafuta mafuta ya kupaka kichwani yanaitwa MOVT mimi ndio yamemaliza tatizo langu.

Nashukuru sana ndugu yangu. Ngoja niyatafute hayo mafuta nipake- Nimeteseka sana tangu mwaka 1988 nilipopata hili tatizo--hadi nilishauriwa kupaka mikorogo nikapaka lakini wapi. Ngoja niijaribu MOVT. Thank u very much.
 
mkuu hilo tatizo nami limenisumbua tangu utoto lakini ghafla mwaka huu nimepona tafuta mafuta ya kupaka kichwani yanaitwa MOVT mimi ndio yamemaliza tatizo langu.

hata mm nitayataka hayo, yanapatikana wapi>
 
Ni kweli mafuta hayo ni mazuri kwa mba tena yanauzwa buku tatu au nne hivi. ila inabidi utumie muda wote ngozi iwe wet na anayekupalka asiwe mvivu
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom